Dodoma: Baraza kuu la TAG lamtunuku Rais Magufuli tuzo kwa namna alivyoongoza Taifa kukabiliana na Korona

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,507
8,136
Punde Rais Magufuli atakuwa hapa Miyuji mjini Dodoma na kunatarajiwa kuwa na mazungumzo baina yake na baraza kuu la kanisa la TAG leo ikiwa ni kilele cha mkutano mkuu wa kanisa ambalo limetimiza miaka 81 tangu kuingia nchini. Nini kutaenda kuzunguzwa? Kaa nami nitakujuza.

=======

10:20 AM: Kwa sasa kwaya ipo kwenye stage ikiimba nyimbo kadhaa wakati Rais Magufuli akisubiriwa afike.

10:39 AM: Rais Magufuli amewasili katika eneo hili la chuo cha biblia

11:10 AM Baraza kuu la Kanisa la TAG kwa kauli moja kwenye kikao chake cha siku tatu limemtunuku Rais Magufuli tuzo maalum ya heshima kwa kutambua jinsi alivyoongoza Taifa kumtegemea Mungu kipindi kigumu cha janga la korona wakati mataifa mengine yakiweka nguvu kwenye kuwazuia watu wao wasitoke majumbani na kufunga shughuli mbalimbali za kuletea mataifa yao Maendeleo, yeye akafanya jambo tofauti kabisa duniani.

Askofu mkuu wa TAG amesema Rais alilielekeza taifa kufunga na kuomba siku tatu mfululizo na kanisa la TAG kuamua kufunga kwa siku saba na baadae kurudia saba. Baadae akaeliekeza Taifa limshukuru Mungu kwani bwana ametenda.

Askofu Mtokambali amesema Rais Magufuli amewezesha kamwe Taifa lisiyumbe kiuchumi kwa janga la Korona jambo ambalo limewagusa kama kanisa na wanamuombe Mungu ambariki kwa kumtanguliza yeye katika uongozi wa Taifa.

Anasema yeye amekula chumvi na hajaona katika historia ya Marais jinsi ambavyo amemuweka Mungu kwanza na mengine baadae.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma: Nawakaribisha Dodoma ambayo ni makao makuu kivitendo na makao makuu kisheria. Niwakumbushe waumini wenzangu, mafanikio haya makubwa ya kuhamishia serikali Dodoma ni moja ya kazi kubwa iliyotakokana na maombi yenu pale makanisa, waumini na watanzania wote mlipokesha mkiomba 2015 tukampata Rais wetu, Dkt Magufuli, mwenye maono, uthubutu na haya matokeo makubwa ni kwa maombi yetu tuliyoyafanya.

Hii miradi mnayoiona mahala pengine inatokea baada ya miaka 20, 40 na 50 lakini hapa imetokea ndani ya miaka 5. Ni maajabu na ajabu lingine mahala pengine yanatokea kwa kukopa fedha, hapa kwa fedha zake za ndani za watanzania.

Wote ni mashahidi ndio kiongozi wa kwanza Tanzania anamaliza miaka mitano hajakanyaga Ulaya, kumbe inawezekana na sasa hivi watu suala la Ulaya hawaliongelei tena.

Waumini wenzangu, kwa maombi yenu mlimpa ushirikiano mheshimiwa Rais tukaomba pamoja mwenyezi Mungu akatuepushia mbali corona, wote ni mashahidi.

Jana niliporudi nyumbani kijana wangu akanimbia baba nilikuwa naangalia TV channel ya CNN jana imetangaza kwa lugha ya hapa kwamba Tanzania is the best and safety destination for Tourism in the world. Mwenyezi Mungu ametupenda na ametupendelea.

Askofu mkuu TAG (Dkt. Barnabas Mtokambali): Sisi hapa Dodoma makao makuu ya nchi pamoja na wewe leo kunatukumbusha moja ya kazi nzito ambayo serikali yako imefanya, kutimiza ndoto ya baba wa taifa na ndoto ya kitaifa ya kuhamishia makao makuu ya nchi hapa Dodoma.

Mwanafalsafa wa uongozi na utawala, Joel Becker aliandika 'Vision without action is merely a dream, action without vision just passes the time bu vision with action can change the world'.

Naipongeza serikali imeongeza na kudumisha nidhamu kwa watumishi wa umma na kupambana na rushwa, ilifikia hatua kila mtu serikalini anafanya anavyosikia yeye with no concreate supervision and accountability, anamjibu mwananchi kile anachotaka na kuuza huduma kwa wananchi hata zile ambazo ni stahiki yao.

Tumejiwekea Malengo ya kujenga chuo kikuu Dodoma, kwa neema ya Mungu tumefanikiwa kupata ekari 560 maeneo ya Chigongwe tangu mwaka 2009 kupitia serikali ya kijiji na mamlaka ya CDA, bado mchakato wa kumilikishwa hujafikia mwisho tunaomba msaada wako.

