Don Shkuba Yupo Huru

Don Shkuba Yupo Huru

Huwez amin jumba lote lile vyumba vya kulala havifika hata vitano mzee mrangi kipind anaanza kujenga alituambia anataka kuteremsha kitu magomeni nzima hakuna
Ndani mule hatari ....
Mzee wang mtama yupo huko migo
Jmn

Ova
 
TOKA MAKTABA :

Magomeni Dar es Salaam

Lwitiko Adamson Mwakasala ‘Tiko’ au ‘Milionea Mtoto’ (pichani), polisi wakitilia shaka utajiri mkubwa alionao.

1702228695482.png
 

Milionea Mtoto Akamatwa Dar​

LAST UPDATED FEB 23, 2016
1
Share
tiko
Lwitiko Adamson Mwakasala ‘Tiko’
Stori: Makongoro Oging’ na Issa Mnally, UWAZI
DAR ES SALAAM: Tumbuatumbua majipu ya Rais John Pombe Magufuli ‘JPM’ inazidi kushika kasi nchini ambapo si serikalini tu, hata watu binafsi wako kitanzini.

Hilo limedhihirika kufuatia hivi karibuni, Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni, kumvamia na kumfanyia upekuzi mkubwa wa saa saba, Lwitiko Adamson Mwakasala ‘Tiko’ au ‘Milionea Mtoto’ (pichani) wakitilia shaka utajiri mkubwa alionao.
1702229033384.png


Moja ya Nyumba anazomiliki.
ENEO LA TUKIO

Tukio hilo lililofunga barabara ya kutoka Sinza kwenda Magomeni lilijiri Februari 15, mwaka huu kwenye jumba lake la ghorofa lililopo Magomeni Makuti jijini Dar jirani na Kituo cha Daladala cha Kwa Bi Nyau.
TAJ (4)-001
Hekalu lake jingine
UPEKUZI KWA SAA SABA

Ilikuwa asubuhi ya saa moja ambapo kikosi cha polisi kutoka Kituo cha Polisi Oysterbay kilivamia kwenye nyumba ya Tiko ambayo ni ghorofa mbili ikiwa na matawi matatu na kufanya upekuzi mkubwa huku wakitaka kujua chanzo chake cha pesa mpaka kujenga jengo hilo ambalo inasemekana linaweza kuwa hoteli, shule, hospitali au ofisi.
“Upekuzi ulikuwa mkubwa sana. Tiko alianza kupekuliwa saa moja asubuhi polisi wakiwa na mjumbe wa nyumba kumi. Kazi ya upekuzi iliisha saa nane mchana,” kilisema chanzo.
TAJ (3)-001
Magari yake yaliyokamatwa yakiwa kituo cha polisi
POLISI WAONDOKA NA MAGARI, WASHIKILIA GHOROFA

Chanzo hicho kilisema kuwa baada ya upekuzi wao, polisi walimchukua Tiko na magari yake manane kwa ajili ya uchunguzi pia wanalishikilia ghorofa hilo huku uchunguzi zaidi wa kujua anapataje pesa ukiendelea.
NI MATAJIRI WATATU
Ndani ya wiki moja sasa, inasemekana watu wengine wawili wenye fedha zao wamekamatwa akiwemo aliyejulikana kwa jina moja la Hemed, mkazi wa Mbezi Beach jijini Dar na mwingine mkazi wa Tabata ambaye jina lake halikupatikana mara moja. Wanashikiliwa na magari yao kituoni hapo kwa uchunguzi zaidi.
WANACHOFANYA POLISI KWA SASA
Kwa mujibu wa chanzo chetu ndani ya jeshi hilo, siku hizi polisi wanamfuata tajiri mmojammoja na kumfanyia upekuzi. Kama atakutwa na madawa ya kulevya, kesi anayo, akikutwa na mali ambazo asili yake au upatikanaje wa fedha haujulikani, pia kesi anayo.
UWAZI ENEO LA TUKIO
Kama ilivyo ada, baada ya kupata taarifa hizo, Uwazi lilifika eneo la tukio na kufanya mahojiano na Mjumbe wa Shina Namba 23, Muharami Daudi ambaye alikuwepo katika zoezi la upekuzi nyumbani kwa Tiko.
“Nakumbuka ilikuwa Jumatatu, saa moja asubuhi, polisi walifika nyumbani kwangu, wakajitambulisha kuwa wametoka Kituo cha Polisi Oysterbay. Wakanitaka nifuatane nao mpaka kwa Lwitiko katika zoezi la upekuzi wa madawa ya kulevya kwamba wana wasiwasi naye katika biashara hiyo.
“Tulikwenda kufanya upekuzi kwa pamoja, lakini hatukupata madawa ya kulevya hivyo polisi waliamua kuondoka na magari yake manane yaliyokuwa pale na bastola kwa uchunguzi zaidi,” alisema mjumbe huyo.
KAMANDA WA POLISI KINONDONI
ACP Christopher Fuime ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni. Katika mahojiano na gazeti hili, alikiri kukamatwa kwa Tiko na watu hao wengine.
“Bado tunawashikilia Lwitiko na Hemed kwa uchunguzi zaidi na kutafuta mtandao wao.
”Unajua kunahitaji uchunguzi wa kina ikiwa ni pamoja na kuchunguza mali zao jinsi walivyozipata kama vile nyumba. Baadhi ya magari yao tunayo hapa tunayashikilia, tunayafanyia kazi,” alisema kamanda huyo.

