Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli, Oktoba atavuna alichopanda

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,854
35,862
Mabibi na mabwana heshima kwenu na moja kwa moja kwenye mada.

Kiswahili lugha ya mama zetu iliyo shehenishwa na semi mbalimbali, ama kwa hakika ni kitamu kweli kweli.

Hujafa hujaumbika, utavuna ulichopanda, usitukane wakunga, usiwatukane mamba, nk nk ni baadhi ya semi hizo ambazo kwa hakika zinamhusu sana leo, nguli au jembe letu bwana jiwe, kama anavyopenda kujiita yeye mwenyewe.

Mkuu wetu huyu kwa kweli katenda mengi katika kipindi chake. Kwa hulka za kibinadamu katenda yote yaliyo mema na yaliyo fyongo. Yeye kama binadamu yapo mema mengi kufanya na pia yaliyo fyongo kwani yeye siyo malaika wala si Yesu Kristo (cc. Kange).

Yote hayo binadamu sisi tuliyashudia kwa namna mbalimbali. Mwenyezi Mungu naye akiyashudia kwa namna yake.

Katika kipindi chake kuna walioshuhudia madege yakinunuliwa, ma flyover, madaraja kama ya busisi yakijengwa. Madaraja ya salenda na barabara za kuizunguka Dodoma yakijengwa kupendezesha majiji. Ma SGR, viwanja vya ndege kama vya Chatto, Msalato, viwanda nk vikijengwa.

Mengine yakiwa hata kupendezesha majiji tu! Fursa iliyo je? Ama kweli staajabu ya Firauni.

Yapo maeneo yali sahaulika hapa hapa nchini na kuwa kama si sehemu ya nchi hii:

Ziara ya Kagera, Magufuli usiende pekee tu Wasaidizi wako wanakokupangia kwenda

Hali ya mbaya mno ya barabara Nyakanazi Rusumo vipaumbele vyetu ni nini?

Barabara ya Rusahunga Rusumo mtaji kwa wagombea

Kupo kwingine nako, wengine hata majoto ya mawe waliyaonja kama wafanyavyo mijusi. Kuna waliokumbwa na matetemeko, waliookotwa kwenye viroba, waliopotea, walionusurika mithili ya ngamia kupita kwenye tundu la sindano kama kina mh. Lissu, kuna waliotekwa, nk nk.

Kwa hakika kila mtu au watu wa sehemu fulani wana yao ya kumwelezea nguli huyu kwa namna zao za kipekee. Hii ikiwa ni mithili ya wale vipofu saba waliopata fursa adimu ya kumpapasa tembo na kumwelezea ki vyao vyao.

Kipofu aliyepapasa mkia akidhani tembo ni kama ufagio wa chelewa chelewa, aliyepapasa pembe akidhani tembo ni kama mchi wa kutwangia, aliyepapasa sikio akidhani tembo ni kama blanketi tu nk nk.

Waswahili wanasema chema chajiuza na *kile kingine* chajitembeza. Wengine wakisema "mwana wacha kupiga mayowe waache waone wenyewe" au "penye ukweli uongo hujitenga."

Barabara ipi alijenga mzee Kikwette, ipi Mkapa (rip), ipi jiwe zote tunazijua kama naye anavyozijua. Hii ni siri iliyo wazi. Kila mtu na ashinde mechi zake na si busara kusafiria nyota za wengine kama zako pasipo na kuweka yote wazi. Ndiyo ustaarabu wa kisomi huo.

Itoshe kusema ng'ombe hanenepi siku ya mnada!

Kwa aliyoyafanya mzee baba, yote kabisa "maji ga nyanja" tunayajua vyema na kwa hakika, ni sawia kusema "huko atavuna alichopanda." Ikizingatiwa historia huwa haiandikwi upya.

"Tusimlaumi dobi kaniki ni rangi yake." Huu ni ukweli mchungu.

Alipopanda bangi atavuna bangi kama alivyoipanda yeye mwenyewe kwa mikono yake. Pia atavuna maharage kote alikopanda maharage yeye mwenyewe. Kwenye haya hayupo wa kumlaumu wala wa kumsifu bali mhusika ni yeye mwenyewe na nafasi ya kufanya vinginevyo alikuwa nayo kama yote.

Katika misahafu kwa kiswahili inasema "mwanamke mpumbavu huivunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe." Mwisho wa kunukuu.

Labda kama analo jipya la kutufanyia au kutupeleka mzee baba, basi ilikuwa vyema tukakutana kwenye midahalo ili kwa hayo tusiyoyajua sote tukaswalishana.

Yaliyopita si ndwele kila siku kama watanzania wenye subira kukubaliana kuganga yajayo ni jadi yetu wala si muhani.

Ninawasilisha.
 
UFIPA huwa mnafurahisha sana mara zingine. Hivi viashiria gani mnavyovichukua vinavyoonesha JPM (kwa maono ya mleta hoja) atashindwa kutokana na alichofanya?. What are the main indicators of JPM's failure? Kama ni nyomi mnaona wenyewe. Na hiyo inaonekana Ni Kwa kiasigani amefanya mambo mengi mazuri sana kwa watanzania hasa wa hali ya chini. Jiandaeni kisaikolojia.

