Do we need a Price Regulatory Authority in Tanzania?

Chapakazi,

Hujanielewa my point nikienda kumuuliza muuza duka kwanini pale Mlimani City anauza kiatu laki mbili na nusu wakati huko anapokinunua hadi hapa ni $60 the rest inaenda wapi anaweza kunieleza? Supply and Demand are forces of determining prices ila there has to be some form of regulatory mechanism kuhakikisha this does not go out of control. Mkisema free market iache tu kujitambua yenyewe unaweza kukuta suppliers (wauzaji kama hawa) wakaform a cartel wakapunguza usambazaji kwa nia ya kupandisha bei juu. Na hili ndio linalotokea kwasababu wauzaji wengine huwa wanafahamiana. Wateja wako scattered na hawawezi kuwa na umoja kutokana na kutofautiana in their purchasing power. Consumer protection agency ndio umoja wao inaweza kuangalia whether there is value for their money katika bei zinazopangwa. Kwasasa bei nyingi za tanzania ziko kwa kiwango cha kutisha na sio kila mtu anajua mahali kulipo na alternative option.

hapo pekundu ndo maana nasema unavuka mipaka. Ukiongelea kuhusu forming cartel, papo hapo competition law inaingia. There is an imaginary line ambayo lazima mtu avuke.
By the way...example yako ya mlimani city sio nzuri maana huyo anaweza kukwambia kuwa ana costs kibao. Kama jengo, wafanyakazi na administration costs zinazopandisha bei ya hicho kiatu juu. Jaribu kuanzisha biashara uone...
 
Nadhani wewe ndio unahitaji kurudi darasani ukasome kwanza nini maana competition, fraud na price regulations.

Competition inajumuisha kuhakikisha market iko competitive na kuprevent unfair trading katika market. Na hilo linajumuisha both at domestic and international perspective kuhakikisha traders do not abuse or monopolise local markets. Tutajuaje kama wauzaji wa madukani na importers huungana katika kusetup prices for their own interest? Wafanyabiasha wengi hata machinga huwa wanafahamiana na wengine hukaa pamoja na kuzungumzia namna gani wakubaliane kupanga bei kwa manufaa ya kwamba wasipoteze wateja na kuhakikisha wanaendelea kupata faida kubwa. Swali ni nani anaweza kuwazuia hawa wasiwaumize wananchi wa kawaida jibu hakuna. FTC huwa inafanya kazi hiyo in US, in UK wana Office of Fair Trading, Federal Cartel office Ujerumani, Conseil de la concurrence France na kwengineko. Hebu soma Act hizi:-

Section 1. Every contract, combination in the form of trust or otherwise, or conspiracy, in restraint of trade or commerce among the several States, or with foreign nations, is declared to be illegal. Every person who shall make any contract or engage in any combination or conspiracy hereby declared to be illegal shall be deemed guilty of a felony, and, on conviction thereof, shall be punished by fine....

Section 2. Every person who shall monopolize, or attempt to monopolize, or combine or conspire with any other person or persons, to monopolize any part of the trade or commerce among the several States, or with foreign nations, shall be deemed guilty of a felony, and, on conviction thereof, shall be punished by fine...."


Hivyo basi ninapoenda kutaka kununua kiatu pale mlimani city nikakubali kukinunua inamaana tushatengeneza mkataba ambao unaendana na kuaminiana kuwa bei nayonunulia ni value for the money I am paying for. Ikiwa muuzaji amenidanganya au kuhadaa hiyo ni conspiracy na hivyo amepoteza uaminifu kwa mteja. He or she is subjected to civil lawsuit. Na hivyo basi muuzaji wa kiatu pale mlimani city anakuwa liable ikionekana amedanganya katika uuzaji wa vitu kwa bei isiyo halali kwa jamii.

Mdondoaji,
1. Price regulation kuzuia monopolies na collusion zipo na sipingi. Kuna hizo chache hapa kama Samatra nk umetajiwa.
They are good.

