Kuna taarifa zinatembea mitandaoni kuwa bashe, Malima na musukuma wamefukuzwa/ wamevuliwa uananchama wa ccm. Kama ni kweli ccm haitakiwi kufika huku. Demikrasia IPI mnayoihubiri Kwa wananchi wenu km watu ambao mnapingana nao mnawavua uanachama.
Bashe kwa nafasi yake ya ubunge bungeni huwa anaibrand ccm sana bungeni.!! Kuwafukuza wakina bashe ni kuonekana chama hakina misingi imara. Chama kikubwa lazma kiwe mfano wa mambo mazuri.
Kama ni kweli hawa wamefukuzwa mjiangalie upya !! Uchaguzi umepita tokea 2015 lakini mpaka leo bado mnatibu majeraha ya uchaguzi..
Kiongozi mzuri ni yule anayewaungasha watu wote wasiompenda na wanaompenda.
Haiwezekani eti waliomuunga mkono lowasa mpaka Leo bado ni maadui wa chama. Mnakosea sana. Na hapa ndiyo mnadhihirisha uafrika wenu. Afrika tunafanya maamuzi yetu Kwa kuangalia hisia zaidi badala ya ueledi, ujuzi na busara. Fukuza fukuza haisaidii chama wala haiongozi kura za 2020 kwenye uchaguzi.
Uongozi wa chama ni tofauti na serikali, uongozi wa chama lazma uwe very diplomatic na mwenye busara sana..kwenye chama lengo kubwa ni kuongeza wanachama na supporter wengi..!! Kwahiyo kiongozi ni yule anayewauunganisha watu wote. Sophia simba amesema hatogombea tena, sasa kwann mmemfukuza uanachama.
Kinana wewe ni katibu mkuu, ebu yaepushe haya na mshauri vyema bosi wako.
Huwez ongeza wanachama Kwa kufukuza fukuza.