Dkt. Mathayo na Ana Kilango: Same "Wachina" wa Tanzania mpaka "VILAZA" wa Kilimanjaro

Mimi ninachoona hapa ni ushabiki mkubwa unaofanywa na FMES bila kujibu tuhuma halisi zilizotolewa na Bangusule. Bangusule ametoa tuhuma kadhaa kubwa. Moja ni kuhusu wilaya ya Same kufanya vibaya kielimu, pili ni suala la ugonjwa uliokumba zao la mpunga, tatu ni ubovu wa barabara, na nne ni ufyekaji wa misitu ambao umesababisha kuharibiwa kwa vyanzo vya maji. FMES anakuja na hoja kwamba mbunge Anne Kilango amechimba visima 30 na kutoa msaada wa baisikeli 20 kwa walemavu. Huu ni upotoshaji mkubwa wa mada na hakuna jibu liliotolewa kuhusu tuhuma alizotoa Bangusule.

Mkuu FMES, tuambie katika tuhuma nne alizotoa Bangusule, mbunge wako Anne Kilango amefanya nini katika kuzitatua? Visima vya maji siamini kama vinatumika kumwagilia mpunga. That is insane! Taumbie visima vyako 30 vinahusiana vipi na ugonjwa uliokumba zao la mpunga. Tuambie visima vinahusiana vipi na wanafunzi kufanya vibaya katika mitihani yao. Tuambie visima vinahusiana vipi na ufyekwaji wa misitu na uharibifu wa vyanzo vya maji.
 


Mtanzania

.....umeeleza vizuri sana ni kw anji agani kiongozi anahitajika kwa jamii.....na anategemewa vipi.......

........bangusule kaleta concern....which is ok as a concern citizen....na concern yake.............does apply sehemu nyingi tu nchini.........

.....now.......check hiyo highlight ya kwanza in red...........tell me how do one arrive to such a conclusion.......!!!

....sidhani kama itakuwa ni kumtendea haki Mh Mbunge kumsema Mbunge eti kuna maradhi ya mpunga na yeye hakuwa na msaada wowote kwa wakulima.........how do one substantiate this claim...........kwa ambao tumekulia kule kajunjumele....tunatakiwa tulielewe hili jambo better than anybody........nafikiri unanisoma............

........Mtu unaweza kuwa na hoja nzuri sana........lakini ukishindwa namna ya kui-present.............mtu anaweza kuku-ignore.....ukashangaa........

......bangusule ana valid concerns......lakini zinaelea......na ndio maana akina Ogah.....wame-comment walivyo -comment..........

.......bangusule should now tell us amelifanyia nini au ana mpango wa kulifanyia nini jimbo lake.........

Kuna mtu hapa kazungumzia suala la wabunge kuwa na ToRs na Performance indicators........wow it might be good idea to start with.....however, we should be able to see and say Mh Mbunge did 1, 2, 3..........to the satisfaction of who......this is debatable.......
 
Bangusule hakusema hawa wabunge ni vilaza. Alichosema ni kuwa Mwalimu akifufuka atawaita watu wa Same ( yeye mwenyewe akiwemo) kuwa vilaza wa Kilimanjaro. Kuuita uongozi wa wabunge waliopo mbovu ni haki yake kama mpiga kura. Mimi sioni alipotukana.

Re: Dr.Mathayo na Ana Kilango: Same "Wachina" wa Tanzania mpaka "VILAZA" wa Kilimanja

- Unajua hata mwenye makengeza hawezi kumbiwa ona hapa, wewe huwezi kuiuliza hoja au kutoa ushauri kwa kiongozi uliyekwisha muita kilaza, that is insane kama sio insanity, halafu ukategemea kujibiwa kwa heshima na hoja, ndio hasa upunguani, ukitaka hoja utajibiwa kwa hoja, lakini ukishaita kiongozi ni kilaza basi wewe ndiye kilaza wa kwanza na hutakiwi kujibiwa kwa ustaaarabu zaidi ya kuambiwa wazi kwamba wewe ni kilaza sasa mebngine yote yanakuwa ni pure nonesense hata kama unasaidiwa na wengi walio na mawazo kama yako yaani yanayoona kuitwa kwa Mbunge aliyechaguliwa na wananchi wa Same East, kwamba ni kilaza kwa sababu unazozijua wewe ambaye hukumchagua na wala huwezi fanya anything kuhusu ubunge wake.

