Malyenge
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 6,658
- 3,646
Clouds FM inafanya mahojiano na yule dogo aliyeandika bongo fleva kwenye mitihani ya kidato cha nne mwaka 2011. Dogo anadai alifanya hivyo ili kufikisha ujumbe kwa wahusika kuwa mfumo wa sasa wa elimu hautambui vipaji vya watu. Dogo anasema yeye hakuwa mtu wa kusoma ingawa alijitahidi sana. Anasema maumbile yake aliyoumbwa na Mungu si ya kusoma. Dogo anadai mfumo wa elimu Tanzania hautambui vipaji vingine zaidi ya formal education, yaani uende shule, usome kisha utafute kazi.
Anasema kuwa mfumo huu wa elimu, mtu anayeshindwa kuufuata basi mfumo unamtupa nje.....
Mashairi aliyoyaandika katika mtihani wake ni ya maelezo haya ambayo watu hawakuelewa anamaanisha nini. Dogo huyo kwa jina anaitwa JULIUS, anasema ana umri wa miaka 23, akaulizwa kwa nini alimaliza form four akiwa na umri mkubwa akajibu alikuwa akirudiarudia form two mara nyingi sana.
Anamalizia kwa kusema wazazi waangalie vipaji vya watoto wao ili wasipoteze pesa zao kwa kusomesha mtu asiye na uwezo wa kusoma. Anaomba msamaha kwa watanzania wote kwa aliyoyafanya, hakuwa na jinsi ya kufikisha ujumbe kwa jamii. Ametoa alblum yake inaitwa Mr. PRESIDENT.
Nawasilisha.