Source : NifahamisheMWANAFUNZI wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Miyui mjini Dodoma amelazimika kuacha shule baada ya kupata ujauzito huku akishindwa kutambua baba wa mtoto aliyepo tumboni kwa maelezo kuwa alikuwa na mahusiano wa mapenzi na watu saba akiwemo mwalimu wake.
Inadaiwa kuwa kati ya hao saba aliokuwa na mahusiano mmoja alikuwa ni mwalimu aliyekua akifundisha katika shule hiyo.
mzazi wa mwanafunzi huyo alipombana kwa kumuhoji kuhusu mtu aliyempa ujauzito huo mwanafunzi huyo alikataa kumtaja hadi akaamua kumpeleka kwa uongozi wa shule hiyo na huko akatoa siri kwa kuwaeleza kuwa hajui nani aliyemtia mimba kwa kuwa alikuwa na uhusiano na wanaume saba kwa wakati mmoja.
Chanzo cha habari cha kuaminika kutoka Ofisi ya Elimu ya Manispaa ya Dodoma kilithibitisha kupewa ujauzito kwa mwanafunzi huyo, na kwamba yupo nyumbani kwao na kuongeza kuna wanafunzi wengine watano wa shule hiyo ambao ni wajawazito nao wameacha shule.
Tutafika?
Last edited by a moderator: