Nilivyokusoma weww umeomba ushauri huku tayar una majibu yako(samahani lakini) ,alafu pia ni kama umefocus kujua anapata mkopo au la,nikwambie ukweli tu mambo ya mkopo ni mambo ya temporary mnooo...hayazid hata miaka 3 kutoka sasa,hata akipata mkopo 100% je future yake ipoje?? Mie nimesoma computer science ila sasa nafanya kaz katika shirika na kaz nayofanya haiusiani na mambo ya computer,kiufupi kibongo bongo bado sana kuitambua thamani ya hii course,yeye aende kuiridhisha nafsi yake tu ila huku awe anasomea ujuzi mwingine,ila kama ana mpango kuishi nje ya nchi kwa computer science ila deal sana,huku wanadhan kaz zetu ni microsoft word na excel,bado kampuni nyingi zinanunua software na wataalamu wanatumia wa nje zaidi,ningekuwa mimi ningemwambia asome computer alafu aongezee na knowledge nyingi za akili mnemba(AI)+ Na lugha mbili tatu za kimataifa(kifaransa,kispain,kijerumani) labda na ujuzi wa kawaida kama plumbing,umeme wa magari(future car zitakuwa za umeme),(kwa kiasi)....ushauri huu mwambie auandike kwenye diary yake miaka 15 ijayo ataelewa nimeandika nini