Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Tumeboresha miundombinu, tumejenga barabara na kuweka taa. Tabora sasa kama Toronto

CCMkuelekeaUchaguzi

Senior Member
Aug 18, 2015
179
77
4.jpg

Umati wa watu uliofurika kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi kwa ajili ya Mkutano wa Kampeni ya CCM mkoani Tabora leo tarehe 21 Septemba 2020

Baada ya kuwasili na kukaribishwa, awasifia wana Tabora kwa ushiriki wao katika kutafuta uhuru. Amesifia Tabora ya leo kwa kuwa na nyumba nzuri nzuri tofauti na zamani.

Anaendelea kusifia barabara za lami. Anakumbushia kuwa akiwa Waziri wa ujenzi Tabora ilikuwa na kilometa chache zaidi za lami Tanzania.

Anakumbushia kuwa 2015 aliahidi mambo mawili; kutatua tatizo la maji na pili kuimarisha miundombinu ya usafiri.

Anasema ahadi hizo mbili zimetekelezwa.

Maji
Mradi wa maji wa kutoa maji Ziwa Victoria kwenda Nzega na Tabora kwa gharama za bilioni 600. Mradi umefika 92% na anaamini akirudi tena ataenda kuzindua. Mradi umefaidisha vijiji takribani 500.

Sambamba na huo mradi, miradi mingine takribani 50 imetekelezwa.

Miundombinu
Kupitia mradi wa ULGSP (Urban and Local Gvt. Strengthening Program) tumejenga barabara nyingi za lami na kuweka taa. Anasema Tabora imekuwa kama Toronto.

Anaeleza kuwa Tabora kwenda Nzega ilikuwa vumbi tu, kwenda Itigi au Manyoni ilikuwa vumbi kiasi kwamba ukifika wanajua umetoka Tabora kwa vumbi unalokuwa nalo.

Anaeleza mpango wa kujenga lami hadi Kigoma Nyakanazi, imetengwa Bilioni 567 za lami. Pia kwenda hadi Sikonge hadi katavi Km 359 pamejaa Makandarasi

Pia anagusia ujenzi wa Reli ya kisasa toka Dar-Dodoma-Tabora-Mwanza/Kigoma na kwenda hadi Kigali. Pia itafika Burundi. Lengo ni Tabora kuwa hub ya kibiashara.

5.jpg

Chopa ya Kampeni ya Chama cha Mapinduzi CCM ikipiga Saluti kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Mgombea Urais, Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
 
Back
Top Bottom