Dkt. Mpango: Kodi si tatizo Bandarini

Karibuni tutaambiwa tufunge mikanda tena ilhali ile ya miaka ya 70 waliyoagizwa wafunge mababu zetu hadi leo hawajafunguliwa!
 
Hivi kweli kabisa tumekosa washauri wazuri wa uchumi kwa nchi yetu?
Nchi ambayo 50% ya mapato yake inatumiwa kulipa mishahara na bado Kuna watu wana jeuri.....
Inasikitisha kafeli uchumi na ni ishara kwamba ataendela kufeli kwa miaka mitanoi
 
Natafakari kwa sauti:
J. K. Nyerere alibana kwa kiasi chake,
A. H. Mwinyi akaachie kidogo,
B. W. Mkapa nae akaja akabana,
J. M. Kikwete akalegeza, sasa kaja
J. P. Magufuli... mwendo ndo kama ulivyo.. Mie nadhani ni nyakati tu zinaongea. Wote wamefanya/wanafanya kwa kadri ya utashi waliojaliwa na Mungu. Tumpe muda JPM.
 
Ni bora kuwa na mizigo michache inayolipiwa kodi kuliko kuwa na lundo la mizigo ya mafisadi isiyolipiwa kodi. Hapa kazi tu
 

Na viongozi wetu wa dini hata kidogo kukosoa kauli tatanishi wao wako kimya. Penye makosa lazima ukweli usemwe. Siyo sahihi kumshusha aliye juu ili aje chini. Ni sahihi aliye chini kumpandisha. Katika hili mimi binafsi naona haiko sawa.
 
japo amekurupuka, ni mapema sana kupima uhai kwa bandari kwa miaka 3 au 5 ijayo.

mbegu lazima ioze ili iote.
 

Bandari. Ilikuwa ina kazi nyingi, mizigo mingi, wafanyazi walikuwa busy, lakini mapato ya bandalini yalikuwa yakiwekwa mifukoni. Wakubwa wa custom wengine walikuwa na nyumba 75. Wafanya biashara waliokuwa wakigawana pesa hizi wafanyakazi majipu sasa wanashock, shock ikiisha na kufanya biashara kwa sheria za nchi mambo yatakuwa sawa.
 
hapo unachangia,huku machozi yakikulenga lenga!
 
Kwenye Maelezo Yangu Kuna Sehemu Nilipolitaja Neno VAT?
 

Safi sana.

Ni lazima sheria na taratibu zifuatwe.
 
Na viongozi wetu wa dini hata kidogo kukosoa kauli tatanishi wao wako kimya. Penye makosa lazima ukweli usemwe. Siyo sahihi kumshusha aliye juu ili aje chini. Ni sahihi aliye chini kumpandisha. Katika hili mimi binafsi naona haiko sawa.
Wakikosoa nyinyi ndio wa kwanza kuwaambia wa-deal na waumini wao. Hii nchi ina wanafiki balaa!
 


Kutoka magari 3500 hadi 1,500 tathmini je kati ya magari 3500 mangapi yalikuwa yanalipia ushuru, hatuwezi kusema magari yanayohudumiwa kwa sasa kuwa ndio yalikuwa yanalipiwa ushuru na ambayo hayapo hayakuwa yanalipiwa la hasha lazima tuweke makadirio kama magari 2500 hivi ndio yalikuwa yanalipiwa. Sasa swala lingine ni kwamba kati ya hayo magari 1500 yapi ni ya transit maana yake hayalipiwi ushuru wa hapa nchini lazima yatakuwa kama 800 maana nimewahi kufika bandarini kuona magari ambayo hawa wageni wanayatoa ni mengi sana. Tukubali lazima kuna shoti ya ushuru je serikali itaendelea kutegemea ushuru wa viwanda vya ndani na kodi za wananchi tukizingatia hatuna viwanda kiivyo lol hapa KAZI KUBWA ni kufikiria jinsi ya kupata fedha kwa ajili ya kuendesha serikali maana DENI ambalo serikali inalipa nje ni kubwa sana Eh mwenyezi MUNGU TUSAIDIE.
 
Siyo suala la udhibiti. Kama ilikuwa ni suala la udhibiti wa ulipaji wa kodi, uchambuzi ulifanywa na kugundua tatizo ni mlipa kodi au au sera ya kodi? Nielewavyo mimi tatizo ni tozo jipya la VAT ambayo halihitajiki kwa mizigo inayopitia bandari yetu kwenda nchi za jirani.

Kama kwenu hakuna bandari sawa; lakini mimi naelewa bandari ni kitega uchumi na kina wajibu wa kimataifa kwa nchi zisizo bandari zinazopakana na nchi yenye bandari. Azimio la UN linataka nchi yenye bandari kupitisha mizigo ya nchi zinazopitisha mizigo yao kwa tozo za kodi za haki na halali. VAT si haki wala halali kutozwa kwa transit good.

Hayo ni ya CCM pekee.
 
Hivi mizigo ya wizi inaumhimu gani wa kuwepo ni bora ibaki michache ambayo unalipa kodi hakuna namna nyingine.
 
Kwenye Maelezo Yangu Kuna Sehemu Nilipolitaja Neno VAT?
Nakufundisha ujue hill kwa kuwa unawaunga mkono wazembe kwenye uvivu wa kufikiri. Amka wewe!! Unakosoa kitu usichokijua. Ndio tunakufundisha hivyo ukawaekeze kwenye kijiwe chenu pale!!
 
Hayo ni makadirio yako ambayo umekadiria wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…