Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,703
- 218,239
Taarifa hizi Muhimu kuhusu Wageni na watoa mada kwenye kikao cha vyama vya siasa kilichoandaliwa na TCD kitakachofanyika Dodoma hivi karibuni , zimepatikana leo kwenye Mkutano na waandishi wa habari ulioitishwa na Chadema kwenye ofisi za chama hicho huko Kinondoni .
Dr Mahera ndiye Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi ya Tanzania , na ndiye aliyesimamia uchaguzi Mkuu wa 2020 , uchaguzi ambao baadhi ya wagombea walitekwa na kupigwa , Kutupwa maporini na wengine kupewa kesi na TAKUKURU , wengine wakipewa kesi za uhujumu uchumi na mauaji ili wagombea wa ccm wapite bila kupingwa , Huyu ndiye mtoa mada mkuu kwenye mkutano wa TCD .
Zitto Kabwe ndiye kiongozi wa TCD aliyetoa mwaliko kwa MTUKUFU MAHERA ili atoe mada ya kidemokrasia siku hiyo .