Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,341
- 51,904
Habari Wakuu!
Leo Kwa habari za Burudani na Sanaa, nimekuwa nikifuatilia Tamthilia za hapa na pale za bongo kama sehemu ya kusapoti na kuona kile wakifanyacho wenzetu katika Tasnia hiyo.
Nikakutana na Dogo mmoja hivi ambaye ameigiza kwenye Tamthilia ya Pazia, namfahamu Kwa jina moja "EDU" Wataalamu mtakuja kunisaidia jina lake halisi.
Taikon kama BINGWA, tupa wa mambo ya Fasihi. Kwa jicho la kisanaa nimemuona huyu Dogo kama hataletewa zengwe, husda na kijicho basi hakuna kijana wa kumzidi wala kumfikia, nazungumzia kijana wa umri wake.
Ni muigizaji mzuri, anayejua kuigiza. Nafikiri waigizaji wakongwe na wakubwa ambao wameshaona akiigiza watajua nazungumzia Jambo Gani.
Mambo ambayo Edu anatakiwa kuyaongeza ili azidishe kipaji chake na kuifanya kazi yake iwe Bora.
1. Aongeze usomaji wa vitabu
2. Ajifunze kuzungumza Lugha ya kingereza imkolee.
3. Ajifunze kuandika Tamthilia na drama zake, kama maandalizi ya kuachiwa mikoba ya Bongomovie hapa Tanzania. Kisha atafute Waandishi na watunzi wa Riwaya na Tamthilia wavipitie na kukushauri.
4. Ajifunze Sanaa zingine kama za martials art's. Zitamsaidia katika uhusika wa filamu za mapigano na ujasusi katika miaka 10 ijayo.
5. Asome mambo magumu gumu yanayohusu Siasa, Rushwa, ujasusi, Teknolojia na ambayo yanaendana na dunia ya SASA na ijayo. Ili abaki kwenye Fomu Kwa muda mrefu. Asiwe kama Kaka zake ambao wameishia kwenye mapenzi.
6. Akae Kwa ukaribu na wasanii wakubwa wenye utulivu kama Jacob Steven, Johari(huyu dada pia ni muigizaji mzuri na anajitahidi kwenye uandaaji wa filamu, kama anamapungufu basi ni mapungufu ya kiwakati).
7. Ajifunze kuwa muongoza filamu iwe Kwa kusoma au kukaa na waongoza filamu mahiri. Au atafute waongoza filamu Wazuri kama maandalizi ya kuchukua mikoba.
Mwisho, akishaanza kuandaa filamu zake basi ajiepushe na urafiki au undugu kwenye ishu za kazi, atafute Wahusika kulingana na Scripts zinavyotaka.
Hayo ni machache Kati ya mengi.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam