Do Zombies and Vampires Exist?

nachukia sana picha za hawa jamaa, viti vya kufikirika vinanikera sana !

Mbona idea ya allah/mungu ni ya kufikirika na kusadikika lakini bado unaikumbatia kwa nguvu zako zooote...acha unafiki.
 
I belive vampire walikuwepo n zombiez too ! Ukiperuz bout Vampire utapata jibu na aim yao kubwa ilikuwa damu hiyo ilikuwa miaka ya nyuma sana enzi za bibi zetu hakukuwa na Vampires but kulikuwa na Mumiani hawa nao walikamata watu usiku kuwatoa damu na kuwaua!

Nowdays yote hayo ni story lakin watu wanatoa kafara za damu nawote tunalijua hilo about zombiez sijui kitu lakin kuna story za misukule watu walanyama za watu!

Nadhani tupende kuwa wadadis homework muulize mama au baba au mzee yeyote kuhusu Mumian atakupa hadhiri yaukwel but waliaminishwa kuwa damu inapelekwa hospital the weekpoint about the stories
 
Isee Broo, uko juu sana rafiki yangu, BRAVO SANA
Zombie ni neno linalotokana na lugha ya Ki Haiti (zonbi; North Mbundu: nzumbe), wakimaanisha animated corpse, maiti inayotembea.

Hizi simulizi za kuwepo hivi viumbe zipo karibia tamaduni nyingi tangia kale... Hata hapa Tanzania wanaitwa kwa majina tofauti tofauti kulingana na lugha ya kabila fulani, kwa mfano zombie wanajulikana kwa jina maarufu la ndondocha au msukule.

Kuna ambao wanajaribu kuwatofautisha kati ya ndondocha na msukule, wanasema kuwa tofauti kati ya viumbe hivi viwili ni:
Ndondocha ni watu waliorogwa na kubadilishwa akili zao kuwa kama watumwa na wakajikuta wanafanya mambo ya ajabu ajabu.
Msukule kwa upande mwingine ni watu ambao wanaaminiwa kuwa wamekufa lakini kumbe wamechukuliwa kwa madawa ili kumtumikia mganga, mchawi, au mwanamazingara Fulani.

Msukule ndio hao kwa kwa Kiingereza wanaitwa “Zombie” lakini bado wanawatofautisha kati ya msukule na zombie, wanasema kuwa Zombie kwa utamaduni na hadithi za kimagharibi, yaani nchi za ulaya ni watu walioukuwa wamekufa lakini wakarudi wakiwa nusu wafu na wasio na akili timamu. Lakini Msukule ni watu ambao hawajafa kabisa ila wamefanywa waonekane wamekufa na binadamu wengine.

Kiukweli kile unacho kiona kwenye filamu za vampire na zombies ni simulizi tu za kutaka kuburudisha watu si mambo ya kweli, japokuwa wanaweza kushabihisha na matukio ya kweli.

Mawazo ya kufikiria kuwa kuna misukule au zombie ni mawazo ya zamani sana, watu wa ulaya waliamini kuwa wafu wana uwezo wa kufufuka na kuja kusumbua watu walio hai, na hii ni kutokana na wivu waliokuwa nao hao wafu, au wakati mwingine hurudi kuja kutafuta haki walizo dhurumiwa n.k. Sasa ili kuwatisha na kuwafanya wasiwe na uwezo wa kurudi ndio kukabuniwa hizi nguo nyeusi ili kuzitisha roho zinazotaka kurudi duniani.

Ni sawa na hadithi za Halloween, sherehe inayofanyika kila mwaka mwishoni mwa mwezi wa October (tarehe 31). Hii ni sikukuu ambayo usheherekewa usiku kabla ya ile sikukuu ya watakatifu wote, kwa ufupi halloween ni sikukuu ya wafu (Mizimu). Na ilianza miaka 2000 iliyopita uko Ireland, lakini imekuja kuwa maarufu sana kwa nchi za ulaya na haswa ikiusisha uvaaji wa nguo za ajabu ajabu, na uchomaji wa moto na mapambo majumbani.

Mwanzoni ilisemekeana wafu/mizimu walikuwa wakija kusumbuwa watu duniani, na haswa waliharibu mazao, ambayo yalivunwa kipindi cha joto na kuwekwa akiba kwa ajili ya kipindi cha baridi (Winter), sasa ili kuwababaisha wasitambuwe nani ni nani ndio wakabuni haya mambo ya kuvaa kama maiti zilifukuriwa ili kuwachanganya hao magosti.

Lakini wengine wanasema kuwa, uvaaji wa nguo nyeusi misibani ni kweli unatokana na utamaduni wa kimagharibi, na haswa Roma ya kale, (ancient Rome), wao walikuwa wakivaa aina ya nguo inayojulikana kwa jina la toga, ni aina ya shuka ndefu nyeusi inayokadiriwa kufika futi 20 (6 m) kwa urefu wake. Ambayo uzungushwa mwilini, toga ilivaliwa na wanaume na wanawake walivaa stola.

Na wengine wanasema kuwa chanzo cha nguo nyeusi kuvaliwa msibani ni pale malkia Victori, alipokuwa akiomboleza kifo cha mumewe alikuwa akivaa nguo nyeusi tu na alivaa kwa muda mrefu sana... Hii ilipelekea raiya nao kuvaa kila wanapopata msiba ya watu wanao wapenda.

Unaweza kupitia link hizi hapa chini kwa habari za hao zombie na vampire.
Zombie › News in Science (ABC Science)
Zombie
Ghoul
Golem
folk_magic
Jiang_Shi
Mind_control
wiki/Vampire
 
Yes, they do exists, tena hapa Tanzania wapo wengi tu,
Zombies ndio Wanachama wa CCM yaana hawajitambu kabisa, wanapelekwa pelekwa tu. Wao kanga na ubwabwa ndo kila kitu.
Vampires ndiohao mafisadi wanyonya uchumi wetu bila haya na ukiwagusa tu wanaweza kukupoteza kwa kasi ya kufa mtu.
Kuwa makini Mkuu, hata hapo ulipo now wapo around wengi tu.
This section is not about politics bwana, be serious.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom