Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba anatarajia kusoma bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2022/23 leo Juni 14, jioni bungeni. Bajeti inayopendekezwa ni Tsh. Trilioni 41.9 ikiwa ni ongezeko la 16% ukilinganisha na bajeti ya mwaka wa fedha 2021/22.

Kati ya matarajio ya bajeti ya mwaka 2022/23 ni Pamoja na ongezeko la bajeti ya kilimo kwa 155% na ongezeko la kima cha chini cha mishahara. Pamoja na chanzo kipya cha mapato cha kodi ya huduma za mtandaoni.

Kwa taarifa Zaidi kwa yatakayopatikana endelea kufuatilia uzi huu Mwigulu akianza kazi yake bungeni.


=======

Waziri wa fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba tayari ameingia Bungeni na ameanza kusoma bajeti



Pamoja na Hotuba hii, nawasilisha vitabu vinne vinavyoelezea kwa kina Bajeti ya Serikali:
  • Kitabu cha kwanza ni makadirio ya Mapato
  • Kitabu cha pili ni Makadirio ya Matumizi ya kawaida kwa Wizara, Idara zinazojitegemea na Wakala za Serikali
  • Kitabu cha tatu ni Makadirio ya Matumizi ya Kawaida kwa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mtaa
  • Na kitabu cha Nne ni Makadirio ya Matumizi ya Maendeleo kwa Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba: Mwaka 2021/22 Mapato yaliyokusanywa TRA ni Tsh Trilioni 17.20 lengo likiwa Tsh Trilioni 21.78, Mapato yasiyo ya kodi Tsh Trilioni 2.3 lengo likiwa ni Tsh Trilioni 3.05, Mapato ya Hamashauri ni Tsh Bilioni 759. lengo likiwa Tsh Trilioni 863.9

Mwigulu Nchemba: Hadi Aprili 20, 2022 Deni la Serikali lilikuwa Tsh Trilioni 64.44 sawa na ongezeko la 14.4%, deni la nje ni Tsh Trilioni 47.07 (67.8%)

Deni la Nje lenye masharti ya Kibiashara ni Tsh 14.2, hivyo sehemu kubwa ya mikopo ya nje ni mikopo yenye masharti nafuu

KUFUFUA UCHUMI
Bajeti ya mwaka huu imelengwa kufufua uchumi kutokana na madhara yaliyopatikana kwenye UVIKO19 na Vita vya Urusi na Ukraine. Imelenga kuboresha ukusanyaji wa mapato

Kuna mapato ya serikali bado yanaingia kwenye mifuko ya watu. Hii inatokana na suala la makadirio ya juu ambapo kichoongezeka huingia kwenye mifuko binafsi. Wananchi wasiotoa rushwa ndio hukadiriwa makadirio ya juu na kutishiwa kufilisiwa.

Pia wafanyabiashara sio waaminifu kwa kuwa na bei ya risiti na bei isiyo ya risiti ambapo bei isiyo ya risiti huwa nafuu Zaidi. Lakini tabia zote hizo ni uhujumu uchumi

WATUMISHI WAHUJUMU UCHUMI WATAFUKUZWA
Watumishi watakaobainika kula rushwa na kuhujumu uchumi hawatahamisha vituo bali watafukuzwa kazi. Wala watu wasidhani kuwa vijana waliohitimu hawana haki ya kuingia katika ofisi za umma

Kwenye suala la uadilifu tunao uwezo wa kufukuza hata ofisi nzima na kuajiri watu upya. Anayetaka kumjaribu mama na amajaribu

KUBANA MATUMIZI
Mkakati wa kubana matumizi 2022/23 tutabana matumizi yasiyo ya lazima.

