Rev. Damasus Mkenda
Member
- Dec 22, 2011
- 67
- 27
Kufanya jambo lolote bila ya kuwa na msingi wa Elimu hautafanikiwa au ukifanikiwa itakuwa ni asilimia ndogo kulinganisha kama ungekuwa na elimu. Ni vizuri huyu kijana akajua kuwa alitakiwa kuwa na msingi mzuri wa elimu walau afaulu form four, ili imjengee msingi wa kipaji chake. Kuimba hakuhitaji elimu lakini inategemea unataka kuimba nini na kwa ajili ya nani na nini. Hiyo elimu anaikataa kwa sasa lakini atahitaji hapo mbele kidogo, ndugu niwaambie Mungu akimsaidia akipata kibali kwa wakubwa na mataifa mengine atafanyaje??? Ni kweli kusoma sio kuelimika lakini kuna mambo ya msingi kwamba destiny yako ni mpaka uiandae. Watoto wangu tayari najua vipaji vyao au talanta zao siwezi kuwaruhusu saa hizi eti waanze (masaa yote) kucheza mpira wa miguu, muziki, kareti, ngumi, nk wakati hata elimu ya kufuta ujinga yaani Form four hawajafika. Napalilia vipawa vyao na wakati ukifika wakijua mwelekeo sahihi I will release them and one day i will say that is my product. Kawaida watoto hufanya kabla hawajafikiria lakini sisi wakubwa tunafikiria kwanza ndio tunafanya na mtoto anahitaji kusaidiwa to seize their dream.
God Bless You.
God Bless You.