2. Hizo sections mbili ulizoweka hapo zina-deal na ishu za competition law - i.e: restrain of trade na monopoly.
Nashindwa kuelewa ni jinsi gani mwenye duka pale Mlimani City anaweza kuwa amevunja hii sheria hata kwenye nchi zilizoendelea.
Huo mkataba ambayo section 1 inaongelea ni kati ya traders wawili. Sio between seller and buyer. Inabidi usome hizi sections kwa uangalifu.
contract yako na muuzaji ni katika quality ya hiyo product kuwa fit for the purpose. Pale unaponunua kiatu, maziwa, gari, nk, lazima viwe fit for the purpose. Kwa hiyo ukinunua gari lisilotembea, una right ya kurudisha. Ukinunua kiatu kibovu, unakuwa na right ya kurudisha. Lakini huwezi kusema nimelanguliwa bei. Soma contract law kwenye ishu ya Offer and Acceptance. Alafu tofautisha na kitu wanaita "invitation to treat". Wewe unamu-offer muuza duka dola 60 kwa kiatu. Akipokea ile pesa, anakuwa ame-accept. A contract is formed!!
Kama ulikuwa hupendi bei, una right ya ku-walk out na kwenda duka lingine lolote.
Kwa hiyo mkuu...with much respect....i feel kuwa unachanganya topics mbili tofauti. na ndio maana nimekwambia inabidi upitie hii kwa uangalifu.
 
Nimesoma michango mingi naona hakuna kitu ambacho hakijaguswa. Tunahitaji kuwa na CONSUMER PROTECTION AUTHORITY itakayokuwa na nguvu za kisheria baada ya sheria hiyo kupitishwa bungeni. Ukiangalia vyombo kama SUMATRA, EWURA, TFDA etc havipo effective kuhakikisha kuwa watumiaji wanalindwa. Mfano kuna jamaa mmoja wa EWURA niliwahi kumuuliza kuwa huwa wanafanya nini kwa mfanyabiashara wakigundua kachakachuwa mafuta yake?, akanijibu ni fine kidogo na kumtaka aka ya refine mafuta hayo and sometimes anatoa chochote kitu ili wafunike kombe. Sasa hapa ndipo kwenye matatizo. Corruption and lack of proper legal actions against perpetrators.

wanasiasa wanatuambiwa kuwa tupo kwenye market economy kitu ambacho mimi sikubaliani nacho, tunahitaji mixed economy kwa nchi kama Tanzania zilizojaa utamaduni wa kisanii na kiwiziwizi. In Tanzania consumers doesn't get value for money as a result kila mwizi (mfanyabiashara) anachukulia advantage ya loophole kuweza kumnyonya mtumiaji.

Tukiweka sheria wazi kuwa ukimuuzia mtu kitu fake kitakachomdhuru unamlipa damages huu usanii utaisha. Kitu kingine kinachoitafuna Tanzania ni conflict of interest walizonazo watunga sera. Wengi ni wafanyabiashara wanaoendesha siasa matokeo yake wanaweka sera za kuwahakikisha faida kubwa kwenye biashara zao. Ingewekwa wazi kuwa unapokuwa mwanasiasa huna ruhusa wala haki ya kumsadia yeyote kupata Govt contracts tungepunguza wanasiasa masilahi wanaoangalia faida kwenye kila maamuzi yao.

CHADEMA ipo sahihi kabisa kuitaka serikali ichukue hatua dhidi ya ongezeko la bei kwani serikali au watendaji wake ni baadhi ya watu wenye hisa kwenye makampuni binafsi. Inapotokea watu wachache katika Tanzania wanapata hela za serikali kiujanjaujanja na kujikuta wanakuwa na disposable income ambayo hawakuitolea jasho hawa ndiyo drives ya inflation kwani wao value for money is nothing for them, yupo tayari kununua kitu cha laki moja kwa Tshs millioni moja. Hapa ndipo utakapoona kuwa tunahitaji mfumo mzima ubadilike, yaani kuanzia wa uongozi mpaka uchumi.

Unapokuwa na wanasiasa wamepata nafasi hizo kwa kuwekwa na wafanyabiashara wakubwa basi ujue kuwa watumiaji ni lazima waumie tu. Kama ni vigumu mtu kupata Shs alfu kumi mpaka aifanyie kazi iwe hivyo kwa system nzima hii nayo ni factor itakayomfanya mtu yeyote asinunue kitu cha mia tano kwa alfu kwa kuwa ana uchungu na pesa aliyofanyia kazi, ila kama yupo atakayekuwa tayari kununua basi anayeumia ni mwenye kipato cha chini. Gap between rich and poor should be minimized through fiscal means eg Taxation, Kwa Tanzania riches hasa wafanyabiashara wakubwa ni wakwepa kodi wakubwa kwa kuwa biashara zao zina mahusiano na viongozi.

