kibogo
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 9,739
- 4,746
Nimeona kupitia taarifa ya habari ITV wakizungumzia juu ya hali za watoto mkoani Dodoma kuwa kwa sasa 56% ya watoto wote umri chini ya miaka 5 wamedumaa.
kiuhalisia mtoto anapodumaa ni wazi kuwa atakuwa na upungufu wa kiakili na kimwili na makuzi yake yatakuwa katika hali hiyo je ni kizazi cha aina gani kinachotengenezwa huko? je hawa tunaowaona kwa sasa ni watu wazima sio na wao wamekuwa katika hali hiyo?
Tuangalie sifa za Dodoma kama ninavyoziandika hapa chini:-
1. WABUNGE WOTE NI KUTOKA CCM
2. MADIWANI WOTE NI KUTOKA CCM
3. WENYEVITI VITONGOJI ZAIDI YA 95% NI CCM
4. WENYEVITI WA VIJIJI ZAIDI YA 95% NI CCM
5. MAKAO MAKUU YA TANZANIA NI DODOMA
6. MAKAO MAKUU YA CCM NI DODOMA
kwa sifa hizi ni wazi wanaowasababishia hali hiyo ni hao hapo juu.

Asilimia 56 ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano mkoani Dodoma, wanakabiliwa na ugonjwa wa utapiamlo sugu au udumavu kutokana na kutokula vyakula bora.
Hali hiyo inachangia kuathiri mfumo wa ukuaji wa mwili na ubongo na kusababisha watoto hao kukabiliwa na uwezo mdogo wa kufikiri.
Akizungumza katika mafunzo ya lishe ya mboga za asili katika kijiji cha Vikonje Manispaa ya Dodoma, Ofisa Lishe wa manispaa hiyo, Stella Kimambo, alisema kumekuwapo na tatizo la watoto kutopata lishe bora ndani ya siku 1,000, hali inayochangia hali hiyo.
Alisema siku 1,000 za mtoto akiwa tumboni na baada ya kuzaliwa, mama anatakiwa kupata vyakula vyenye viini lishe vya kutosha kwa kula mboga za asili ambazo husaidia mtoto kukua vizuri.
Kimambo alisema endapo suala hilo litaendelea kufumbiwa macho, hali hiyo itaathiri ustawi wa uchumi wa mkoa huo kwani tayari dalili zimeanza kujionyesha za kuwapo na ufaulu mdogo wa watoto shuleni.
Aidha, aliitaka jamii kuacha tabia ya kuweka magadi wakati wa kupika mboga za majani kwani husababisha kuondoa Vitamin A na C kwenye mboga hizo.
Naye Ofisa Lishe Kitengo cha Kilimo katika manispaa hiyo, Praxeda Kashaija, alisema jamii inakabiliwa na tatizo la magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo yanatokana na kudharau matumizi ya vyakula vya asili.
Alisema vyakula vya asili vina virutubisho vingi mwilini na vinapatikana kwa wingi nchini, lakini kwa sasa jamii haitumii na kusababisha kupata magonjwa hayo ambayo yanatajwa kuongoza kwa vifo.
CHANZO:NIPASHE