DNA: Nusu ya watoto ni wa kusingiziwa

Mbimbinho

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2009
Messages
6,915
Points
2,000

Mbimbinho

JF-Expert Member
Joined Aug 1, 2009
6,915 2,000
hivi unajua kuwa 80%ya wazee wetu waliokwenda kupigana vita ya ed amin dada waliporudi walikuta wake zao wana watoto?na walinyamaza kimya ,sasa basi kama wewe ni wa enzi hizo jinyamazie kimya na kama baba yako alikwenda.asilimia kubwa sio baba zetu kabisa ,sasa basi usianzie mzigo mbali wewe kwanza anza kijipim akwa mama yako kweli wewe ni mtoto halali wa baba yako?then njoo upime wanao lasivyo nyamaza kimya!!na tena itakuta baba uako ni **** kapuku maskini mama yako akaona huyu ngoja nimshikilie hapa ili apate elimu umeipata sasa unachokonoa inawezekana kabisa ungeishia la saba wewe funga domo hilo.
kwa hili ndipo tumewaweza wanaume kwa kweli
Hii I bet inakuhusu kwa asilimia 100, maana ulivyopaniki...:glasses-nerdy:
 
Kakke

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Messages
1,882
Points
2,000

Kakke

JF-Expert Member
Joined Dec 4, 2010
1,882 2,000Florence Majani

ASILIMIA 44 ya wapenzi wanaokwenda Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kupima vinasaba (DNA), kwa ajili ya kujua uhalali wa watoto kwa baba, wamethibitishiwa kuwa watoto hao si wa kwao.

Takwimu za mwaka 2012 kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, zimeainisha kuwa kati ya watu 90 waliokwenda kupima DNA, 40 ambao ni sawa na asilimia 44, wameonekana kubambikiziwa watoto.

Takwimu hizo za kuanzia Januari hadi Oktoba mwaka huu, zilionyesha kuwa katika kesi 50 za waliokwenda kupima, matokeo yalionyesha kuwa ni wazazi halisi wa watoto wao.

Hata hivyo, idadi hiyo inayoonyesha kuwa kinababa siyo wazazi halisi wa watoto, imeshuka ikilinganishwa na takwimu za mwaka 2008/2009 ambazo zinaonyesha kuwa asilimia 60 ya watu waliochukua vipimo hivyo wamebainika kuwa si wazazi halisi wa watoto hao.

Mkemia na Mtambuzi wa Vinasaba vya Makosa ya Jinai, Gloria Machuve alisema jana kuwa ni vyema ikitambulika kwamba takwimu hizo zinatokana na watu waliokwenda kupima baada ya kutokea migogoro ya kimapenzi na siyo takwimu iliyochukuliwa kutoka kwa Watanzania wote.

"Hatusemi kuwa sasa wanaume wote Tanzania wanalea watoto ambao si wa kwao. Hizi ni takwimu za waliokuja kupima; yaani wale wenye matatizo," alisema.

Machuve alisema katika maabara hiyo, kesi nyingi zinazoonyesha kuwa watoto hao si halali, zimetokana na uhusiano wa ziada au usio rasmi baina ya wenza.

"Kwa mfano, mwanamume ana mwanamke wa nje ya ndoa au mwenye uhusiano usio rasmi, halafu mwanamke huyo anadai mtoto ni wa huyo mwanamume, mara nyingi matokeo huwa si mazuri," alisema Machuve.

Aidha, Machuve alisema takwimu za kuanzia mwaka 2005 hadi 2010 zinaonyesha kuwa tabia ya upimaji imeongezeka miongoni mwa Watanzania.

Alisema mwaka 2005/2006, kesi za upimaji wa vinasaba zilikuwa 96 na mwaka 2008/2009 kesi hizo zilikuwa 113 wakati mwaka 2009/2010, kesi za waliokwenda kupima zilifikia 125.

Alisema watu wengi wanaojitokeza kupima katika miaka ya karibuni wanataka kufahamu uhalali wa watoto wao ili wawajibike kuwalea kihalali.

"Lakini pia kuongezeka kwa kesi za utambuzi wa vinasaba kunatokana na kukua kwa uelewa na uwezo wa kiuchumi," alisema Machuve.

Alisema kuwa idadi ya upimaji wa DNA imeongezeka pia kwa watu wanaotaka kugawana mirathi na masuala ya uhamiaji.

"Wale wanaoishi Ulaya wanapotaka kuchukua watoto au ndugu zao, ni lazima wapimwe ili kuhakikisha, hivyo wanatuma vielelezo vyao kisha tunavifananisha na vielelezo vya walio hapa," alisema.

Machuve alisisitiza kuwa katika kesi nyingi, wanawake hukimbia katika hatua za upimaji na ni mara chache wanaume wakaukwepa mchakato huo.

Aidha, Machuve alisema upimaji wa vinasaba vya makosa ya jinai umefanikiwa kwa asilimia kubwa na asilimia 80 ya kesi zilitoa majibu chanya, yaani vielelezo vilivyoletwa viliwanasa watuhumiwa wa makosa ya jinai.

"Kuna kesi kama za ubakaji na mauaji ambazo tunaletewa vielelezo kama mbegu za kiume au silaha na tulipofanya utambuzi wa vinasaba tuliupata ukweli kwa kuwanasa watuhumiwa katika asilimia 80 ya kesi," Machuve.

Upimaji wa jinsia tawala

Aidha, mkemia huyo alisema maabara hiyo inapima jinsia tawala kwa wale wanaozaliwa na utata wa jinsia.

Alisema wapo watoto wanaozaliwa wakiwa na utata katika jinsia, kwa mfano ana sura ya kiume na sauti lakini ana sehemu ya siri ya kike.

"Watu kama hao wakifika hapa, tunaweza kuwapima ni jinsia ipi inatawala ili wapatiwe matibabu na kisha waitumie jinsia inayotawala. Wanaweza kufanyiwa upasuaji au kupewa vichocheo vya jinsia inayotawala," alisema.

Machuve pia alizungumzia suala lililojitokeza hivi majuzi kwamba Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angela Kariuki alisema baadhi ya kesi za upimaji DNA zitolewe bure akisema hilo haliwezekani kwani mchakato mzima wa upimaji una gharama kubwa.

"Upimaji wa DNA una gharama nyingi ambazo zinahitaji fedha, kuna gharama za kuendesha mtambo, kuna dawa ambazo punje ndogo tu inagharimu Sh200,000, hatuwezi kutoa bure huduma hii labda Serikali ilipie gharama hizo," alisema.
 
KYALOSANGI

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2011
Messages
2,564
Points
2,000

KYALOSANGI

JF-Expert Member
Joined Jan 21, 2011
2,564 2,000
hii ripoti nilishawahi kuisikiaga, lakini kutokana kiwango kikubwa cha udanganyifu kilichopo kwenye ndoa hiyo inawezekana. Kwani hata wanawake walio kwenye ndoa ukiwatongoza hawakatai. Sijui kwasababu hawapati dozi inayotosheleza, maana na wao binadamu tusiwalaumu tu. Ila jamani wenzao tunachoka saana kutokana na matatizo ya maisha, lakini woa wanajijali wao tu. Maana kiiukweli wanaume wengi hawaendi zaidi ya raundi moja ya heshima tu, wakati wenzetu wao wako fiti ile kinoma. Bahati mbaya sana gemu lenyewe kwetu sisi linahusisha brain 100%. Sasa ukichanganya na mahangaiko ya dunia, du, brain inakua overloaded.

sasa hakuna jema, ukiwa huna hela bado anatafutwa mwenye hela, ukiwa na hela lakini unachoka katika kutafuta hiyo hela, anasajiliwa house boy au dereva anae peleka watoto shule.

Katika hali hiyo ndio naweza kukubali kua 50% or more, wamebugi meen.

lakini, je kama mkemia mkuu amekosea, just human or machine error? sisi tunakua na uhakika gani as they say in court, beyond reasonable doubt?
mzimu umenena ! Tuombe mizimu ituepushe kwa sababu siku hizi ukimtania tu mke wa mtu anakuganda najua na wa kwetu pengine hivi2!
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2010
Messages
7,295
Points
2,000

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2010
7,295 2,000
Kuna kabila lina desturi kwamba watoto wako ukiwa mwanaume hawawezi kurithi mali yako kwa kuwa huwezi kuwa na uhakika kama kweli ni wa kwako. Watoto wa dada zako ndio wanaorithishwa mali zako kwa sababu hao hakika ni ndugu zako. Sasa hili la Mkemia Mkuu linaonyesha kuunga mkono wazo hili!

