Dodoma: Mwenyekiti akutwa ameuawa na kutupwa mtaroni

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,568
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kisokwe wilayani Mpwapwa, Mkoa wa Dodoma, Patrick Nyangauya amekutwa amefariki dunia na mwili wake kutupwa kwenye mtaro na kufunikwa na majani.

Akizungumza leo Jumatano Januari 17, 2024 kijijini hapo, Mtendaji wa Kijiji cha Kisokwe, Anna Fundichuma amesema alipigiwa simu na mwalimu kuwa kuna maiti imeonekana pale shuleni.

“Nikawasiliana na viongozi (bila kuwataja) ambao walikuja na baada ya kufunua mwili tukagundua ni mwenyekiti wa kijiji chetu. Ni huzuni kubwa imetukumba,” amesema.

Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho, Patrick Msumba amesema hawawezi kufahamu sababu hasa ya mauaji hayo na kwamba si mara ya kwanza kitokea mauaji kama hayo.

Alipotafutwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno ameahidi kumrudia mwandishi baada ya dakika moja, lakini baada muda simu yake iliita bila majibu.
 
Kijijini ukisikia mtu anakwenda kutoa mashtaka kwa mwenyekiti wa kijiji ni sawa na mtu kwenda International Court of Justice pale The hague, wenyeviti wa vijiji wapewe ulinzi kutokana na kesi wanazo kutana nazo mfano wakulima na wafugaji inaweza kuwa risk kwao. Mijini wenyeviti tunawachukulia poa.
 
Back
Top Bottom