Mdondoaji,
Hapo kwenye bold ndipo kuna utata.Regulations kwa watanzania ni kumbana zaidi mlaji au hata muuzaji bila kuhakikisha ubora au value for money.Ndio sababu nikauliza hizi bodies ziko kwa manufaa ya nani?
" Consumer protection"bado ni kitendawili.
Naam swadakta na ndio maana nikasema Consumer protection board ni muhimu ili serikali ifahamu kuwa customer gets what they deserve. Miezi kama minne iliyopita nilienda kufanya shopping Mlimani City nikakuta Kiatu cha ngozi kinauzwa laki mbili na hamsini, nikajiuliza maswali mengi majibu sikupata nikaenda amazon US nikakuta kiatu kile kile cha laki mbili na nusu nikiagiza na kusafirishiwa mpaka Tanzania kitanigharimu si zaidi ya $60 tena wananiletea na DHL.
Ukitazama laki mbili na nusu ya madafu ni equal to $159.84
Mie nikinunua Amazon na usafirishaji = $60
Tofauti ni = $99.8 approximately $100
Je wateja wanapata value for their money?