Kuhusu uchaguzi mkuu, tunatambua kwamba 28/10 mwaka huu nchi yetu itakuwa na Jambo muhimu sana la uchaguzi mkuu, kwanza tunashukuru sana wewe kuwa Rais wetu, serikali tangu miaka ya 70 tukiomba kwamba uchaguzi usifanyike siku ya ibada hatimae kupitia kwako Mungu amejibu dua zetu, tumepokea tarehe ya uchaguzi ambayo itakuwa siku ya Jumatano kwa furaha tele, na tunakushukuru sana wewe kwa kuitangaza siku ya Jumatano kuwa siku ya mapumziko.

Ni matumaini yetu uchaguzi huu utaendeshwa kwa haki na amani kupata viongozi bora kwa taifa letu. Wahenga wanasema dalili ya mvua ni mawingu, tumeanza kuziona dalili nzuri za mvua za uchaguzi huru na haki hasa kupitia mchakato wa wagombea ndani ya vyama vyetu vya siasa ambao umeonekana kuwa na uwazi na kidemokrasia sana.

Tunaomba serikali yako inadumisha uwazi huu katika uchaguzi mkuu yaani kuhesabu kura na kutangaza matokeo kufuate utaratibu mzuri wa kwenye vyama ili pasitokee na nafasi kwa wale wepesi wa kudhani kuwa kila wanaposhindwa wameibiwa kura kuweka mazingira ya amani katika hali ya utete.

Rais Magufuli: Nakushukuru sana baba Askofu mkuu pamoja na viongozi wengine kwa kunialike, ni heshima kubwa kwangu na nilipoingia kwenye ukumbi huu nimeuona uwepo wa Mungu katika ukumbi huu.

Nawashuru kwa tuzo mliyonipa, napenda nikiri haikunistahili mimi, hiyo tuzo ni ya Mwenyezi Mungu alietujaalia kutokomeza gonjwa hili la korona lakini nashukuru sana zawadi hii imenigusa, imenigusa sana. Nawashukuru sana kwa upendo huu mkuu na tuombane wote na hasa sisi viongozi ili nisije kupata kiburi cha shetani ya kujiona mimi wa maana sana kuliko wengine bali nikasimame na kuendelea kumtumikia Mungu na kumtegemea yeye.

Nilipopokea mwaliko wako awali nilishtuka, ulieleza mlinialika ili nije kuongea na baraza kuu la kanisa. Nikajiuliza mimi ni nani, mimi mwanasiasa, niliwahi hata kuwa padri lakini nikashindwa. Sasa nimealikwa kwenda kuzungumza na maaskofu na wachungaji, nitaenda kuwaeleza nini? Mimi ndio natakiwa kuelezwa na kuombewa, natakiwa kuwa mpokea neno kutoka kwenu, baadae nikalikumbuka neno la bwana katika kitabu cha Yeremia, Yeremia alipotumwa kwenda kuhubiri, alimjibu bwana yeye hajui kusema lakini bwana akanena naye na kusema tazama nimetia maneno yangu kinywani yangu na ndio sababu nikakubali mwaliko huu. Historia ya kanisa hili hapa nchi ni nzuri sana, lilianzia Mbeya.

Napenda nikupe moyo na kusisitiza na bahati nzuri mkuu wa mkoa amelisikia kwamba mna eneo ambalo mnataka kujenga chuo kikuu, nataka nikuhakikishie askofu mkuu, tuko pamoja na wewe.

Na mimi nafikiria msingeishia tu kwenye kujenga chuo kikuu lakini mnaweza kutenga tena eneo lingine mkaanzisha viwanda hata kama ungeanzisha kiwanda cha kuchimba chuma kule Mmanga lakini viwanda vile vikawa chini ya TAG kwa sababu hakutakuwa na wizi wa msumari, chumba hiko kiko wazi.

Mheshimiwa mkuu wa mkoa ni jukumu lako kuhakikisha amri kutoka kwa Mungu ya baba Askofu mkuu kwa sababu waliagizwa watakayofungua duniani yamefunguliwa na Mungu.

Tulimtanguliza Mungu kama mnavyofahamu ugonjwa huu ulizusha hofu sio tu hapa nchi bali duniani kote. Na leo nimeshukuru sana nilipoingia humu sijamuona mtu amevaa barakoa, ningeshangaa sana kwamba ni nani huyo mchungaji ambae hamuaini kristo kwamba ni mponyaji. Ninani asietambua nguvu ya Mungu wakati umeshika biblia unaenda kuhubiri kanisani.

Kwa hio siku zote Mungu lazima atangulie mbele, nyinyi mmethibitisha hilo, asanteni sana na ndio maana nasema kwa dhati nilipoingia hapa nimemuona Mungu yuko hapa. Sisemi kwa unafiki.

Tumeshinda na Mungu ametusikia pamoja na kejeli nyingi tulizozipata sisi watanzania tumeweza kushinda ugonjwa huo na sasa nchi yetu ipo salama.

Nimewashukuru sana wageni wetu kutoka Sweden na USA, asanteni sana kwa kuja na nina uhakika sasa mnaweza kuthibitisha kwamba na Mungu hakuna kinachoshindikana.

Natamani muende na kuwaambia ushuhuda kazi nzuri iliyofanywa na Mungu Tanzania kama mfano. Na ninawashukuru sana hawa wageni na wao hawakuvaa barakoa na kwa sababu wanamtanguliza Mungu Mbele katika mambo yao.

 
Back
Top Bottom