Dkt. Philip Mpango: Mimi ni mzima, walionizushia kifo nimewasamehe

KooZito

JF-Expert Member
Dec 14, 2020
396
1,377
Katika kuuaga mwili wa Balozi John Kijazi Karemjee, Rais Magufuli amesoma hadharani ujumbe mfupi wa simu aliyotumiwa na Waziri Mpango akimjulisha Rais juu ya Afya yake.

Nukuu

''Mheshimiwa Rais asante nimepata ujumbe wako kupitia kwa mke wangu, kwa Neema ya Mungu naendelea vizuri, nakula na ninafanya mazoezi ya kifua, wanaonizushia kifo niliwaombea msamaha kwa Yesu wakati wa sala ya jioni jana

Mheshimiwa Rais, Mungu akubariki na akupe Neema ya ujasiri zaidi katika kuliongoza Taifa letu katika wimbi hili, naungana na wewe na familia katika maombolezo ya kifo cha mpendwa wetu Balozi kijazi''. - Mwisho wa nukuu


Rais Magufuli amewaonya "walioniua Mpango" huko tweeter.

My Take: Tumuombee Mpango na wagonjwa wengine wote.
 
Back
Top Bottom