- Kwenye topic moja hapa JF, hivi hivi mliwaita wandishi wa habari vilaza nilipowajibu on vilaza line, forums nzima ikaja juu kwamba kilaza ni matusi na yasiruhusiwe hapa JF na topic ikafungwa, sasa leo mmegeuka wale wale kwamba eti kumuita kiongozi kilaza wakati kilaza ni wewe mwenyewe kwa sababu huna sababu za msingi zaidi tu ya kutaka kujionyesha huku ukiungwa mkono na mnaofanana kwa akili, kama unataka kujadili hoja kwa ustaarabu basi next time ondoa matusi ambayo naona hata Mods wameyakubali, hapana wakuu hatuwezi kubadili the rules of the game kwa sababu tu ya kumtukana Mama Kilango, amelifanyia mema mengi sana taifa letu, kama kuna ambao hamuwezi kuonyesha shukrani kwake, kuna ambao tunaouthamini sana mchango wake kwa taifa hili ana atakumbukwa sana na vizazi vivyajo kwa kuweza kusimama na kuhesabiwa.
 


- Tatizo lako mkuu wangu ni kwamba unamalizwa sana na chuki za binafsi bila hata hoja ya msingi, sasa tizama hizi quote zako hapo juu kama zinafanana, ndio maana ninasema hivi wewe ndiye kilaza namba moja hapa kwa sababu huna hata clue ya unachokisema, one minute uansem one thing, halafu next minute unasmea another, make up your mind unataka nini hasa, maana hatuwezi kukusaidia kama wewe mwenyewe unajichanganya kama hapo juu.

Thanxs!
 


- Again tizama maneno yako mwenyewe, kule juu umesema nimetoa ushahid lakini chini kwa sababu nimekubana sana mbavu umebadilika na kujaribu kula mamneno yako mwenyewe, that is you na kujaribu kubadili hoja yangu kuhusu baiskeli yes kwangu ni big deal tena sana inagwa kwako sio kwamba wananchi walioshindwa kutoka nje almost all their life leo wamepatiwa chombo cha kuwawezesha kutoka nje na kushiriki kwenye maendeleo ya jimbo lao, kwako ni nothing na insane, labda kwa wasiokujua maana tunaokujua vizuri hizi ndio tabia zako za ajabu ajabu na kuropoka maneno bila kufikiri, kama vile wkenye ishu ya Dr. Masau, ukaropoka ropoka mpaka ulipokamamtwa.

- Eti unasema visima vya maji 30 vipya wka jimbo huko vijijini sio big deal na kuna watu wenye ehshima zao wanakuunga mkono maneno ya dhartau wka wananchi namna hiyo, je wewe uliwahi kutoa visima vingapi katika masiha yako mkuu kwa kijiji chochote kile cha Tanzania, licha ya Same East ambalo wala sio jimbo lako? Eti kabla ya hivi visima kuwekwa m,aji yalikuwa yanapatikana wapi? Au ni wewe ndiye uliyekua unawapa? Mkuu ukipata nafsi nenda Same East ukaone maendeleo, huyu Mama ni mpaka atakapoacha mwenyewe, hapewi ubunge na wewe huku JF, hapana anachaguliwa na wananchi, na wananchi wa Same East sio wajinga au vilaza kama wewe, shughuli za maendeleo na sifa za mbunge wao kwa kazi za jimbo na taifa zinafahamika sana mkuu, ngoja tuendelee kukuwekea ushahidi hapa chini.

Thanxs!
 
Kama wamefeli mwambie mkuu wa wilaya akawachape bakora hao walimu
 
Mkuu wangu naomba tuanze mwanzo, ona chini jinsi mbunge alivyoingia ubunge wa Same East, maana ni lazima tuanzie alikoanzia na hili jimbo alimtwanga mbunge fisadi.


 
Jamaa anaona Same tu ndio wamefeli aulize Lindi,Mtwara mbona wanafeli miaka yote na hakuna anayeshtuka
 
Baada tu ya kupata ubunge wa Same East, Mbunge mpya alikwenda Malasyia na Indonesia, ambako akishirkiana na wabunge wengine wa huko Kilimanajro aliweza kuwaleta hawa wakulu ambao wamufanyia mengi sana kielimu mkoa mzima na hasa jimbo la Same East, soma chini hapa;-


 

- Haya wewe unasema elimu imeshuka huko Same, kwa sababu ya mbunge wa sasa, hawa ambao ni wahusika wakubwa wa kuimarisha elimu kitaifa, walipokwenda huko Same na kilimanjaro kwa ujumla, hawakusema kuwa kushuka kwa elimu huko ni tatizo la mbunge au wabunge wa Kilimanjaro, kama unavyodai.
 