Source : Global Publishers TZ
 
yule mwenzie wa Tanga Yanga Omar..

Almaarufu rais wa Tanga amepambana sana kujinasua


View: https://m.youtube.com/watch?v=vTmSkr2yFvo

MAHAKAMA Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi, imeridhia maombi ya utaifishaji mali za mfungwa Yanga Omari Yanga kufuatia Maombi ya Mkurugenzi wa Mashtaka dhidi ya mfungwa huyo kuomba mali zake zitaifishwe.

Uamuzi huo uliotokana na shauri namba 1/2021 uliotolewa hivi karibuni na Jaji Elinaza Luvanda baada ya kuridhika kuwa mali za mshtakiwa huyo ni mazalia ya uhalifu uliotokana na kosa la usafirishaji wa dawa za kulevya.

Mwaka 2020 mfungwa Yanga Omari Yanga alihukumiwa na Mahakama hiyo kutumikia kifungo cha miaka 30 gerezani baada ya kukutwa na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin zenye uzito wa gramu 1052.63.

Akisoma uamuzi huo Jaji Luvanda alisema sheria inaelekeza kuwa mali zote zinazopatikana kwa njia ya uhalifu ni lazima zitaifishwe ili kutoa fundisho kwa jamii kuwa uhalifu haulipi.

Mali zilizotaifishwa na Mahakama ni Kiwanja No, 32 Block "C" Magaoni Tanga, Kiwanja namba 73 Block "A" Mwambani Tanga, Kiwanja No. 144 Block "B" Mwakidila Tanga, kiwanja namba 615 na namba 617 Block "B" Kange Tanga, Kiwanja namba 30 Block "C" Mwakidila/Magoani Tanga, kiwanja namba 605 Block "A" Mwambani Tanga na kiwanja namba 606 Block "A" Mwambani Tanga.

Mali hizo zote zipo mkoani Tanga alipokuwa anaishi mfungwa huyo.

Wakati wa usikilizwaji wa shauli hili, upande wa Jamhuri uliwakilishwa na wakili wa serikali Mwandamizi Sabrina Joshi na upande wa utetezi uliwakilishwa na Wakili Nehemia Mkoko.

Rais wa Tanga, Yanga Omari amefika hadi mahakama ya rufaa Court of Appeal Tanzania sasa labda mahakama za Afrika Mashariki na ile ya Afrika ndiyo zimebaki akitaka kujaribu kujinasua

1702229854299.jpeg

charge were proved beyond reasonable doubt and as such this appeal is
without merit and it is hereby dismissed in its entirety.
DATED at TANGA this 31st day of May, 2021.
S. E. A. MUGASHA
JUSTICE OF APPEAL
W. B. KOROSSO
JUSTICE OF APPEAL
L. J. S MWANDAMBO
JUSTICE OF APPEAL

The judgment delivered this 1st day of June, 2021 in the presence of Mr. Majura Magafu and Mr. Werehema Kibaha, learned counsel for the appellant and Mr. Pius Hilla, learned Senior State Attorney and Mr. Waziri
Magumbo, learned State Attorney for the Respondent / Republic, is hereby
certified as a true copy of the original.

F. A: MTARANIA

Sources :


Source : Yanga Omari Yanga vs Republic (Criminal Appeal 102 of 2019) [2021] TZCA 220 (1 June 2021)

Source : kutaifisha Mali
TanzLII
https://tanzlii.org › sourcePDF
In this application, the properties mentioned herein below are ...


30 Jun 2023 — That, properties mentioned in paragraph one of the affidavit was acquired in the year 1986 by the late Omary Yanga the...
 
Back
Top Bottom