DODOMA: Bashe, Musukuma na Malima waachiwa

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,599
6,669
Wameachiwa muda si mrefu usiku huu.

Nini wamehojiwa?

Kwanini wameachiwa?

Nini hatma yao?

Tutajua baadae. Ila wako huru sasa!
========

Kulingana na taarifa ya kamanda wa polisi mkoa wa Dododma, wahusika walikamatwa kwa kufanya vurugu katika vikao vya chama cha mapinduzi vinavyoendelea mjini Dodoma.
 
Yaaani walichofanyiwa ni sawa na enzi zetu unaenda kuruka ukuta uingie kutazama mechi huku hauna hata mbuni, afu Bahati mbaya ukiingia tu ndani baada ya kuruka ukuta unakuta askari hawa hapa na mbwa zao,
walichokuwa wanafanya askari wale ni kuwarukisha kichura chura na kuwagonga virungu 2 -3 vya ugoko na kisha kukupa /kuwapa adhabu ya kukaa unaangalia ukutani au kulala chini huku mechi inaendelea kama kawaida, afu mchezo ukibakiza dk10 za mwisho ndo wanawaachieni mkaangalie game, hapo huwa wanafungulia hata mageti yote kipindi hicho .

Kuingia uwanjani muda huo wa lala salama tulipenda kuita kwa jina maalufu la " kipindi cha fungulia mbwa" . Ila pia ubaya wake ilikuwa ni kukasrika sana masela wakikutania kuwa uliingia fungulia dog time, kwani ilikuwa ni fedheha sana, na hivyo ilimlazumu muhusika kufanya jitihada za kujichanganya na walioingia toka mwanzo na pia kuleta leta ubishi ili tu apate dondoo za DK za mwanzo ili asije pata aibu ya kutoelewa game ilivyokuwa toka mwanzo. Ikiwemo kutaka kuoneshwa wachezaji maarufu kama kina peter manyika, chambua, mayay, mwameja,jembe ulaya,madaraka Suleiman, ili walau awe na cha kusema (asiwe Tomaso).

Sasa hawa jamaa Nimeona wamefanyiwa hivyo hivyo ila tofauti yake tu wao ni kwenye siasa.
Kwani maamuzi yashafanyika na wenye kuvuliwa gamba tayari washavuliwa. Hivyo na wao ndo wanaibuliwa DK za lala Salama toka.machimbo.
Au mwasemaje wakuu..??
 
Back
Top Bottom