Donda ndugu, ni nini?

Donda ndugu, ni nini?

Mzigua_255

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2026
Posts
911
Reaction score
1,860
Wakuu habari?
Nimekua nikisikia Neno donda ndugu je.? donda, ndugu linamaanisha
Kitu gani, Yani nahitaji ufafanuz kuhusu neno hili
 
Neno "donda ndugu" (au dondandugu) linamaanisha kidonda sugu, kikubwa, na kisichopona kwa muda mrefu.
Neno hili limeundwa kwa kuunganisha maneno mawili: "Donda" (jeraha kubwa) na "Ndugu" (ikimaanisha kuwa kidonda hicho kimegandana au kimeambatana na mwili wako kama ndugu wa damu asiyetaka kuondoka)
 
Umeeleza kwa uzuri sana.
Donda ndugu ni kidonda kisichopona kwa wakati muafaka. Na hivi vidonda vilikuwa maarufu sana miaka ya nyuma huko kutokana na uduni wa huduma za afya maeneo ya vijijini.

Leo hii sina uhakika kama hivi vidonda bado vipo.
 
Akili zangu sasa dah! Eti nimewaza kuwa dondandugu ni mbususu 😂🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️

agatha_ngongi_3988271865563979913.jpg
 
Umeeleza kwa uzuri sana.
Donda ndugu ni kidonda kisichopona kwa wakati muafaka. Na hivi vidonda vilikuwa maarufu sana miaka ya nyuma huko kutokana na uduni wa huduma za afya maeneo ya vijijini.

Leo hii sina uhakika kama hivi vidonda bado vipo.
Bado vipo huko vijijini
 
Bado vipo na vinatema harufu balaa

Kuna dogo nilimuona juzi tu hapo mwezi wa Saba alikua anasema sana nilipomdodosa nikagundua ana kidonda kikubwa mguuni anasema aliungua na exoust ya pikipiki tangu mwaka 2023
 
Kuna sababu ambazo zinafanya kidonda kuchelewa kupona,
Ukiwa na kisukari kidonda huchelewa kupona pia sababu sukari nyingi kwenye mzunguko wa damu huharibu mishipa midogo ya damu,hali hiyo hupelekea oksijeni na virutubisho kutokufika kwenye jeraha,pia kisukari huharibu neva na kuathiri mishipa ya fahamu na kumfanya mgonjwa asisikie maumivu ya jeraha na kidonda huendelea kua kikubwa,
Kisukari hupelekea mwili kushindwa kujenga tishu mpya za ngozi haraka kama ilivyo kawaida coz kisukari hupunguza collagen mwilini.
 
Kidonda sugu kisichopona, mtu anaweza kukaa nacho kwa miaka mingi .

Mara nyingi humpata mtu mwenye kisukari cha kurithi (Diabetes type1) awali mtu huwa mzima wa afya ila shida huanza anapopata kidonda kidogo cha kawaida kinashindwa kupona sababu ya sukari na kuanza kuongezeka ukubwa yaani kinakuwa kama tikiti maji lilopasuka.

Hivi vidonda hutembea kwenye familia au ukoo kwa sababu ya kisukari

Chanzo ni kisukari cha urithi yaani mtu anazaliwa nacho kisukari then akiumia tu kidogo tayari kidonda hakiponi hivyo basi tunasema ana donda ndungu
 
Back
Top Bottom