Uchaguzi 2020 Dkt. Ryoba: TBC itaonyesha mikutano ya kampeni ya vyama vyote vya siasa, wanasiasa watumie lugha za staha

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,976
Mkurugenzi wa TBC Dkt. Ryoba amesema shirika lake litaonesha mikutano ya vyama vyote vya siasa wakati wa kampeni.

Dr Ryoba amewataka viongozi wa kisiasa kutumia lugha za staha na kuzingatia maadili ya viongozi.
Kadhalika Dr Ryoba amesema atakuwa na kikao na viongozi wa vyama vya siasa ili kuweka utaratibu mzuri wa matangazo nyakati za kampeni.

Chanzo: Star tv

Maendeleo hayana vyama!
 
Kwanza kwa wapinzani wa kweli hawawezi kukubali kuitumia hiyo channel maana lazima wazifanyie editing kabla ya kuzirusha
Sioni cdm na Act wakipewa nafasi na hiyo TBC. Sana sana natarajia kuona ccm na michepuko yake Nccr, Cuf, TLP nk wakipewa nafasi.
 
Hapo wanatafuta namna ya kumrusha Magufuli peke yake, huu ni mtego Chadema wakigoma itawarahizishia zaidi mpango wao.

Chadema wakikubaki watarusha mkutano mmoja halafu watasema haina maadili wanakatisha matangazo wataendelea na Magufuli.

NCCR, TLP, CUF na wengine watarushwa Sana Ila sio Chadema na ACT.
 
Aseme tu wataonesha ya ccm. Sasa hiyo nj geresha ionekane kuwa vyama vyote vitaoneshwa. Hanma kitu hapo.
 
This time CCM wana hofu sana, hawajui nyongo za wapinzani zimebeba nini!
Wanalilia lugha za staha wakati Jiwe anadhalilisha watu hadharani!
Nchi inaongwazwa kwa kufuata sheria, kuomba wapinzani wapige kampeni kwa kuibembeleza CCM kwa kigezo cha lugha ya staha ni upumbavu!
 
This time CCM wana hofu sana, hawajui nyongo za wapinzani zimebeba nini!
Wanalilia lugha za staha wakati Jiwe anadhalilisha watu hadharani!
Nchi inaongwazwa kwa kufuata sheria, kuomba wapinzani wapinge kampeni kwa kuibembeleza CCM ni upumbavu!
 
TBC siyo kuchuja,watakachofanya ni kuonyesha vile vyama vya upinzani kama cuf na nccr ambavyo vinadhaminiwa na ccm,na pia wanaweza kutafuta kisingizo wasirushe chadema au ACT kwamba wanatumia lugha kali na matusi
Ryoba muongo sana huyo, yeye angebaki na CCM tu kama ilivyo ada na ndipo anapolipwa
TBC watachuja sana, awaachie vyombo vingine tunavyovijua vina balance habari za Kampeni
 
Back
Top Bottom