Dodoma mji unaoongoza kwa masista wengi

Dodoma mji unaoongoza kwa masista wengi

Kondoa darasa linaweza lisiwe na mkristu, au yuko mmoja tu. Nakumbuka shule ya Miningani kwenye darasa letu la wanafunzi 73 A & B, Wakristu tulikua wawili tu. Shule nzima tulikua 23.
unamfahamu mwalimu Comorrow?
 
Wadau nimebahatika kutembea miji/makao makuu ya mikoa karibia yote Tanzania ukiacha Zanzibar tu.Katika udadisi wangu nimegundua mji wa Dodoma una masista wengi(Catholic nun)kuliko mji mwengine wowote apa Tanzania.

Ukitembea maeneo ya katikati ya mji hadi pembezoni mwa mji na manispaa ya Dodoma ni kitu cha kawaida sana kukutana na Masista hawa wakiwa wanatembea au wapo kwenye magari yao.

Japo huku Dodoma ndio kitovu cha Kanisa la Anglican lakini ama kwa hakika Wakatoliki wamejiimarisha pia.Inasemekana masista wengi wanatoka Kondoa-Irangi pamoja na Usandawe kwani Warangi na Wasandawe wanapenda sana Usista na Upadre kuliko Wagogo(Ni nadra sana kukuta Sista mgogo).

Uwepo wa Mashirika ya kitawa ya Kikatoliki Dodoma kama vile waPassionist,St Donbosco,St Gema ,Damu Azizi Ya Yesu n.k kumechangia Dodoma kuwa na Masista wengi.

Shalom Dodoma!
Sista afu Mrangi? Dodoma kunafaa kutimiza ndoto zangu kwa kweli...
 
Back
Top Bottom