DNA: Nusu ya watoto ni wa kusingiziwa

Mademu siku hizi wana wanaume pembeni wengine ndio maana watoto tunabambikiwa kumbe wa mwanaume mwingine
 
Tatizo la wanaume kubambikiwa wototo lipo. Mimi juzijuzi mwanamke niishiye naye kamuandikisha mtoto shule kwa jina la bwana yake wa zamani. Kwa hiyo shuleni anaitwa jina B nyumbani anaitwa jina A !!!
 
Hivi kule Maternity Ward, huwa hakuna uwezekano wa watoto kukosewa na kupewa mama mwingine?...najua huwa kuna alama wanafungwa watoto mikononi

Asilimia hii ni kubwa sana. Usije ukakuta machine ya kupima DNA ni miongoni mwa mashine feki zinazoingizwa hapa nchini.
 
Wanaokwenda huko tayari wako katika "high risk group" ya kutokuwa wazazi halisi wa watoto.

Kwa sababu mtu anayemuamini mkewe, kisha akazaliwa mtoto ambaye anafanana sana na baba, anakuwa hana haja ya kwenda huko.
 
ndio wanamme wachangamke sasa.

Haya mambo ya kila mita tano kuna bango la 'mganga toka Sumbawanga na naijeria, anaongeza nguvu'

ila hii sio 'random sampling', hawa ni wale walioenda kupima. Na hadi kufikia point kupima uwezekano wa kuwa kulikuwa na doubts upo.
 
Ingawa si wote, huu ni ushahidi kuwa ufuska kwenye ndoa umezidi. Ni ushahidi wa mmomonyoko wa maadili. Kwenye mikoa kama Mbeya, Kilimanjaro, Singida, Dodoma, Kagera, Lindi, Mtwara na Zanzibar sijui hali inatisha kiasi gani? Tunajenga taifa la wanaharamu siyo? Nashukuru Mungu watoto wangu wote hufanana nami. Isitoshe mambo ya kuzaa nshamalizana nayo.
 
Kongosho inabidi tukapime. Pamoja na kuwa ulibeba ile mimba kwa miezi nane nina wasiwasi kama mtoto ni wako.

Nina wasiwasi wewe ni surrogate mother. Akyanani tena.
 
Last edited by a moderator:
sikubishii wala kukutisha
kufanana si huwa inatokea sana

iko hivi kwa uzoefu wangu
kama mie nina watoto 6, wanne wa mme, 2 nimechakachua

watoto wote huwa wanaonekana wanafanana maana sura ya mama inakuwemo ndani yao.

Unless baba awe ana wasiwasi na tabia za mkewe, ila kama hajawahi stuka. Analea wote bila wasiwasi. Tatizo huwa ni kwenye vitabia, unakuta mtoto anakuwa wa 1 kila siku wakati baba anajijua akili zake za kubip ama mtoto wa mwisho kila siku wakati baba kipanga.

Vitabia ndio huumbua sana!
Ingawa si wote, huu ni ushahidi kuwa ufuska kwenye ndoa umezidi. Ni ushahidi wa mmomonyoko wa maadili. Kwenye mikoa kama Mbeya, Kilimanjaro, Singida, Dodoma, Kagera, Lindi, Mtwara na Zanzibar sijui hali inatisha kiasi gani? Tunajenga taifa la wanaharamu siyo? Nashukuru Mungu watoto wangu wote hufanana nami. Isitoshe mambo ya kuzaa nshamalizana nayo.
 
he he he he, umeanza.

Siku hizi hata akina mama nao tunachakachua tu, daym

ila mbona yule mtoto macho yangu kabisa?
Wanangu wote macho huwa kama yangu so wote wanafanana na mie.

Kongosho inabidi tukapime. Pamoja na kuwa ulibeba ile mimba kwa miezi nane nina wasiwasi kama mtoto ni wako.

Nina wasiwasi wewe ni surrogate mother. Akyanani tena.
 
