Wadau nimebahatika kutembea miji/makao makuu ya mikoa karibia yote Tanzania ukiacha Zanzibar tu.Katika udadisi wangu nimegundua mji wa Dodoma una masista wengi(Catholic nun)kuliko mji mwengine wowote apa Tanzania.
Ukitembea maeneo ya katikati ya mji hadi pembezoni mwa mji na manispaa ya Dodoma ni kitu cha kawaida sana kukutana na Masista hawa wakiwa wanatembea au wapo kwenye magari yao.
Japo huku Dodoma ndio kitovu cha Kanisa la Anglican lakini ama kwa hakika Wakatoliki wamejiimarisha pia.Inasemekana masista wengi wanatoka Kondoa-Irangi pamoja na Usandawe kwani Warangi na Wasandawe wanapenda sana Usista na Upadre kuliko Wagogo(Ni nadra sana kukuta Sista mgogo).
Uwepo wa Mashirika ya kitawa ya Kikatoliki Dodoma kama vile waPassionist,St Donbosco,St Gema ,Damu Azizi Ya Yesu n.k kumechangia Dodoma kuwa na Masista wengi.
Shalom Dodoma!