Ununuzi wa magari utafuata waraka wa serikali, ambapo tutaangalia aina ya magari na aina ya matumizi ya magari. Gharama kubwa hupatikana kwenye ununuzi wa magari, mafuta na vipuri vya magari. Safari za ndani na nje zitapunguzwa

Tutapunguza uwakilishi kwa vikao vya ndani na nje
Tutapimiana mafuta
Uchambuzi wa wastani wa mafuta utafanywa kutegemea ulazima wa majukumu na umuhimu
Utaratibu wa kuwakopesha wafanyakazi wenye hadhi ya kukopeshwa na serikali, umependekezwa kuwa utaratibu wa kununua magari yao wenyewe, na kununua vipuri wenyewe

MFUMO WA MANUNUZI YA UMMA
Tutaacha mfumo wa manunuzi wa umma kwa sababu haujaleta tija kwa kuwa bei zinazotangazwa huwa ni bei kubwa kwa jumla na rejareja, bei huwa kubwa kulliko bei ya soko. Manunuzi yatafuata mchakato ili kudhibiti matumizi.

Bei za manunuzi zitakuwa na ukomo, ili kuwa na ukomo wa bei ili mfumo wa TANEPS usiwe na bei uliozidi bei ya soko kwenye kupata zabuni

TEHAMA KUONDOA MATUMIZI YA KARATASI
Napendekeza TEHAMA iwe chaguo namba moja ili kuondoa matumizi ya karatasi. Suala la kutotumia karatasi bunge wameweza. Kumbi za mikoa ziwe na mifumo ya kimtandao ili kuweza kufanya vikao virtually

Tutaendelea kuboresha manunuzi ya umma katika mfumo wa elektroniki na kuweka ukomo wa bei za bidhaa zinazotumika zinakuwa na ukomo wa bei itakayotumika Serikalini, ili kuzuia ambao wakiona ni Serikali wanapandisha bei

Utaratibu wa kuita Wakuu wa Mikoa, Wilaya, Idara, Hamashauri kuja kukaa mahali kusikiliza ni mzigo mkubwa kwa walipa kodi, tumekopa fedha nyingi kwa ajili ya mkongo wa taifa lakini bado tunatumia gharama kubwa kufanya kazi ‘manually’

Mtu anasafiri siku 4, anaacha kuhudumia wananchi kwa jambo ambalo anaweza kulifanya kwa nusu saa, kwa karne hii jambo hilo sio muafaka

Mahakama wameonesha Tehama inawezekana kw akuendesha kesi kupitia mtandao, lazima tutumie vizuri

CAG AONGEZWE FEDHA
Napendekeza CAG aongezewe fedha ili apate Watumishi wa kutosha ili aweze pia kuhamisha watumishi kutoka idara moja kwenda nyingine pindi anapohitaji,ametengewa fedha kama alivyoomba

Rushwa imesababisha miradi kuwa chini ya viwango, fedha zimeenda kwa watumishi wasio wazalendo, mradi ukisainiwa wanaanza kugawana fedha kabla ya mradi

Tunaimarisha ukaguzi wa fedha, tutawabaini wazembe, tutawakamata na tutawafunga

MSHAHARA UZINGATIE NAFASI HUSIKA
Mtumishi wa Umma atakeyeteuliwa kwenye nafasi za kuteuliwa baadaye akatenguliwa nafasi aliyoteuliwa basi arejee kwenye mshahara ule wa awali kabla hajateuliwa.

Kumlipa mtu mshahara wa nafasi ambayo hayupo tena (aliyokuwa ameteuliwa) ni kuwabebesha mzigo mkubwa Watanzania. Mtu akitenguliwa mara moja na mshahara alipwe ule wa nafasi aliyokuwa awali.

Unaweza kukuta nchi ina wizara 25 lakini lakini ina Makatibu Wakuu 50 au zaidi

Unaweza ukakuta tuna halmashauri 184 lakini ukakuta tuna Wakurugenzi 300 au zaidi. Na hivyo hivyo kwa taasisi nyingine kwasababu waliotolewa wanaendelea kulipwa kama bado wapo ofisini

USAILI KWA USHINDANI (WAKUU WA MASHIRIKA YA UMMA)
Kwa mashirika ya umma yanayofanya kazi kibiashara yafanye kazi kibiashara na kupunguza mzigo kwa serikali. Wakuu wa mashirika wa umma wafanyiwe usaili kwa ushindani badala ya teuzi kama awali. Imezoeleka mashirika kuwa bila bodi, wakati mwingine bodi na menejiment huwa na urafiki na kukosa uwajibikaji wa kutosha

