Kasie
Platinum Member
- Dec 29, 2013
- 22,801
- 43,177
- Thread starter
- #21
Unawasha ili kureverse kutoka kwenye passenger bay ili kupisha ndege nyingie, kisha una-taxi hadi kwenye lot nyingine kusubiri abiria at a later time ambapo utaizima. Sasa ni bora tu ulivute kuliko hiyo process.
Yaani umenidadavulia barabara sasa nimeelewa, basi mie nilidhani ndege itapotua kushusha abiria basi hapo hapo itasubiri kupakia Abiria wengine Bila kusogea. Kumbe hilo zoezi huwa linatokea pale ambapo anashusha abiria na mizigo wakati anasubiria abiria wa kuondoka nao anaenda sehemu ingine ili pale apishe ndege ingine ishushe abiria. Japo hii itatumika haswa kwenye viwanja ambavyo si vikubwa. Nadhani kwenye viwanja vikubwa ambapo kila dakika ndege inapaa na kutua kama Istanbul Airport watakuwa na sehemu nyingi bila kuhitaji ndege kupishana eneo la kushusha abiria.
Yaani niko so interested sijui ni kwasababu napenda kusafiri..... hata sijielewi.
