Warioba : Namfahamu Nchimbi sio chawa

Warioba : Namfahamu Nchimbi sio chawa

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
506
Reaction score
806
Jaji Mstaafu Sinde Warioba amesema kwamba anamfahamu vyema aliyekuwa Makamu wa Rais, Balozi Emmanuel Nchimbi, akisema kuwa sio chawa.

Ameeleza kuwa Nchimbi amekuwa akimtembelea, ambapo hupata fursa ya kuzungumza masuala mbalimbali ya kisiasa, kichama pamoja na kiuchumi. Amesema kwamba moja ya jambo muhimu ambalo alimsisitiza Nchimbi alipomtembelea ni umuhimu wa kupata Katiba mpya na kushughulikia masuala ya rushwa .


View: https://www.youtube.com/live/ieUrniUezG0?si=UfWUqNulWAE6F8Ji

Amesema kwamba baada ya kuona taarifa alimpigia hakupokea, lakini anasema baada ya kusikia amevuliwa uanachama alimpigia lakini simu haikupokelewa wala ujumbe kujibiwa.

Hata hivyo amesema kuwa kuna taarifa kuwa amenyenganywa simu zake.

Aidha amedai kuwa kumekuwepo na madai kuwa kauli kuhusu katiba mpya ndizo zimechangaia kumtia matatani.

Warioba ameongeza kuwa kwa sasa kusema ukweli ni jambo ambalo linaleta changamoto na misukosuko.

Ameyasema hayo wakati akichangia mada kuhusu hali ya Demokrasia nchini katika jukwaa la Demokrasia ambalo limeandaliwa na wadau ikiwemo TLS, TWAWEZA , LHRC na UDASA

Sambamba na hayo Warioba amesema kwamba anasisitiza umuhimu wa katiba mpya kupatikana mapema kabla ya chaguzi zijazo ili kuepusha hali iliyojitokeza kwenye chaguzi zilizopita, amesema kama Katiba haitapatikana uenda hali itakuwa mbaya zaidi kwenye chaguzi zijazo.
 
Kazi kwelikweli,huyu anamfahamu Nchimbi yule anamfahamu Babu Deo!😀
 
huyo jamaa ya chanzo yuko vizuri sana hata anavyoongea tu kwa utulivu, lugha imenyooka, grammar imekaa sawa, i mean, he sounds smart.

kudos to him ...
 
Hivi mtu mkubwa kama yule mwenye cheo cha pili kwa ukubwa mpaka unyang'anywe simu ina maana huna ulinzi wa kutosha? Ule ulinzi tunaona huwa ni feki? Mara Lissu kakamatwa, mara Heche kadakwa, ina maana hawa viongozi wazito huwa hawana ulinzi imara au wanazidiwa na maadui zao? Maadui wakija kukukamata inatakiwa walinzi wako ndio wakupambanie kufa na kupona usikamatwe kindezi
 
Hivi mtu mkubwa kama yule mwenye cheo cha pili kwa ukubwa mpaka unyang'anywe simu ina maana huna ulinzi wa kutosha? Ule ulinzi tunaona huwa ni feki? Mara Lissu kakamatwa, mara Heche kadakwa, ina maana hawa viongozi wazito huwa hawana ulinzi imara au wanazidiwa na maadui zao? Maadui wakija kukukamata inatakiwa walinzi wako ndio wakupambanie kufa na kupona usikamatwe kindezi
Dah we jamaa?? Hujui kama huyo VP walinzi wake ni waajiriwa wa hyo hyo serikali ya SISIMKA na hujui nchi hii SISIMKA ndio tasisi yenye nguvu kuliko zote mpaka wanachi watapozinduka toka usingizini?
 
Back
Top Bottom