Je taifa linaonaje kazi ya Mama Kilango mbunge wa Same East, kwa jimbo lake na taifa pia? Hebu soma kidogo hapa chini;-



....Itaendelea..........!
 
Jamaa anaona Same tu ndio wamefeli aulize Lindi,Mtwara mbona wanafeli miaka yote na hakuna anayeshtuka

Looh! statements kama hizi ndio zinanisikitisha sana. Inaelekea kuna Watanzania wamekata tamaa kweli kweli mpaka wanaona kila jambo ni sawa tu.

Anayelalamika anaonekana ndio mjinga na wanaokaa kimya ndio wanajua hali halisi.

No wonder tuna wabunge vilaza bungeni na ukifika uchaguzi bado wanashinda tu. Halafu tunaanza kupiga kelele kwanini hatuendelei?
 
Again jhapa chini ni uchambuzi wa wataalamu wetu wa elimu Tanzania, ambao ni wasomi waliobobea kuhusu elimu, sasa nimesoma yote hapa chini ya uchambuzi wao, sijaona hata mahali pamoja wakilaumu wabunge kuhusu kushuka kwa elimu ya taifa zima na sio jimbo moja tu akama unavyotaka tuamini hapa mkuu, sasa kule elimu zaidi hapa chini ya sababu hasa ya kushuka kwa elimu ya shule zetu za msingi, haina anything to do na mbunge wa Same East, bwa! ha! ah! ah! ah!


....Itaendelea........!
 
Anayelalamika anaonekana ndio mjinga na wanaokaa kimya ndio wanajua hali halisi.

- Unapoamua kulalamika basi lalamikia panapotakiwa, lakini huwezi kukurupuka tu na maneno ya kuita wabunge waliochaguliwa na wananchi wao kuwa ni vilaza bila sababu maalum, otherwise inakuwa vigumu kujua kilaza hasa ni nani hapa, kabla hujaita mbunge mmoja kialza hebu tupe mifano wabunge ambao sio vilaza ambao in three years za ubunge wao wamebadilisha mifumo ya elimu katika majimbo yao na sasa wanaweza kuwa mfano wa kuigwa na wengine. Ni kweli kama huna ukweli ni vyema kunyamaza kuliko kuharibu majina ya viongozi bure, hapa Jf sio mahali pa kutukana tu kiongozi kwa sababu umeamka leo unajisikia kutukana kiongozi, naona kuna mnaoikubali hii tabia lakini hatutasita kuikataa kwa nguvu zote.

No wonder tuna wabunge vilaza bungeni na ukifika uchaguzi bado wanashinda tu. Halafu tunaanza kupiga kelele kwanini hatuendelei?

- Kwenye hili ukweli uko wazi kwamba tunaowachagua ndio vilaza zaidi, kwa sababu elimu imeshuka kwa taifa zima, sasa tunawarudishaje wabunge wale wale bungeni kama hii nayo ni hoja nzito?, ina maana sisi wananchi ndio vilaza zaidi tumewachagua weee lakini hakuna mabadiliko, tatizo ni letu wananchi kwanza baadaye ndio viongozi.

Kama ni ukilaza basi sisi wananchi ndio vilaza tunaowachagua, au?
 

- Hivi ni mbunge gani anayeweza kuatatua tatizo hili hapo juu?
 

Mkuu Ogah,

Matatizo ni hayo hayo hata kule kwetu Kajunjumele. Si niliwahi kuandika, kwanini migomba
iwe na afya nzuri Rungwe, ukifika tu Kyela unakuta imefifia na hata mazao yake hovyo kabisa.

Tatizo kubwa ni uongozi. Enzi za Nyerere hao mabwana shamba walikuwa wanawajibika. Leo hii sijui kwanini hata tumeajiri mabwana shamba ambao wanakaa ofisini mjini na hakuna wanachofanya.