ASILIMIA 44 ya wapenzi wanaokwenda Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kupima vinasaba (DNA), kwa ajili ya kujua uhalali wa watoto kwa baba, wamethibitishiwa kuwa watoto hao si wa kwao. Takwimu za mwaka 2012 kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, zimeainisha kuwa kati ya watu 90 waliokwenda kupima DNA, 40 ambao ni sawa na asilimia 44, wameonekana kubambikiziwa watoto.

Source: Mwananchi
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Messages
64,530
Points
2,000

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2012
64,530 2,000
Maana yake ni kwamba hao wakina mama bila shaka yoyote wala woga wowote ule walifanya ngono za kizembe na wanaume wengine , wenye wapenzi wengine , nao wenye wapenzi wengine na wengine ! Tuko wangapi ? Usitegemee ukimwi kwisha kwa style hii !
 
pilau

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Messages
1,578
Points
1,225

pilau

JF-Expert Member
Joined Aug 16, 2012
1,578 1,225
........ Kweli kabisa ....kama ni watoto wa nje...wanawake wanaamua kumpa mtoto mwanamume mwenye kipato.. na wengine wako ndani ya ndoa lakini uchakalamu wao wanatembea nje... lakini kuna usemi KITANDA HAKIZAI HARAMU ..... hapo tusemeje?
 
Mzalendo_Mkweli

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2012
Messages
1,214
Points
1,500

Mzalendo_Mkweli

JF-Expert Member
Joined Jan 30, 2012
1,214 1,500Florence Majani

ASILIMIA 44 ya wapenzi wanaokwenda Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kupima vinasaba (DNA), kwa ajili ya kujua uhalali wa watoto kwa baba, wamethibitishiwa kuwa watoto hao si wa kwao.

Takwimu za mwaka 2012 kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, zimeainisha kuwa kati ya watu 90 waliokwenda kupima DNA, 40 ambao ni sawa na asilimia 44, wameonekana kubambikiziwa watoto.

Takwimu hizo za kuanzia Januari hadi Oktoba mwaka huu, zilionyesha kuwa katika kesi 50 za waliokwenda kupima, matokeo yalionyesha kuwa ni wazazi halisi wa watoto wao.

Hata hivyo, idadi hiyo inayoonyesha kuwa kinababa siyo wazazi halisi wa watoto, imeshuka ikilinganishwa na takwimu za mwaka 2008/2009 ambazo zinaonyesha kuwa asilimia 60 ya watu waliochukua vipimo hivyo wamebainika kuwa si wazazi halisi wa watoto hao.

Mkemia na Mtambuzi wa Vinasaba vya Makosa ya Jinai, Gloria Machuve alisema jana kuwa ni vyema ikitambulika kwamba takwimu hizo zinatokana na watu waliokwenda kupima baada ya kutokea migogoro ya kimapenzi na siyo takwimu iliyochukuliwa kutoka kwa Watanzania wote.

"Hatusemi kuwa sasa wanaume wote Tanzania wanalea watoto ambao si wa kwao. Hizi ni takwimu za waliokuja kupima; yaani wale wenye matatizo," alisema.

Machuve alisema katika maabara hiyo, kesi nyingi zinazoonyesha kuwa watoto hao si halali, zimetokana na uhusiano wa ziada au usio rasmi baina ya wenza.

"Kwa mfano, mwanamume ana mwanamke wa nje ya ndoa au mwenye uhusiano usio rasmi, halafu mwanamke huyo anadai mtoto ni wa huyo mwanamume, mara nyingi matokeo huwa si mazuri," alisema Machuve.

Aidha, Machuve alisema takwimu za kuanzia mwaka 2005 hadi 2010 zinaonyesha kuwa tabia ya upimaji imeongezeka miongoni mwa Watanzania.

Alisema mwaka 2005/2006, kesi za upimaji wa vinasaba zilikuwa 96 na mwaka 2008/2009 kesi hizo zilikuwa 113 wakati mwaka 2009/2010, kesi za waliokwenda kupima zilifikia 125.

