Je, huyu askari yuko sahihi ama anataka nimpe rushwa tu?

Mkushi Mbishi

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2018
Posts
347
Reaction score
560
Habar wakuu
Kuna siku mida ya saa tatu usiku nilipita sehemu nikavamiwa na vijana wakanikaba,kunitishia silaha na wakafanikiwa kuniibia simu pamoja na pesa kidogo,nikaenda kuripoti kituo Cha polisi nikafungue kesi na kupatiwa RB.
Nikamtafuta mtuhumiwa wangu kimyakimya maana anajulikana na maskani zake zote baadhinya marafiki zangu wanazitambua na tukawa tunafanya msako mara kwa mara na marafiki zangu maana baada ya kupatiwa RB sikuweza kupata msaada wowote Tena wa kumtafuta mwizi huyo zaidi niliambiwa nikiweza kumkamata mwenyewe nimpeleke polisi ni sawa ama nitafute mwanamgambo nilmlipe akanikamtie,niliamua kumtafuta mwenye na kampani yangu.dogo alipoona Kila sehemu tumeacha ujumbe wa kumtafuta akamtumanmzazi wake arudishe simu kwa mwenyekiti wa Kijiji,na akaomba msamaha nimsamehe kwani usiku ule hakujua kuwa ni Mimi,nikapgiwa simu na m/kiti nikakabidhiwa Mali yangu nikaona poa tu acha niendelee na harakat zangu zingine nisiendelee kupoteza muda

Sasa kama baada ya kupitia miez miwili Kuna siku Kuna askari kanifuata nyumbani amepaniki anasema kwahiyo wewe unatufanya sisi maku..a,mm ni mpelelez wa kesi yako kumbe Mali yako umeipata na mbona hujarudi kutoa taarfa,nikamuambia nilikuwa bize na shughli zingine,Sasa akadai nimpe pesa akafunge jalada la kesi yangu.

Tena ananipigia simu mara kwa mara kuwa nimpe pesa ya kufunga jalada mpaka imekuwa KERO.

Mm ndio mlalamikaji,nimeibiwa nimepoteza garama katika harakati za kumtafuta mwizi wangu mpaka nimempata bila msaada wowote kutoka kwao,Leo hii anataka nimpe pesa ya kufunga jalada Tena kwa nguvu Sasa nauliza

Ni kweli utaratibu upo hivyo?
Nimpe ama nimpotezee tu,maana anatishia kuja kuniweka ndani kama sijampa pesa nimeamua tu kukaa kimya au nimripoti?
 
Kiutaratibu ulipaswa kuripoti ili jalada lifungwe .. ilhali ulishachukua rb ..
Hapo hamna namna mkuu .. we fungal jalada
 
Mara nyingi ukufungua kesi polisi uamuzi huo unatakiwa usiwe wa mihemko au hasira,sababu inabidi utambue kuwa mchakato wa kesi unapoteza fedha na muda wako pia
 
Rushwa kwa polisi ishakuwa kama desturi.

Wanapokea kwa mshtaki na mshtakiwa na kazi hawafanyi.

Usimpe hata sent 5 bro.
Wala usiende kufunga jalada.

Mtumie sms kwa simu kuwa Unaomba ufunge jalada iwe kama ushahidi.
Na yeye akujibu kwa sms kuwa anataka hela ya kufunga jalada.
(Akikupigia simu mwambie , kaka naomba nitumie sms hayo unayosema)

Mtishe kidogo ataogopa na ataacha yaishe.
 
Ila na wewe unafanya mambo kienyeji sana huyo dogo umemuqchia kirahisi sana halafu hata unreport polisi,pamoja na hayo huyo mpumbavu usimpe hela yoyote
 
Habar wakuu
Kuna siku mida ya saa tatu usiku nilipita sehemu nikavamiwa na vijana wakanikaba,kunitishia silaha na wakafanikiwa kuniibia simu pamoja na pesa kidogo,nikaenda kuripoti kituo Cha polisi nikafungue kesi na kupatiwa RB.
Nikamtafuta mtuhumiwa wangu kimyakimya maana anajulikana na maskani zake zote baadhinya marafiki zangu wanazitambua na tukawa tunafanya msako mara kwa mara na marafiki zangu maana baada ya kupatiwa RB sikuweza kupata msaada wowote Tena wa kumtafuta mwizi huyo zaidi niliambiwa nikiweza kumkamata mwenyewe nimpeleke polisi ni sawa ama nitafute mwanamgambo nilmlipe akanikamtie,niliamua kumtafuta mwenye na kampani yangu.dogo alipoona Kila sehemu tumeacha ujumbe wa kumtafuta akamtumanmzazi wake arudishe simu kwa mwenyekiti wa Kijiji,na akaomba msamaha nimsamehe kwani usiku ule hakujua kuwa ni Mimi,nikapgiwa simu na m/kiti nikakabidhiwa Mali yangu nikaona poa tu acha niendelee na harakat zangu zingine nisiendelee kupoteza muda

Sasa kama baada ya kupitia miez miwili Kuna siku Kuna askari kanifuata nyumbani amepaniki anasema kwahiyo wewe unatufanya sisi maku..a,mm ni mpelelez wa kesi yako kumbe Mali yako umeipata na mbona hujarudi kutoa taarfa,nikamuambia nilikuwa bize na shughli zingine,Sasa akadai nimpe pesa akafunge jalada la kesi yangu.

Tena ananipigia simu mara kwa mara kuwa nimpe pesa ya kufunga jalada mpaka imekuwa KERO.

Mm ndio mlalamikaji,nimeibiwa nimepoteza garama katika harakati za kumtafuta mwizi wangu mpaka nimempata bila msaada wowote kutoka kwao,Leo hii anataka nimpe pesa ya kufunga jalada Tena kwa nguvu Sasa nauliza

Ni kweli utaratibu upo hivyo?
Nimpe ama nimpotezee tu,maana anatishia kuja kuniweka ndani kama sijampa pesa nimeamua tu kukaa kimya au nimripoti?
Achana nae huyo ni mpuuzi TU ana njaa zake. Mimi nilishafungua majalada Kibao na nikiona napoteza muda kumtafuta mhalifu wangu napotezea! Hamna cha kufunga jalada Wala nini huyo ni muhuni TU!
 
Back
Top Bottom