KUFUFUA SEKTA YA UVUVI
Sekta ya uvuvi tumeiongezea fedha ili kuongeza pato la taifa, kutakuwa na usambazaji wa boti 250 za kisasa za fiber ili kufufua Shirika la Uvuvi

WATUMISHI WA BENKI WASIO WAAMINIFU
Kuna watumishi wa Benki sio waaminifu, wanapenda kitafuta wateja haraka ili kuuza dhamana za wateja, wanauza kwa thamani ambayo aihusiani, hili linawatia umasikini Watanzania

Vyombo vya usalama vifuatilie minada inapofanyika

Napendekeza kutenga Tsh bilioni 8 kwa ajili ya watoto wanaotoka katika familia masikini, ambapo kwa sasa Madiwani, Wabunge na watu wengine wamekuwa wakifuatwa kuombwa misaada

KUFUTA ADA KIDATO CHA 5, 6
Elimu ya ufundi itaimarishwa, tuna vyuo 77 vya VETA

Elimu ya kidato cha 5 na 6 kuna vijana wa vijijini wanapata shida kuendelea na masomo kwa kuwa hakuna shule za juu katika baadhi ya Kata, ili kupunguza gharama napendekeza kufuta ada kwa wanafunzi wa Kidato cha 5 na 6

MALIPO YA WATUMISHI NA WASTAAFU
Rais ameongeza mshahara wa kima cha chini kwa 23%, ameboresha viwango vya posho, tutaendelea kulipa madeni ya watumishi

Serikali pia imeridhia kuongeza malipo ya mkupuo wastaafu kwa 33% badala ya 25% iliyopendekeza mwaka 2018

WAJASIRIAMALI
Serikali itaendelea kutenga maeneo ya miundombinu kwa wajasiriamali wadogo, Rais atatoa Tsh milioni 10 kila mkoa ili kuimarisha uongozi wa Wamachinga na ofisi zao

Pia kuna Tsh Bilioni 45 ya mikopo kwa Wamachinga na miundombinu

MAPENDEKEZO YA MABORESHO YA MFUMO WA KODI, ADA, TOZO
Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye vifaa na mitambo ya hali ya hewa vinavyoingizwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA). Hatua hii inalenga kuimarisha mifumo ya utendaji kazi kwa kutumia vifaa vya kisasa kutabiri hali ya hewa kwa ajili ya mipango sahihi na usalama wa Taifa

- Huduma za Mtandaoni
Kufanya marekebisho ya Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, SURA 148 ili kuiwezesha Serikali kukusanya Kodi ya Ongezeko la Thamani katika biashara mtandao (digital services) bila kuathiri uwajibikaji chini ya Sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 332.

Marekebisho haya yanalenga kurahisisha utaratibu wa usajili wa walipakodi wanaotoa huduma za kidijitali bila ya kuwa na makazi hapa nchini (simplified registration).

- Simu janja
Kufuta msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye simu janja za Mkononi (Smartphones). Hatua hii inalenga kuiongezea Serikali mapato kiasi cha Shilingi milioni 33,705

Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye malighafi za kutengeneza mbolea

- Uzalishaji wa mbolea
Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye malighafi za kutengeneza mbolea. Hatua hii inalenga kutoa unafuu kwa wazalishaji wa mbolea na kuvutia uwekezaji nchini.

- Zana za uvuvi
Kusamehe kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye nyavu za kuvulia. Lengo la hatua hii ni kukuza wavuvi wadogo na kuchochea ukuaji wa Sekta ya Uvuvi

- Uingizaji na Uzalishaji
Kupunguza ada ya leseni kwa wazalishaji na waingizaji wa bidhaa zinazotozwa Ushuru wa Bidhaa kutoka shilingi 500,000/= hadi shilingi 300,000/=. Hatua hii inalenga kuwapa unafuu wazalishaji na waingizaji wa bidhaa hizo pamoja na kusaidia kurejesha ukuaji wa Sekta baada ya athari za UVIKO19 na athari zinazotokana na msukosuko wa kiuchumi duniani.

