figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,492
- 54,895
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Onesmo Lyanga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amebainisha kuwa Jeshi hilo linaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo.
Chanzo: Radio One
=======
Watu watano wa familia moja wakazi wa kijiji cha Zanka wilayani Bahi Mkoa wa Dodoma wameuawa na watu wasiojulikana.
Waliouawa ni mume, mke, watoto wawili na mjukuu mmoja wote wa familia moja.
Mdogo wa baba wa familia hiyo, Noah Kapande amesema miili hiyo iligunduliwa na watoto waliokwenda kufungua ng'ombe jirani na nyumba hiyo jana Jumamosi saa 10 jioni baada ya kusikia harufu.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka akiongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo amewataka wakazi wa kijiji hicho na ndugu kutoa ushirikiano ili waliofanya kitendo hicho wajulikane.
“Hili jambo litakuwa limefanywa kwa ushirikiano na watu wa hapa hawezi kuja mtu kutoka huko kwenye nyumba ya mtu akaua watu watano asiwe na mwenyeji hapa,”amesema.
Ameagiza vyombo vyote vya ulinzi na usalama na uchunguzi vya mkoa kuhamia katika kijiji hicho kufanya uchunguzi wa tukio hilo na waone namna ya kushirikiana na wenzao kama italazimika kufanya hivyo.
“Ni lazima hawa watu wapatikane ni lazima.labda wananzaka muwe wanafiki naomba wananchi watoe ushirikiano…, hii ni damu ya watu watajisema tu,” amesema.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Onesmo Lyanga amesema madaktari wanafanya uchunguzi miili hiyo na baada ya uchunguzi watakuwa na nafasi ya kusema watu hao waliuawa kwa namna gani.
“Polisi tunaendelea kufanya uchunguzi tunatarajia tutawapata waliohusika na hili tukio lakini kwa sasa bado mapena kusema nani kahusika moja kwa moja,” amesema.
Mwananchi