Do not withdraw your weapon if you won't use it; kulikuwa na sababu ya msingi ya kurelease sauti zilizodukuliwa za kina Membe?

Paul Alex

JF-Expert Member
Jul 14, 2012
4,240
9,527
Kawaida unapokabidhiwa silaha kuna mambo unatakiwa ufahamu. Hauruhusiwi kuitoa au kuionyesha silaha yako kama hauna sababu na hakika ya kuitumia.

Ni wazi kwamba utakutana na watu wenye fujo tena viburi ila kama hauna sababu na hakika ya kuitumia basi iache silaha yako kwenye holster na uwe mtulivu. Hauruhusiwi kupeleka mkono kwenye silaha wala kusogeza shati ili silaha ionekana maana 'brandishing' ya namna hii inatafsiriwa kama vitisho.

Ukifanya brandishing ya silaha, kwenye akili yako unaweza dhani ni kwaajili ya kutishia tu ila kwenye akili ya judge atatafsiri kama 'promise/ahadi' ya kuitumia.

Anyway, kwenye mazingira ya kawaida silaha ni pamoja na siri za mtu. Kuna 'watu' waliodukua na kuwa na sauti za kina Membe, Makamba, Kinana, Nape, n.k
Hivi hawa walikuwa na sababu ya kufanya 'brandishing' ya 'silaha' zao?

Je, brandishing imekuwa na faida au hasara kwao?

Moja kati ya sababu za kushinda vita ni 'element of surprise' /uwezo wa kushtukiza.
Sasa unapomjulisha adui yako silaha yako wakati huna hakika ya kuitumia unakuwa umefanya ujinga gani?

Membe amesema waziwazi sauti iliyodukuliwa 100% ni yake, tena kwa kujiamini! Enhe!! Kwa wadukuzi hii imekaaje?
Maana kama kuna ujumbe mlitaka kutuma kwenye jamii, basi umesaidia zaidi ujumbe wa Membe na agenda zake!

Hizi sauti za kudukua zingekuwa msaada kama zingebaki siri hivyo waliyokuwa wakiyaorganize kina Membe mngeyajua kabla na wakati wote kuwa mbele yao kwenye maamuzi.
Sasa mmepoteza hiyo element of surprise na hizo sauti hamuwezi kuzipeleka kwenye kikao chochote cha maamuzi tofauti labda na vikao vya uchawi!!

Do not withdraw your weapon if you don't intend to use it!
 
Kuna wakati ni muhimu kuitoa silaha na kulenga lakini bila ya kufungua usalama au kukoki kwa lengo la kuonya ili kuepusha madhara, kutoa tahadhali (deterrent), inawekana wahusika walikuwa na siri kubwa kwa hiyo ilikuwa lazima watishwe
 
Kwahivyo wametishika na wameacha?
Kuna wakati ni muhimu kuitoa silaha na kulenga lakini bila ya kufungua usalama au kukoki kwa lengo la kuonya ili kuepusha madhara, kutoa tahadhali (deterrent), inawekana wahusika walikuwa na siri kubwa kwa hiyo ilikuwa lazima watishwe
 
Zile audio clips zimeondoa maana nzima ya waraka wa Kinana na Makamba, zimeonyesha ni kama watu wenye uroho wa madaraka na ukwasi walio na gubu ya kuzibiwa miraja yao. Nia ya waraka ilikuwa ni kuanzisha vugu vugu la kumuondoa Magu 2020 ila baada ya zile clips kutoka hakuna mwana CCM atakayekuwa upande wa kina Nape/Membe kwa uwazi tena.

Zile clips zilikuwa tu ni ujumbe kuwa tunajua kila kitu kinacho endelea na tukiamua kuwashughulikia tuna uwezo huo pia, ndio maana Makamba katoswa uwaziri na hakuna madhara kwa chama.

Madhara yangekuwa makubwa kama wangeacha hilo vugu vugu lishike kasi maana kuna wana siasa wengine wengi wangeweza kujiunga nalo, kheri nusu shari kuliko shari kamili, jina la Kinana, Makamba, Nape na Membe ni kama kinyesi kwa ndani ya CCM kwa muda huu, hakuna kigogo atakayekubali kukaa karibu nao.
 
Hapana,
wana CCM wengi zaidi wapo sympathetic na hao wazee ila wapo Kimya kwa sasa (Strategic silence)!.
Wale waliotoka mbele ni kama "wameombwa" kufanya hivyo ili waseme chochote.
Lakini kuna underground movement ndani ya chama haikubaliani na mambo ya kumtumia Musiba
 
Do not withdraw your weapon if you don't intend to use it!
Kwenye vita kuna 'pre emptive strikes' kufagia uwanja na kuonesha kwamba tupo vizuri
Wewe una hangaika bure,lakini Membe ameshajua kuwa tayari ameumia,akizidisha gagari watu watamuweka uchi.
Masuala ya kuituliza nchi dhidi ya watu wambea na vidomi domi kama membe ya njia zake
 
Preemptive strike ni offensively strategic strikes to disable the enemies capabilities to strike first~ they are for defensive purpose!

Sasa, hili la kuachia sauti zilizodukuliwa limemkwamishaje Membe au mipango yake?
Kwenye vita kuna 'pre emptive strikes' kufagia uwanja na kuonesha kwamba tupo vizuri
Wewe una hangaika bure,lakini Membe ameshajua kuwa tayari ameumia,akizidisha gagari watu watamuweka uchi.
Masuala ya kuituliza nchi dhidi ya watu wambea na vidomi domi kama membe ya njia zake
 
Brandishing hiyo ya weapon ni kutahadharisha kuwa tuna silaha japo walioiona hiyo silaha hawaingiwi na hofu bali watatafuta namna inayofaa ya kusecure mipango yao
 
Hapana,
wana CCM wengi zaidi wapo sympathetic na hao wazee ila wapo Kimya kwa sasa (Strategic silence)!.
Wale waliotoka mbele ni kama "wameombwa" kufanya hivyo ili waseme chochote.
Lakini kuna underground movement ndani ya chama haikubaliani na mambo ya kumtumia Musiba
Wengi wangapi? Umetumia kipimio gani kujua?
 
Back
Top Bottom