Mtumishiwetu
Senior Member
- Jul 13, 2022
- 187
- 334
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso ameweka jiwe la msingi katika mradi wa maji katika Kata ya Dabalo Wilayani Chamwino Mkoa wa Dodoma ambapo ametoa pongezi nyingi Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) na kwa kampuni ya PLASCO inayotengenenza matanki makubwa ya plastiki yaliyotumiwa katika mradi huo ikiwa ni kwa mara ya kwanza inatumika katika miradi ya maji nchini.
Waziri Aweso ameahidi kuwa Serikali itaendelea kutumia teknolojia hiyo badala ya ile ya kujenga kwani inatumia muda mfupi wa wiki mbili tu kuyaweka katika chanzo cha maji na yanadumu kwa muda mrefu wa zaidi ya miaka 70.
Mradi huo unaogharimu zaidi ya shilingi milioni 907 unatekelezwa na RUWASA chini ya Ofisi ya Meneja wa Mkoa wa Dodoma na Wilaya ya Chamwino kwa fedha za Mfuko wa Taifa wa Maji ambapo mkandarasi anayeujenga ni Medes Company Limited na unatarajiwa kuhudumia wakazi 8,134 utakapomilika Julai 30, 2022.