Last edited by a moderator:
Mwanangu Kongosho ingawa una tabia chafu ya kuchakachua watoto nimekupata. Kwangu sina shaka na wanangu kwa vile wamezaliwa Ulaya. Niliwazalia kisiwani ambapo nashukuru Mungu hapakuwapo na waswahili toka Bongo au karibu na Bongo. Iisitoshe bi mkubwa wangu si kiruka wala mtu wa kutishwa na mapenzi ya wizi. Hivyo sina shaka. Nami ninao sita.
 
Wengine huwa hatuhitaji hiyo kitu kwa sababu tukifyatua
watoto utafikiri tuliingizwa kwenye fotocopy machine yaani
Kwa mama anachukua rangi tu lakini vingine vyote ni mimi
mwenyewe.
Bila shaka utakuwa mpare wewe. wale hawabahatishi
 
kama ni kisiwani hapo sawa, na kama bi. Mkubwa katulia hiyo ni bonus.

Mie ni mchakachuaji mashuhuri, ngoja nile maisha, nikizeeka natulia.

Mwanangu Kongosho ingawa una tabia chafu ya kuchakachua watoto nimekupata. Kwangu sina shaka na wanangu kwa vile wamezaliwa Ulaya. Niliwazalia kisiwani ambapo nashukuru Mungu hapakuwapo na waswahili toka Bongo au karibu na Bongo. Iisitoshe bi mkubwa wangu si kiruka wala mtu wa kutishwa na mapenzi ya wizi. Hivyo sina shaka. Nami ninao sita.
 
Ingawa si wote, huu ni ushahidi kuwa ufuska kwenye ndoa umezidi. Ni ushahidi wa mmomonyoko wa maadili. Kwenye mikoa kama Mbeya, Kilimanjaro, Singida, Dodoma, Kagera, Lindi, Mtwara na Zanzibar sijui hali inatisha kiasi gani? Tunajenga taifa la wanaharamu siyo? Nashukuru Mungu watoto wangu wote hufanana nami. Isitoshe mambo ya kuzaa nshamalizana nayo.

Mkuu kitanda hakizai haramu!
 
Hiyo ni falasafa ya kishenzi na ya zamani na ya kizaramo ambapo uanaharamu ni asili yao. Kitanda kinazaa haramu tena chafu sana. Kwangu kitanda kinazaa haramu na ikitokea huyo mama na kitoto chake wanapugwa haraka iwezekanavyo. Sina simile wala huruma na hii kwa vile mie siko tayari kuzaa nje ya kitanda changu.
 
Ila mwanangu Kongosho angalia miwaya. Inaweza kukukumba hata kabla hujazeeka ukafa kwa majuto. Hata ukizidaka nyingi kiasi gani hutazimaliza na tamaa haitaisha. Dawa ya kumaliza tamaa ni kuachana nayo na kutulia kwa mmoja. Nadhani kimeeeleweka. Ila kama unaona hilo la kugawa kama una ugomvi nayo ni deal go ahead and perish. Amen!
 
mmh, sio lazima niikwae, as long as I follow the rules.

Katika kila game, wachezaji wanajua rules za mchezo, na nazingatia sheria hizo.

Not for money, just for fun!

Ila mwanangu Kongosho angalia miwaya. Inaweza kukukumba hata kabla hujazeeka ukafa kwa majuto. Hata ukizidaka nyingi kiasi gani hutazimaliza na tamaa haitaisha. Dawa ya kumaliza tamaa ni kuachana nayo na kutulia kwa mmoja. Nadhani kimeeeleweka. Ila kama unaona hilo la kugawa kama una ugomvi nayo ni deal go ahead and perish. Amen!
 
Good fact kwamba infidelity ipo sana tu ila tunaifumbia macho kwa kupretend kwamba haipo

matatizo ni makubwa zaidi hasa mijini na ndio maana hata maambukizi ya ukimwi kwa wanandoa yako juu.... maana ni pekupeku tu

swali: je baada ya miaka 10 ukagundua kwamba mtoto umpendaye hapo nyumbani si wako.... utamtafuta baba yake?? Je na mama utamuacha??? nini athari katika familia??

TUNAPENDA MIKASI LAKINI HATTAKI ITUKATE... MWE
 
Aisee utawapa watu presha bure. Ujue hizi takwimu inabidi kuzielewa vizuri pia. Wanaoenda kupima DNA watakuwa na sababu za kutaka kuhakikisha kuwa mtoto ni wa kwao. Mfano labda kuna tetesi toka kwa majirani kuwa mke wa mzee fulani anatembea na jirani, mtoto katoka hafanani na baba, anafanana na muuza bucha, au labda kulikuwa na dalili za mke kumsaliti. Kwahiyo of course takwimu zinaonesha kwamba karibia nusu ya wanaopimwa DNA hazimatch. Ukisema upime nchi nzima DNA nina uhakika kwamba asilimia itakuwa chini zaidi.

Nilishatoa mfano kwenye thread nyingine. Unaweza kusema asilimia 97 ya wabakaji ni wanaume, lakini haimaanishi kwamba asilimia 97 ya wanaume ni wabakaji.

Kwahiyo unaweza kusema asilimia 44 ya waliopima DNA wamekuta watoto si wao, lakini haimaanishi kwamba asilimia 44 ya watoto nchi nzima ni wakubambikizwa. Pia hiyo sample ni chini ya watu 200 ambayo ni ndogo saana.

Anyways, kila siku kuna thread za kuzaa watoto nje na vimada. This is just the female equivalent, not as obvious!

damu_safi.jpg

Asilimia 44 ya wapenzi wanaokwenda Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kupima vinasaba (DNA), kwa ajili ya kujua uhalali wa watoto kwa baba, wamethibitishiwa kuwa watoto hao si wa kwao. Takwimu za mwaka 2012 kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, zimeainisha kuwa kati ya watu 90 waliokwenda kupima DNA, 40 ambao ni sawa na asilimia 44, wameonekana kubambikiziwa watoto.

Takwimu hizo za kuanzia Januari hadi Oktoba mwaka huu, zilionyesha kuwa katika kesi 50 za waliokwenda kupima, matokeo yalionyesha kuwa ni wazazi halisi wa watoto wao. Hata hivyo, idadi hiyo inayoonyesha kuwa kinababa siyo wazazi halisi wa watoto, imeshuka ikilinganishwa na takwimu za mwaka 2008/2009 ambazo zinaonyesha kuwa asilimia 60 ya watu waliochukua vipimo hivyo wamebainika kuwa si wazazi halisi wa watoto hao.

Mkemia na Mtambuzi wa Vinasaba vya Makosa ya Jinai, Gloria Machuve alisema jana kuwa ni vyema ikitambulika kwamba takwimu hizo zinatokana na watu waliokwenda kupima baada ya kutokea migogoro ya kimapenzi na siyo takwimu iliyochukuliwa kutoka kwa Watanzania wote. "Hatusemi kuwa sasa wanaume wote Tanzania wanalea watoto ambao si wa kwao. Hizi ni takwimu za waliokuja kupima; yaani wale wenye matatizo," alisema.

Machuve alisema katika maabara hiyo, kesi nyingi zinazoonyesha kuwa watoto hao si halali, zimetokana na uhusiano wa ziada au usio rasmi baina ya wenza. "Kwa mfano, mwanamume ana mwanamke wa nje ya ndoa au mwenye uhusiano usio rasmi, halafu mwanamke huyo anadai mtoto ni wa huyo mwanamume, mara nyingi matokeo huwa si mazuri," alisema Machuve.

Aidha, Machuve alisema takwimu za kuanzia mwaka 2005 hadi 2010 zinaonyesha kuwa tabia ya upimaji imeongezeka miongoni mwa Watanzania. Alisema mwaka 2005/2006, kesi za upimaji wa vinasaba zilikuwa 96 na mwaka 2008/2009 kesi hizo zilikuwa 113 wakati mwaka 2009/2010, kesi za waliokwenda kupima zilifikia 125.
Alisema watu wengi wanaojitokeza kupima katika miaka ya karibuni wanataka kufahamu uhalali wa watoto wao ili wawajibike kuwalea kihalali.

Ni wale wanaofanyiwa utafiti na mkemia mkuu wa Serikali - Habari - mwananchi.co.tz
 
Back
Top Bottom