Waziri Aweso Asema "Tusizoee Shida za Wananchi Twendeni Tukafanye Kazi"

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
943

WAZIRI AWESO - TUSIZOEE SHIDA ZA WANANCHI TWENDENI TUKAFANYE KAZI

Waziri Wa Maji Mhe.Jumaa Aweso ametoa wito kwa Bodi mbili zilizozinduliwa leo kusimamia utendaji na ufanisi katika kutekeleza majukumu ya kikazi.

Akizungumza baada ya kuzindua Bodi ya RUWASA na Bodi ya Mfuko wa Maji Waziri Aweso amewahihiza watendaji wa sekta ya Maji na Taasisi hizi kutozoea changamoto za wananchi ikiwa ni sambamba na kuepuka kufanya kazi kwa mazoea bali kujidhatiti na kufanya kazi kubwa ili kukidhi matarajio ya wananchi.

Aidha, Aweso amewataka watendaji Wa Mfuko Wa Maji Wa Taifa Kubadilika Kiutendaji na Kutokufanya Kazi Kwa Mazoea, na Badala Yake watumie Teknolojia Kwa Ajili ya Kufanya Mageuzi Na Urahisishaji Wa Utendaji Katika Kazi.

"Lazima Tuangalie Mifuko Mingine wanafanyaje Kazi Kwa Mfano: Mfuko Wa Barabara wanafanyaje. Tubadilike Tusifanye Kazi kwa mazoea.”

Aweso Ameyasema Hayo Leo Juni 27 akizindua Bodi Ya Mfuko Wa Taifa Wa Maji Na Bodi Ya Wakurugenzi ya Wakala Wa Maji Na Usafi Wa Mazingira Vijijini (RUWASA) atika ukumbi wa PSSF Jijini Dodoma.

Katika hatua nyingine Waziri Aweso amesema Mfuko wa Maji ni kichocheo kikubwa ya Utekelezaji wa miradi ya Maji hivyo kuitaka Bodi hiyo kwenda kutengeneza vyanzo vingine vya mapato ili kuweza kujiendesha na kutokutegemea zaidi Fedha ya Serikali.

"Tunamshukuru Sana Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, Hakuna hata mwezi mmoja hatupati Fedha. isiishie tu hii Fedha ambayo tunayoipata ya serikali hivo tuangalie sasa tukatengeneze vyanzo vingine vya Mapato.

"Mbona Kuna Asasi Za Kiraia (NGO'S) zinapata Fedha na zinafanya Kazi Vizuri kwenye Miradi ya Maji.
Huu Mfuko tuangalie namna gani tunaweza tukawaomba wadau mbalimbali tuone ni jinsi gani ya kuweza Kuongezea kuliko ilivyosasa ambapo Chanzo Chake Kimebaki Hicho hicho" Amesema Aweso.

Aidha, Waziri Huyo Amewasisitiza watendaji wa RUWASA kuwa kila anatakiwa kufanya kazi Kwenye nafasi yake ili kuhakikisha wananchi vijijini wanafikiwa na huduma ya Maji kupitia RUWASA ambayo imepewa dhamani hii muhimu na watanzania wana matarajio makubwa.

Akiizungumzia RUWASA, amekiri kuwa tayari kazi kubwa ya utekelezaji wa Miradi mingi vijijini imefanyika na sasa ni wakati wa kusimamia uendelevu wa miradi hiyo ili iendelee kuwa na tija na kutoa huduma kwa wananchi.
 

Attachments

  • Fzov5IHacAAoBpE.jpg
    Fzov5IHacAAoBpE.jpg
    48.5 KB · Views: 4
  • Fzov5IIaEAEE8Jz.jpg
    Fzov5IIaEAEE8Jz.jpg
    128.3 KB · Views: 5
  • Fzov5IRaUAMsxg5.jpg
    Fzov5IRaUAMsxg5.jpg
    112.5 KB · Views: 4
  • Fzov5IPaYAEMhpY.jpg
    Fzov5IPaYAEMhpY.jpg
    98.7 KB · Views: 5
  • Fzr8WORaAAEn7RA.jpg
    Fzr8WORaAAEn7RA.jpg
    86.5 KB · Views: 5
Back
Top Bottom