Dkt Philip Mpango Mgeni Rasmi Ufunguzi Mkutano Mkuu wa BAKWATA Tanga

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,207
4,703
Wadau wa JF

Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Isdory Mpango atakuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA)

Mkutano huo mkuu utafanyika siku ya Jumapili Juni 27,2021 Mkoani Tanga

Taarifa imetolewa na Katibu Mkuu wa BAKWATA

Alhaji Nuhu Nurdini

FB_IMG_16240380079486329.jpg
 
Afadhali aiseeeee, utawala ule ulijitahidi kutumaliza
 
Akija aondoke na viongozi wabadhirifu, wala rushwa, wakandamizaji, wamiliki magenge ya uhalifu na wanaosababisha migogoro ya ardhi
Tutampokea kwa mabango.

Pia aje na waandishi wake wa habari maana waandishi wa Tanga wapo likizo siku zote
 
Kwa hiyo Tanga hakuna waandishi wa habari.

Taja unaodhani hawafai hapo Tanga tutawahiji kidigitali mpaka waingie kwenye kumi nanane.

Jina na tuhuma yake, idara pia
 
Kwa hiyo Tanga hakuna waandishi wa habari.

Taja unaodhani hawafai hapo Tanga tutawahiji kidigitali mpaka waingie kwenye kumi nanane.

Jina na tuhuma yake, idara pia
Mkurugenzi wa Tanga na Shigela walisha wanunua waandishi wa habari jumla. Hakuna waandishi wa habari Tanga. Ama kweli rushwa ni adui mkubwa sana
 
27 June 2021
Tanga, Tanzania

MKUTANO MKUU WA BARAZA LA BAKWATA



Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt Philip Isdor Mpango hii leo Juni 27, 2021 amefungua Mkutano mkuu wa baraza la waislamu Tanzania (BAKWATA) Unaofanyika Jijini Tanga.

Makamu wa Rais amewahakikishia BAKWATA kwamba serikali ipo pamoja nao na ipo tayari katika kupokea ushauri na maoni watakayotoa juu ya mwenendo wa serikali wakati wowote.

Makamu wa Rais amewaomba viongozi wa dini kuendelea kuliombea taifa, kuwahimiza wananchi kufanya kazi ambazo ni halali, kudumisha Amani na umoja katika taifa, kusisitiza maadili mema kwa jamii pamoja na umuhimu wa kuhifadhi mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Aidha Makamu wa Rais amewasihi viongozi wa dini kuendelea kuwahimiza waumini kuchukua tahadhari juu ya janga la corona, ikiwa ni pamoja na kufuata maelekezo byote yanayotolewa na wataalamu wa afya nchini.

Makamu wa Rais amesihi BAKWATA, Viongozi wote wa dini ya Kiislam na dini nyingine na pia Wakuu wa Taasisi zote za Dini kujitahidi kuziendesha Taasisi hizo kwa mujibu wa Katiba zao na mafundisho ya Dini.

Awali akisoma hotuba ya BAKWATA Katibu wa Baraza hilo Sheikh Nuhu Jabir Mruma amesema Bakwata itaendelea kushirikiana na serikali pamoja na kuwahimiza waumini wa dini ya kiislamu kulipa kodi kwa manufaa ya taifa.

Kwa Upande wake Mufti Mkuu wa Tanzania Aboubakar Zuber Bin Ali amewataka waislamu nchini kote kuongeza umoja na mshikamano ambao utaleta utulivu katika nchi.
 
Wadau wa JF

Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Isdory Mpango atakuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania ( BAKWATA)

Mkutano huo mkuu utafanyika siku ya Jumapili Juni 27,2021 Mkoani Tanga

Taarifa imetolewa na Katibu Mkuu wa Bakwata Alhaji Nuhu Nurdini

View attachment 1823025
Aendelee hukohuko akimaliza akazindue mbegu mpya za maparachichi, akimaliza akatembelee sanasana, akitoka hapo apelekwe kwenye uzinduzi wa wiki wa nanenane, akimaliza arudi kwa watoto yatima.

Nadhani baada ya hapo itakuwa vema akienda kusalimia kaburi maarufu. Maana aliacha kwenda kusalimia la Nyerere au Mkapa akaona lile kaburi lake pendwa ndio akalitembelee pekee.
 
Dah. Huyu mshua mara tu miezi mitatu hii kachana hivi?

Au ndiyo analipizia alivyopoteza mwili kwa kuumwa?
 
Dah. Huyu mshua mara tu miezi mitatu hii kachana hivi?

Au ndiyo analipizia alivyopoteza mwili kwa kuumwa?
Enzi zile alikuwa analazimishwa kula machukuchuku ya mapanki ya samaki, sasa hivi analetewa kachori na sharubawti za Zanzibar sheikh 😃

Naona amegundua maisha ni marefu ila hayana maana you live always and you die once.
 
Back
Top Bottom