- Kilimo/Mazao
Kusamehe Ushuru wa Mazao kwenye mbegu (seeds). Hatua hii inalenga kuwapa unafuu wakulima na kuongeza tija kwenye uzalishaji mazao mbalimbali

-Mazao ya Misitu
Kupunguza Ushuru wa Mazao ya misitu (forest produce cess) kutoka asilimia 5 hadi asilimia 3. Lengo la hatua hii ni kupunguza 109 gharama kwa wafanyabiashara wa mazao ya misitu na kukuza sekta ya misitu

- Fidia kwa Wafanyakazi
Napendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kwa kupunguza kiwango cha mchango kwa sekta binafsi kutoka asilimia 0.6 inayotozwa sasa hadi asilimia 0.5 ya mapato ghafi ya wafanyakazi. Lengo la hatua hii ni kuleta usawa katika uchangiaji kati ya wafanyakazi wa sekta binafsi na wa umma.

- Mifumo ya Malipo
Kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Mifumo ya Malipo ya Taifa kwa kupunguza tozo ya muamala kutoka kiwango kisichozidi shilingi 7,000 hadi kiwango kisichozidi shilingi 4,000 katika kila muamala wa kutuma au kutoa pesa. Punguzo hili ni sawa na asilimia 43 ya kiwango cha sasa. Lengo la 113 hatua hii ni kupunguza makali ya maisha kwa mtanzania hasa katika kipindi hiki cha changamoto kubwa ya kiuchumi na kuweka usawa katika utozaji wa tozo hiyo.

- Mafuta ya kula
Kurejesha utozaji wa Ushuru wa Forodha wa kiwango cha asilimia 0 kutoka kiwango kilichokuwa kinatumika cha asilimia 25 kwenye mafuta ghafi ya kula

-Taulo za Watoto
Kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 35 kwa mwaka mmoja kwenye taulo za watoto (Baby Diapers) zinazotumbulika kwa HS code 9619.00.90. Lengo la hatua hii ni kulinda viwanda vinavyozalisha bidhaa hii nchini, kuongeza ajira pamoja na mapato ya Serikali

- Matumizi ya King'amuzi
Kuanzisha utaratibu wa kutoza ada ya shilingi 1,000 hadi 3,000 kwenye ada ya matumizi ya king’amuzi kulingana na kiwango cha matumizi.

- Kazi za Sanaa
Napendekeza kuanzisha tozo ya asilimia 1.5 kwenye vifaa vinavyotumika kuzalisha, kusambaza, kudurufu na kutunza kazi za Sanaa, uandishi na ubunifu mwingine kama vile muziki, filamu, vitabu, picha na aina nyingine za kazi za ubunifu. Hatua hii inatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 9,600

Bunge laongezewa Bilioni 5
Serikali inatambua uzito wa majukumu ya Bunge na hivyo itaendelea kuhakikisha kwamba Bunge linawezeshwa kifedha na kujengewa uwezo ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake ya msingi ya kutunga sheria, kushauri na kusimamia Serikali.

Kwa kulitambua hilo, katika mwaka wa fedha 2022/23, Bunge limeongezewa kiasi cha shilingi bilioni 5 kwa ajili ya matumizi mengineyo ili kuwezesha utekelezaji wa majukumu yake ikiwemo kuwajengea uwezo wabunge ili waweze kuisimamia vizuri Serikali.

Serikali pia imeongeza bajeti ya mfuko wa Jimbo ili kuwawezesha wabunge kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za kuchochea maendeleo katika majimbo yao.