Hapo ndipo uongozi unapokuja, ukiwa na wanaoelewa wajibu wao kama ambavyo nimekuwa nikitumia mfano wa prof. Mwandosya, utakuta bado viongozi na watendaji wengi wa wilaya wanawajibika na hukutani na hilo tatizo sugu kwenye nchi yetu la elimu mbovu, kilimo kibovu nk. kwa kiasi kikubwa. Kuna wilaya zina nafuu sana kuliko wilaya zingine.

Ukipita kwenye wilaya za wasanii, waulize wananchi lini wamemwona bwana shamba? Huenda sasa hata hawaelewi bwana shamba anafanya kazi gani. Wanaonekana mabwana mifugo tu, wakivizia nyama wananchi wanapochinja mifugo yao.

Ukiwaambia wananchi wawabane viongozi wao kwa maendeleo duni, wapambe wanakuja juu, wanaanza kusema unajiandaa 2010. Ni ujinga ujinga mtupu umejaa!

Wenzetu wanajua kweli kulalamika, hata akianguka na kuvunjika mguu kwenye snow anawalalamikia council kwanini wameshindwa kusafisha barabara mpaka snow inaganda? Mpaka wanamlipa. Mbongo atakuambia wewe sio makini kwanini uanguke.

Mimi ushauri wangu ni mmoja kwa vijana mnaojua maana ya maendeleo na ambao kweli mnataka mabadiliko, hiyo 2010 inakaribia. Chukueni forms na huenda wakati umefika wa kuwaonyesha hao yes we can't kwamba yes we can kwa vitendo.

Ukiwa mchapa kazi na kama huna lengo la kushinda Dar na Dodoma ukivizia allowances kwenye kamati, kuna mambo mengi sana unaweza kuyafanikisha kule wilayani. Mambo mengi kinachotakiwa ni mobilization ya resources ile ile ambayo iko wilayani.

Hii ya wabunge kushinda Ulaya kutafuta vitabu na vifaa vingine ambavyo hata havikidhi haja ya kule kwetu, kisha kuongozana na waandishi habari wa kulipwa, lipenenge na mdundiko ni usanii wa hali ya juu mno! Mungu isaidie Tanzania.

Toka nimeanza kumfuatilia prof. Mwandosya sijawahi kuona akitafuta Waandishi wa habari wa kwenda kumwandikia anayoyafanya kule jimboni kwake. Aliyesema chema chajiuza na kibaya cha jitangaza hakukosea kabisa. Timiza wajibu wako, wananchi watajua, wala sio wajinga.
 
Originally Posted by Kaizer
Hivi kazi ya wabunge ni KULETA maendeleo?

Kumbe ni nini?

Swali la Kaizer ni la msingi.

Dhana hii ya kumwona Mbunge ndiye anayewajibika kwa maendeleo ya endeo lake ndiyo inayoturudisha nyuma kimaendeleo. Dhani hii inawatutumua Wabunge kujiona ndiyo wenyewe, wanayoyasema lazima yatekelezwe nk. Kibaya zaidi, ndiyo dhana inayolipeleka Taifa kwenye siasa zaidi kuliko utendaji.

Kimsingi, Mbunge ni mwananchi, ni mwakilishi wa wananchi katika maamuzi na kutunga sheria. Mbunge si Serikali, hana bajeti ya miradi ya maendeleo, hapokei kodi. Serikali ndiyo inayopokea kodi, ndiyo yenye bajeti. Ndiyo inayopaswa kutekeleza miradi ya maendeleo. Mbunge ni sawa na diwani katika kata na Halmashauri yake.

Kwa kuwa inadaiwa kuwa kodi zetu, pamoja na mapato mengine ya Serikali hayatoshelezi mahitaji ndipo suala la wananchi kuchangia ili kutekeleza miradi linakuja. Inapotokea suala la kushirikisha wananchi ndipo diwani na Mbunge wanapohitajika sana ili kupitisha maamuzi na kuwashawishi wananchi.

Msimamo wangu:
Mimi naomba hivi; tujenge tabia ya kuimarisha utendaji na watendaji. Tujenge tabia ya kuwafanya watendaji wawe wawajibikaji. Kazi ya diwani na wabunge iwe ni kusimamia Serikali kuu na serikali za Mitaa. Wanaopaswa kuwajibia wawe ni Serikali yaani watendaji.

