Dodoma: Spika Ndugai amfukuza Bungeni Salome Makamba

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565
Spika Job Ndugai amemfukuza bungeni kwa siku saba kuanzia leo, Mbunge wa Viti Maalum, Salome Makamba (Chadema), baada ya mbunge huyo kulieleza Bunge kuwa marekebisho ya Kanuni za Kudumu za Bunge yatafanyika kwa matakwa ya Spika, Naibu Spika na watu wao.

"Spika Job Ndugai amesema ametumia miaka 20 ya maisha yake bungeni na amekutana na watu wema na changamoto nyingi sana. “Baadhi huuliza najisikiaje kumaliza bunge la 11 salama, jibu langu sifa apewe bwana wa majeshi” "Wakati mwingine mnisamehe ninapokutana na mtu mjinga"

"Nilipokuwa chuo cha MWEKA Moshi, nilikuwa mmoja wa Wanafunzi maskini sana, baadhi ya likizo sikuwa na nauli za kurudi Kongwa, nakumbuka jinsi ambavyo wenzangu walivyokuwa wakipanda magari kuondoka mimi nilikuwa najificha kwa aibu ya kuulizwa huna kwenu?"- Spika Ndugai.

"Leo nimekuja na rafiki yangu, Mama umenivumilia sana,hata nilipokuwa ICU India alikuwa analala pembeni yangu masaa 24 amekaa kwenye kiti, amekuwa Daktari wangu muda wote, hakika wewe ni mke mwema,kwa kukopa maneno ya Dk Mpango Asante sana kwa kunipa raha"
 
kweli mkuu, mi hata mada imenipotea!
Mkuu umetupia ishu Kama 4 hivi kwa pamoja hata kuchangia kunakuwa kugumu kidogo Ila yote kwa yote sidhani Kama Ni sawa kumfukuza mbunge Tena wa upinzani kwa kusema maneno tofauti na spika.

Alafu kabisa mzee baba anasema amemaliza bunge la 11 salama! Hivi ingekuwaje ndio angesema hajamaliza salama?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kila mtu akisema umasikini wake hali itakuwaje? Ccm wakumbuke huo umasikini wao wa Zamani bado ungalipo.
 
Hivi kila mtu akisema umasikini wake hali itakuwaje? Ccm wakumbuke huo umasikini wao wa Zamani bado ungalipo.

Ndugai ana faili Mirembe. Ni kichaa. Hakustahili kuwa Spika. Ndiyo maana ni dhaifu kuliko Maspika wote waliopita.
 
Back
Top Bottom