Do Zombies and Vampires Exist?

Zombie ni neno linalotokana na lugha ya Ki Haiti (zonbi; North Mbundu: nzumbe), wakimaanisha animated corpse, maiti inayotembea.

Hizi simulizi za kuwepo hivi viumbe zipo karibia tamaduni nyingi tangia kale... Hata hapa Tanzania wanaitwa kwa majina tofauti tofauti kulingana na lugha ya kabila fulani, kwa mfano zombie wanajulikana kwa jina maarufu la ndondocha au msukule.

Kuna ambao wanajaribu kuwatofautisha kati ya ndondocha na msukule, wanasema kuwa tofauti kati ya viumbe hivi viwili ni:
Ndondocha ni watu waliorogwa na kubadilishwa akili zao kuwa kama watumwa na wakajikuta wanafanya mambo ya ajabu ajabu.
Msukule kwa upande mwingine ni watu ambao wanaaminiwa kuwa wamekufa lakini kumbe wamechukuliwa kwa madawa ili kumtumikia mganga, mchawi, au mwanamazingara Fulani.

Msukule ndio hao kwa kwa Kiingereza wanaitwa "Zombie" lakini bado wanawatofautisha kati ya msukule na zombie, wanasema kuwa Zombie kwa utamaduni na hadithi za kimagharibi, yaani nchi za ulaya ni watu walioukuwa wamekufa lakini wakarudi wakiwa nusu wafu na wasio na akili timamu. Lakini Msukule ni watu ambao hawajafa kabisa ila wamefanywa waonekane wamekufa na binadamu wengine.

Kiukweli kile unacho kiona kwenye filamu za vampire na zombies ni simulizi tu za kutaka kuburudisha watu si mambo ya kweli, japokuwa wanaweza kushabihisha na matukio ya kweli.

Mawazo ya kufikiria kuwa kuna misukule au zombie ni mawazo ya zamani sana, watu wa ulaya waliamini kuwa wafu wana uwezo wa kufufuka na kuja kusumbua watu walio hai, na hii ni kutokana na wivu waliokuwa nao hao wafu, au wakati mwingine hurudi kuja kutafuta haki walizo dhurumiwa n.k. Sasa ili kuwatisha na kuwafanya wasiwe na uwezo wa kurudi ndio kukabuniwa hizi nguo nyeusi ili kuzitisha roho zinazotaka kurudi duniani.

Ni sawa na hadithi za Halloween, sherehe inayofanyika kila mwaka mwishoni mwa mwezi wa October (tarehe 31). Hii ni sikukuu ambayo usheherekewa usiku kabla ya ile sikukuu ya watakatifu wote, kwa ufupi halloween ni sikukuu ya wafu (Mizimu). Na ilianza miaka 2000 iliyopita uko Ireland, lakini imekuja kuwa maarufu sana kwa nchi za ulaya na haswa ikiusisha uvaaji wa nguo za ajabu ajabu, na uchomaji wa moto na mapambo majumbani.

Mwanzoni ilisemekeana wafu/mizimu walikuwa wakija kusumbuwa watu duniani, na haswa waliharibu mazao, ambayo yalivunwa kipindi cha joto na kuwekwa akiba kwa ajili ya kipindi cha baridi (Winter), sasa ili kuwababaisha wasitambuwe nani ni nani ndio wakabuni haya mambo ya kuvaa kama maiti zilifukuriwa ili kuwachanganya hao magosti.

Lakini wengine wanasema kuwa, uvaaji wa nguo nyeusi misibani ni kweli unatokana na utamaduni wa kimagharibi, na haswa Roma ya kale, (ancient Rome), wao walikuwa wakivaa aina ya nguo inayojulikana kwa jina la toga, ni aina ya shuka ndefu nyeusi inayokadiriwa kufika futi 20 (6 m) kwa urefu wake. Ambayo uzungushwa mwilini, toga ilivaliwa na wanaume na wanawake walivaa stola.

Na wengine wanasema kuwa chanzo cha nguo nyeusi kuvaliwa msibani ni pale malkia Victori, alipokuwa akiomboleza kifo cha mumewe alikuwa akivaa nguo nyeusi tu na alivaa kwa muda mrefu sana.

Hii ilipelekea raiya nao kuvaa kila wanapopata msiba ya watu wanao wapenda.
 
images
 
Zombies cannot exist sababu ile post mortem decomposition inaharibu structure ya mwili. Mfano muscle za mapaja zikianza kuoza na kupungua atashindwa kusimama na kupiga hatua ili atembee. He won't be able to carry himself.

Vampires exist in the sense that kuna watu wanahitaji kunywa fresh blood to survive, wengine can't stand sun light or they would die, wengine tena change skin color haraka sana when exposed to sun light. A combination of the three diseases has never been observed. Any patient of these three category is not dangerous to other people and they don't live in a vampire society. Last: haviambukizwi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom