Dkt. Samia: Kinachotokea bandarini nitakisomea Ikulu

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,237
103,890
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo June 09,2023 amefungua na kushiriki Mkutano wa 14 wa Baraza la Biashara (TNBC), Ikulu Dar es salaam ambapo moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba yake ni kwamba kazi kubwa inaendelea kufanyika ya kuboresha mifumo ya TEHAMA kwenye Sekta za Umma ili ianze kusomana ambapo ameahidi kuwa sio zaidi ya miezi sita kinachotokea Bandarini atakuwa anaweza kukisoma akiwa Ikulu.

Rais Samia amenukuliwa akisema “Kazi kubwa inaendelea kufanyika ya kuboresha mifumo ya TEHAMA, mifumo yetu haisomani, taarifa hazioani, kazi tunayokwenda kufanya kwa nguvu kubwa sasa ni kufanya mifumo ndani ya Sekta ya Umma isomane pia iwe na vigezo vya Kimataifa”

“Changamoto zilizotajwa hapa hizo za Kariakoo na nini ni kwamba mifumo yetu haijaweza kuchukua taarifa zote hizo, kazi iliyopo sasa ni kuhakikisha mifumo yetu inabeba taarifa zote hizo ili tuweze kuwa na taarifa nyingi ambazo zitapelekwa kufanya maamuzi, hiyo ni kazi mbele yetu kwa upande wa Serikali na ninawaahidi nadhani sio zaidi ya miezi sita tutakuwa tunasoma kinachotokea Bandarini nakisoma Mimi Ikulu huku”

My Take
Mpaka hapa tuna sababu ya kuitisha uchaguzi mwingine
 
FiBzr7GXoAAslq1.jpg
 
Hiyo TEHAMA haitasaidia kitu ikuwa mtu huna hulka ya kusoma unacholetewa mezani.
Mkataba wa bandari sidhani kama aliusoma na mapungufu yake yote zaidi ya kuwaambia wasaidizi nendeni mkalitazame!
Hata juzi kati hapa kachomekewa jina la Katibu Tawala aliyemtumbua miezi kadhaa nyuma, leo jina linasoma kwanza ubini halafu majina mengine yanafuata ila mtu ni yule yule aliyefukuzwa kwa uzembe...hakugundua na wadaidizi washajua mapungufu yake wanamchomekea tuu kwa sabb hajiridhishi.
 
Uchaguzi haijawahi kuwa suluhisho Afrika,kifo labda
 
Hiyo TEHAMA haitasaidia kitu ikuwa mtu huna hulka ya kusoma unacholetewa mezani.
Mkataba wa bandari sidhani kama aliusoma na mapungufu yake yote zaidi ya kuwaambia wasaidizi nendeni mkalitazame!
Hata juzi kati hapa kachomekewa jina la Katibu Tawala aliyemtumbua miezi kadhaa nyuma, leo jina linasoma kwanza ubini halafu majina mengine yanafuata ila mtu ni yule yule aliyefukuzwa kwa uzembe...hakugundua na wadaidizi washajua mapungufu yake wanamchomekea tuu kwa sabb hajiridhishi.
Kusoma nacho ni kipaji🙏
 
Back
Top Bottom