BILIONI 20 KUONGEZWA OFISI YA MWENDESHA MASHTAKA MKUU WA SERIKALI

Serikali imeongeza kiasi cha shilingi bilioni 20 kwenye bajeti ya Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali kwa ajili kugharamia mashahidi wa makosa ya jinai na ujenzi wa vituo jumuishi 64 vya utoaji haki na kutafsiri sheria nchini

MKOPO WA TRILIONI 1.165 KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI

Bajeti Kuu imeonesha kuwa mnamo mwezi Juni 2022, Serikali ilisaini mikataba ya kusambaza maji kwa miji 28, ambazo ni fedha mkopo wenye thamani ya dola za Marekani milioni 500 kutoka Exim bank - India

Kati ya fedha hizo dola milioni 35 sawa na 85,585,000,000 kati ya hizo zitatekeleza miradi ya maji Zanzibar
 

Attachments

  • BAJETI YA SERIKALI KUU KWA MWAKA 2022 23_14_06_2022.pdf
    1.5 MB · Views: 32
Kabla ya dhalimu kuingia madarakani na kuanza kuleta siasa za kiki, watu walikuwa wanavutiwa na bunge, na hata siku ya bajeti ilikuwa na mvuto. Ila alivyoligeuza bunge kuwa kibogoyo, na akanajisi uchaguzi wa 2020 hakuna mtu anayejitambua anafuatilia tena hilo bunge. Inshort hakuna mtu anafuatilia kinachoendelea huko bungeni, hivyo msome bajeti, msisome hakuna anayejali.
 
Kabla ya dhalimu kuingia madarakani na kuanza kuleta siasa za kiki, watu walikuwa wanavutiwa na bunge, na hata siku ya bajeti ilikuwa na mvuto. Ila alivyoligeuza bunge kuwa kibogoyo, na akanajisi uchaguzi wa 2020 hakuna mtu anayejitambua anafuatilia tena hilo bunge. Inshort hakuna mtu anafuatilia kinachoendelea huko bungeni, hivyo msome bajeti, msisome hakuna anayejali.
Bora uangalie hata maigizo lakini siyo huu uchafu wao
 
Ngoja tutasikiliza ili tutambue muelekeo wa taifa. Wavutaji wa sigara na wanywa bia tunasubiri kwa hamu.

Ikiwapendeza VAT Ishuke ata 16%
 
Kama maendeleo ni kuzunguka sana nje ya nchi, hiyo nchi ya Oman kiongozi wao mkuu huwa anafanya ziara wapi?
 
14 June 2022
Muscat, Oman

Tanzania na Oman zakubaliana kupitia mikataba maalum (tax treaties) kukabiliana na wakwepa kodi za mapato pia kuzuia Masuala ya Double Taxation

The Sultanate of Oman does not levy any taxes on personal income, including income from capital gains, wealth, death or property. However, Personal Income Tax (PIT) regime is being evaluated by the Government following its inclusion in the 2020-2024 Medium Term Fiscal Plan

Oman, Tanzania sign pact to avoid double taxation​

Oman Tuesday 14/June/2022 09:25 AM
By: Times News Service
Oman, Tanzania sign pact to avoid double taxation




Muscat: An agreement was signed between the Sultanate of Oman and Tanzania on the avoidance of double taxation and the prevention of tax evasion on income.

Oman News Agency (ONA) said: "The Ministry of Foreign announces that an agreement has been initiated between the governments of the Sultanate of Oman and Tanzania on the avoidance of double taxation and the prevention of tax evasion on income
 
Kabla ya dhalimu kuingia madarakani na kuanza kuleta siasa za kiki, watu walikuwa wanavutiwa na bunge, na hata siku ya bajeti ilikuwa na mvuto. Ila alivyoligeuza bunge kuwa kibogoyo, na akanajisi uchaguzi wa 2020 hakuna mtu anayejitambua anafuatilia tena hilo bunge. Inshort hakuna mtu anafuatilia kinachoendelea huko bungeni, hivyo msome bajeti, msisome hakuna anayejali.
Bora uangalie hata maigizo lakini siyo huu uchafu wao
Ikitokea , nasema ikitokea mishahara ikipanda nyie muendelee kupokea ya zamani
 
Hii bajeti naona fedha kwa ajili ya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha ni nyingi sana, ambazo kimsingi zilipaswa ziwe located kwenye miradi mipya!
 
Back
Top Bottom