Ninakumbuka wakati wa Nyerere wafanyakazi wa umma walikuwa waoga sana wa kufanya mambo ambayo ni juu ya uwezo wa kipato chao bila ya kuwa uthibitisho wa extra income, leo hii unamkuta mtumishi wa umma kaanza kazi miezi kumi iliyopita ana miliki mali ambazo angekuwa nazo kama atafanya kazi kwa miaka mia tano bila ya kutumia hata senti moja ya kipato chake cha sasa yaani awe anaweka tu na hakuna wa kumuuliza. Matokeo yake unakuta few resources are concentrated in few people who turns the burden of inflation to the majority. Wewe umejidunduliza na kupata hela zako unasema labla ununue asset ambayo market value yake ni sawa na hela zako leo hii anajitokeza mtu kapata dili la EPA analipa mara ishirini yako unadhani muuzaji atakuangalia wewe?

Nimalizie kwa mfano mmoja: Wakati ninasoma tulikuwa na jamaa mmoja alikuwa kipanga sana darasani(Bright student), yaani yeye kila mtihani alikuwa ni lazima apata alama A sasa walimu wakaanza kufanya nae mashindano kwa kutunga mitihani migumu sana, still akawa bado anapata A while anaemfuata ana C au D and the rest wanapata E. Ukiangalia mfano huu utaona kwamba darasa la watu 200 limeathiriwa na mtu mmoja mwenye uwezo wa juu sana ambaye amefanya walimu kuwa vipofu kuwa kuna wengine 199 ambao hawatafanya vyema kwa ugumu wa mtihani. Hili ndilo soko la Tanzania leo hii
 
Q:Do we have a price regulatory board in Tanzania?If not;Can we have it in a economy which is not socialistic?

Swali:Tuna bodi ya kufuatilia bei za bidhaa Tanzania?Kama hapana;Tunaweza kuwa nayo katika uchumi usio wa kijamaa?

Isije kuwa yale ya kujadili mabadiliko ya katiba bila kuifahamu katiba au ahadi ya mgombea ya kudhibiti bei za bidhaa bila kueleza mikakati!

Mungu Ibariki Tanzania.
Kwangu EWURA ni mzigo,sioni nacholipia.sitajadili
Hivi kwanini Tanzania kuingiza Magari ya mitumba toka nje lazima ulipie gharama kubwa?? tunamsidia mwananchi wa chini?? Siku hizi wabongo ili kukwepa ushuru mkubwa na vipenati wanaptisha
magari Kenya,Burundi,Rwanda,Congo nk.Hii ni akili au matope???????????????
 
Well utaweka athari katika market kama utaingilia bei na kuzipanga wewe. Kwa sababu kuna gharama za kuzalisha hizo bidhaa ambazo nazo itabidi uzi control if you want to control the market price, it is a complicated issue and not as simple it has been potrayed.

Tatizo kubwa ni kwamba Tanzania atujafikia what economist call a perfect competition, kwa maana hiyo market bado aijakuwa na ushindani wa kutosha hili ku stabilize the real prices. Kwa hiyo kuna majarabio wafanyabiashara wataweka bei za juu na iwapo watu wata nunua ujue jamaa hawatashusha bei kwa upande wao kuna faida. For the invicible hand to function there have to be enough competition in the market na hapo ndio bado.

Halafu kuna suala la ushuru Tanzania aizalishi products nyingi na kuna ushuru mkubwa hii nayo inachangia gharama za bidhaa kuwa juu baada ya kulipa vat. This is just mission impossible at the moment na kama kuna mtu atajaribu ujue hasara ni kubwa kuliko faida. What is needed ni financial regulators kuhakukikisha mambo yanatendeka bila short cuts na watu wanafuata sheria hili litachangia kufanya wafanya biashara kutokuja na mbinu za ujanja ujanja mfano wa majukumu ya hawa financial regulators ni kama yafuatayo fuata link:Financial Services Authority

Bado kuna suala la kuchapisha noti ovyo ovyo hili nalo linasababisha kushusha gharama ya hela na kusababisha mfumuko wa bei, kama unadaiwa halafu ukachapisha noti kutatua matatizo yako ujue na thamani ya hela inapungua matokeo yake bidhaa zitapanda tuu. Kwa hiyo kwa serikali kama ya Tanzania na yenyewe ina mchango mkubwa sana katika huu mfumuko wa bei kutokana na sera zake hafifu na fikra za ovyo ovyo halafu kutokuwa wakweli kwenye matendo yao na kuwaachia gharama wananchi.
 
