Azathioprine
JF-Expert Member
- Sep 16, 2013
- 589
- 380
Nadhani sio sahihi sana kuhusisha siasa (CCM) moja kwa moja na Hali ya utapiamlo(kudumaa kwa watoto) mkoani Dodoma.
Ukifanya utafiti Leo watoto wengi nchi hii wana utapiamlo. Hii ni kweli sehemu kubwa ya Kusini Jangwa la Sahara.
Swali la msingi hapa.. Nini chanzo/visababishi vya utapiamlo kwa watoto wetu wengi?? Naamini utafiti huu utakua umeweka wazi chanzo kulingana na dodoso zake.
Kwa mara kadhaa Elimu duni ya huduma kwa watoto ikiwemo utoaji wa lishe na makuzi imeonekana ni chanzo cha kudumaa kwa watoto wengi. Hata hapa DSM. Nenda Leo Hospitali ya Mwananyamala/Amana/Temeke/ Muhimbili Wodi ya watoto asilimia kubwa ya watoto mule wana Utapiamlo. Ukitoa dodoso kufanya utafiti wa chanzo utagundua wazazi/walezi wengi hawana stadi bora ya kuhudumia watoto kwa lishe kulingana na umri wao.