Hofu yangu:
Tunapojenga mfumo au mtazamo 'Mbunge ndiye mleta maendeleo' tunakuwa tumemwinua sana kiasi cha kujiona yupo juu ya Serikali hali inayoweza kuathiri utekelezaji wa mipango ya maendeleo hasa ile ya muda mrefu. Mbunge atapenda mipango ya muda mfupi ili kuonyesha alichokifanya katika muda mfupi. Atafanya hivyo kwasababu anataka kura za ndiyo.

Hofu yangu ni kujenga Taifa la wanasiasa. Wanasiasa hawajengi nchi, wanaojenga nchi ni watendaji. Tunapokuwa na Taifa lililojaa wanasiasa, kitakachopewa kipaumbele ni michezo ya kisiasa badala ya kutafuta teknolojia na kutekeleza masuala ya maendeleo.

Kwa mfano Mkuu bangusilo anatoa hoja kuwa Mama Anne Malecela (MB) hafai kuwa Mbunge kwa kuwa kidato cha nne wamefeli mitihani. This is redicolous! Hapa Mbunge kama mwananchi, alaumiwe katika jambo ambalo hakulitekeleza.

Hoja ambayo ingeleta msingi, ilitakiwa kuwa, kwa mfano: walimu katika shule hizo hawapo/hawatoshi na katika bajeti kulikuwa na code ya kuajiri walimu, Serikali haikuajiri na Mbunge hajaihoji Serikali. au kulikuwa na tatizo la vitabu shuleni, serikali ilipendekeza vununuliwe lakini madiwani/Mbunge walikataa kupitisha bajeti ya kununua vitabu. nk,

Hoja za namna hii, ndiyo zenye maana yaani zinawajibisha wataalam/watendaji. Mbunge au diwani anawajibika kwa kuto wasimamia watendaji au kukwamisha mipango mizuri ya Serikali.
 

Mkuu Nziku,

Unapotosha kabisa dhana ya mbunge kuleta maendeleo au kusukuma maendeleo kwenye jimbo lake.

Haina maana yeye ndiye anaamua nini cha kufanya au yeye ndio anatoa resources za kufanya hayo maendeleo yatokee.

Mbunge ndio kiongozi aliyechaguliwa na wananchi ili awasaidie kutatua matatizo yao. Sasa kama kuna shule mbovu, ni wajibu wa mbunge kuwakutanisha wadau wote na kuangalia namna ya kuongeza ubora.

Kama kuna mabomba yamejengwa na wafadhili, wameondoka na maji nayo yamehama nao, ni wajibu wa mbunge kuangalia kutafuta solution kwa kushirikiana na viongozi wengine wa wilaya pamoja wananchi. Kwanini wafadhili wakiondoka na maji yakauke?

Kama kilimo cha kawaha au mpunga kinaanguka, ni wajibu wa mbunge kupata majibu ya kitaalamu kupitia vyanzo mbalimbali na ikiwezekana ku mobilize resources iliyopo ili kusaidia kutatua tatizo.

Kwa mimi ningetaka mbunge wangu awe a troubleshooter na sio mropokaji tu. Awe na uwezo wa kuwakutanisha watu pamoja kwenye mambo ya maendeleo na sio mtu wa kuwagawa watu.

Aweze kuibana serikali kuu, aweze kuibana halmashauri ya wilaya kwa niaba ya wananchi wake ili watekeleze ahadi walizoahidi, ili miradi wanayoendesha iwe value for money nk.

Nimeshangaa kuona idadi kubwa ya wana JF wanafikiri kazi ya mbunge wa Tanzania ni kwenda kupiga kelele kule Dodoma. Eti kukusanya matatizo ya wananchi na kwenda kuyawakilisha bungeni, nonsense, wala hata huhitaji kusubiri bunge kuwakilisha matatizo yalipo. Kama umeona tatizo, ni hapo hapo kuanza kutafuta solution, kama haiwezekani wilayani, basi huko mkoani, huko wizarani, huko bungeni nk.

Wasanii wetu wengi hawafanyi kitu, anapiga kelele siku moja bungeni, kisha anarudi kwa wananchi na kuwaambia mmenisikia bungeni?
 
Hapa sitashangaa Anna Kilango (aka Mrs John) asipokalia hicho kiti 2010. This is sabotage. Ukiwa mkweli siku zote watu watakuchukia>
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…