Nimeona post nyingi zinazoshadadia serikali kupanga bei,hii siyo sahihi kama mnavyofikiria!Serikali ina regulate ku ensure fair competition.Ikipanga bei ita discourage investment.Ukitaka kuona wananchi wanawezaje kujikita hebu angalia huu mfano mdogo sana ambao ni moja ya harakati zinazoendelea tanzania lakini hazipewi ukurasa wa mbele na magazeti yetu ya kifisadi.
http//:Singida farmers unite to tripple the price of their produce
Pia kuna harakati zinazoendelea mikoa ya lindi na mtwara kwa wakulima wa ufuta!...ningeshauri serikali ipromote vitu kama hivi ila tu tudhibiti rushwa na muingilio wa serikali kwenye vyama hivi.
 
Nimeona post nyingi zinazoshadadia serikali kupanga bei,hii siyo sahihi kama mnavyofikiria!Serikali ina regulate ku ensure fair competition.Ikipanga bei ita discourage investment.Ukitaka kuona wananchi wanawezaje kujikita hebu angalia huu mfano mdogo sana ambao ni moja ya harakati zinazoendelea tanzania lakini hazipewi ukurasa wa mbele na magazeti yetu ya kifisadi.
http//:Singida farmers unite to tripple the price of their produce
Pia kuna harakati zinazoendelea mikoa ya lindi na mtwara kwa wakulima wa ufuta!...ningeshauri serikali ipromote vitu kama hivi ila tu tudhibiti rushwa na muingilio wa serikali kwenye vyama hivi.

Magazeti ya kifisadi ni yapi?Naona umeshaweka siasa kabla hata hujaanza mjadala.Actually niliulizia scale ya lengo kwa taifa zima.Rudia kusoma post yangu na asante kwa kuchangia.
 
Magazeti ya kifisadi ni yapi?Naona umeshaweka siasa kabla hata hujaanza mjadala.Actually niliulizia scale ya lengo kwa taifa zima.Rudia kusoma post yangu na asante kwa kuchangia.
Ndugu sheka,
Post yako nimeielewa vizuri sana!....jibu nilishatoa,nalo ni..."IMPRACTICAL" katika nchi yetu bali wananchi wenyewe ndio wanaweza kudhibiti bei za bidhaa mbalimbali.We don't need Price regulating entities,those are just bureaucratic bodies that spends taxpayers money doing nothing!
Magazeti mengi ya Tanzania hayachapishi success stories kama niliyoilink hapo juu kwa sababu vitu kama hivi viko against the bussiness community inayotawala siasa za nchi yetu!wote hawa kina mbowe,mtei.mengi,cheyo,....wanapingana na rostam,manji,mohamed enterprises,dewji etc for their own good using wananchi.....Thats bogus!
 
hakuna duniani nchi iliyokuwa 100% soko huria lazima kuwe na mfumo wa kuratibu mwenendo wa bei kwa kiwango fulani na si kuacha jamii kuteseka...popote duniani juzi juzi tu tumesikia marekani akimwambia china kuongeza bei ya bidhaa zake zinazoingia US........
 
mnataka price regulatory body ya namna gani? Ipange bei ya mchele, sukari, nguo, nk?
 
hakuna duniani nchi iliyokuwa 100% soko huria lazima kuwe na mfumo wa kuratibu mwenendo wa bei kwa kiwango fulani na si kuacha jamii kuteseka...popote duniani juzi juzi tu tumesikia marekani akimwambia china kuongeza bei ya bidhaa zake zinazoingia US........
huria zipo!...unasimamia competition na bei za bidhaa sensitive sio kiubabe bali kibiashara,hamna mtu anayeongelea soko hlela,tunazungumzia uwezekano wa serikali kupanga bei za bidhaa,hasa serikali ya tanzania!
 
Great thinkers, embu pitieni hiyo attachment.....i think ina good points!

Sharing is caring!
 

Attachments

  • price regulation.pdf
    245.1 KB · Views: 169
Great thinkers, embu pitieni hiyo attachment.....i think ina good points!

Sharing is caring!
Ina good points ambazo sidhani ziko practical in tanzania.The problem is ,our government is broke! and most policies nowadays aim at attracting investors rather than protecting the public.Serikali imeshika makali na wawekezaji wameshika mpini
 
Back
Top Bottom