Alisema watu wengi wanaojitokeza kupima katika miaka ya karibuni wanataka kufahamu uhalali wa watoto wao ili wawajibike kuwalea kihalali.

"Lakini pia kuongezeka kwa kesi za utambuzi wa vinasaba kunatokana na kukua kwa uelewa na uwezo wa kiuchumi," alisema Machuve.

Alisema kuwa idadi ya upimaji wa DNA imeongezeka pia kwa watu wanaotaka kugawana mirathi na masuala ya uhamiaji.

"Wale wanaoishi Ulaya wanapotaka kuchukua watoto au ndugu zao, ni lazima wapimwe ili kuhakikisha, hivyo wanatuma vielelezo vyao kisha tunavifananisha na vielelezo vya walio hapa," alisema.

Machuve alisisitiza kuwa katika kesi nyingi, wanawake hukimbia katika hatua za upimaji na ni mara chache wanaume wakaukwepa mchakato huo.

Aidha, Machuve alisema upimaji wa vinasaba vya makosa ya jinai umefanikiwa kwa asilimia kubwa na asilimia 80 ya kesi zilitoa majibu chanya, yaani vielelezo vilivyoletwa viliwanasa watuhumiwa wa makosa ya jinai.

"Kuna kesi kama za ubakaji na mauaji ambazo tunaletewa vielelezo kama mbegu za kiume au silaha na tulipofanya utambuzi wa vinasaba tuliupata ukweli kwa kuwanasa watuhumiwa katika asilimia 80 ya kesi," Machuve.

Upimaji wa jinsia tawala

Aidha, mkemia huyo alisema maabara hiyo inapima jinsia tawala kwa wale wanaozaliwa na utata wa jinsia.

Alisema wapo watoto wanaozaliwa wakiwa na utata katika jinsia, kwa mfano ana sura ya kiume na sauti lakini ana sehemu ya siri ya kike.

"Watu kama hao wakifika hapa, tunaweza kuwapima ni jinsia ipi inatawala ili wapatiwe matibabu na kisha waitumie jinsia inayotawala. Wanaweza kufanyiwa upasuaji au kupewa vichocheo vya jinsia inayotawala," alisema.

Machuve pia alizungumzia suala lililojitokeza hivi majuzi kwamba Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angela Kariuki alisema baadhi ya kesi za upimaji DNA zitolewe bure akisema hilo haliwezekani kwani mchakato mzima wa upimaji una gharama kubwa.

"Upimaji wa DNA una gharama nyingi ambazo zinahitaji fedha, kuna gharama za kuendesha mtambo, kuna dawa ambazo punje ndogo tu inagharimu Sh200,000, hatuwezi kutoa bure huduma hii labda Serikali ilipie gharama hizo," alisema.
Nani wa kulaumiwa:- Malezi ya vijana, tamaduni, utandawazi, wababa au wamama???
 
Nivea

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2012
Messages
7,462
Points
1,250

Nivea

JF-Expert Member
Joined May 21, 2012
7,462 1,250
Hahaha hii kitu itawatesa sana wanaume wakifika leo huko home nikuangalia tu watoto km wamefanana nao,kitanda hakizai kharamu!!!!!
 
M-mbabe

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2009
Messages
9,089
Points
2,000

M-mbabe

JF-Expert Member
Joined Oct 29, 2009
9,089 2,000
Hivi kule Maternity Ward, huwa hakuna uwezekano wa watoto kukosewa na kupewa mama mwingine?...najua huwa kuna alama wanafungwa watoto mikononi
I think you are raising a very valid point here. unakuta mtoto kwenye family hiyo hiyo ana features na traits ambazo huwezi kuzi-link ama kwa baba au mama au hata kukaribiana na nduguze wa "tumbo moja"!

kuna haja ya utafiti huu ulioibuka na hii 44% pia uende deep zaidi....like what's the probability kwamba mtoto hana vinasaba vya wote baba na mama?
 
ngonani

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2012
Messages
1,371
Points
1,250

ngonani

JF-Expert Member
Joined Aug 27, 2012
1,371 1,250
Nafikiri hakuna jipya,wote waliokwenda kupima DNA ni wale ambao wana mashaka fulani,uwezi kwenda kupima DNA ya laki 3 just for fun
 
Forum statistics

Threads 1,344,066
Members 515,323
Posts 32,806,448
Top