Tarehe 28 octoba mtarudi mniambie haya ninayoyasema. Ushindi wa JPM this time haushuki 80%. Huwezi kuilinganisha TL na Lowasa wa 2015. Vinginevyo tuendeleeni kupeana burudani humu JF. JPM ni habari nyingine mtake msitake.
 
UFIPA huwa mnafurahisha sana mara zingine. Hivi viashiria gani mnavyovichukua vinavyoonesha JPM (kwa maono ya mleta hoja) atashindwa kutokana na alichofanya?. What are the main indicators of JPM's failure?. Kama ni nyomi mnaona wenyewe. Na hiyo inaonekana Ni Kwa kiasigani amefanya mambo mengi mazuri sana kwa watanzania hasa wa hali ya chini. Jiandaeni kisaikolojia. Tarehe 28 octoba mtarudi mniambie haya ninayoyasema. Ushindi wa JPM this time haushuki 80%. Huwezi kuilinganisha TL na Lowasa wa 2015. Vinginevyo tuendeleeni kupeana burudani humu JF. JPM ni habari nyingine mtake msitake

Kipi usichoelewa kwenye mada.

"Atavuna alichopanda." Ulitaka avune bangi alipopanda mchicha?

Buku 7 tu hizo hadi akili mnashikiwa?

Kwamba yeye hajui atakachovuna? Majuha wa wapi nyie?

Au ulitaka tumhakikishie kuwa hatavuna alivyopanda?
 
Kila wakati nasoma sredi zako kuhusu ile barabara muhimu sana kwa ustawi wa nchi. Hii barabara inaunganisha siyo tu Rwanda na Burundi tu, inaunganisha Uganda na Kenya (endapo kipande cha km 124 cha kutoka Benaco hadi nyakahanga). Aidha utafiti tulioufanya miaka ile ilionesha kama mzigo unatoka Mombasa hadi kigali kwa kupita juu ya Uganda ni palefu sana ukilinganisha na kupitia Kyaka benaco hadi kigali (masaa 9).

Hiyo barabara imesahaulika kama unavyosema kila wakati. Ila approach yako kuifanya iwe mtaji wa kisiasa ndipo unaichimbia kaburi. Chonde chonde tusiingize katika siasa. Ni barabara nyeti na kama SGR itajengwa toka isaka hadi kigali; kwa vyovyote itatengenezwa tu. Najua uchungu wa kusahau wilaya ya Ngara.
 
Alikuwa ananunua wabunge wa upinzani kwa gharama kubwa sana kwa madai ya kuunga Juhudi.

Alikuwa tayari kuona tukirudia chaguzi kwa gharama ili tu apate kuungwa mkono, hii biashara ilikuwa kichaa sana.

Watanzania tusifanye makosa Jiwe must go out .
Huu mradi aliyemshauri Mungu anamuona
 
UFIPA huwa mnafurahisha sana mara zingine. Hivi viashiria gani mnavyovichukua vinavyoonesha JPM (kwa maono ya mleta hoja) atashindwa kutokana na alichofanya?. What are the main indicators of JPM's failure?. Kama ni nyomi mnaona wenyewe. Na hiyo inaonekana Ni Kwa kiasigani amefanya mambo mengi mazuri sana kwa watanzania hasa wa hali ya chini. Jiandaeni kisaikolojia. Tarehe 28 octoba mtarudi mniambie haya ninayoyasema. Ushindi wa JPM this time haushuki 80%. Huwezi kuilinganisha TL na Lowasa wa 2015. Vinginevyo tuendeleeni kupeana burudani humu JF. JPM ni habari nyingine mtake msitake
Jifariji kidogo

IMG-20200917-WA0213.jpg
 
UFIPA huwa mnafurahisha sana mara zingine. Hivi viashiria gani mnavyovichukua vinavyoonesha JPM (kwa maono ya mleta hoja) atashindwa kutokana na alichofanya?. What are the main indicators of JPM's failure? Kama ni nyomi mnaona wenyewe. Na hiyo inaonekana Ni Kwa kiasigani amefanya mambo mengi mazuri sana kwa watanzania hasa wa hali ya chini. Jiandaeni kisaikolojia.

Tarehe 28 octoba mtarudi mniambie haya ninayoyasema. Ushindi wa JPM this time haushuki 80%. Huwezi kuilinganisha TL na Lowasa wa 2015. Vinginevyo tuendeleeni kupeana burudani humu JF. JPM ni habari nyingine mtake msitake.
Kiashiria kikuu ni hofu waliyonayo kwa Lissu kingine ni fujo kupitia NEC lakini watashindwa tu.
 
UFIPA huwa mnafurahisha sana mara zingine. Hivi viashiria gani mnavyovichukua vinavyoonesha JPM (kwa maono ya mleta hoja) atashindwa kutokana na alichofanya?. What are the main indicators of JPM's failure? Kama ni nyomi mnaona wenyewe. Na hiyo inaonekana Ni Kwa kiasigani amefanya mambo mengi mazuri sana kwa watanzania hasa wa hali ya chini. Jiandaeni kisaikolojia.

Tarehe 28 octoba mtarudi mniambie haya ninayoyasema. Ushindi wa JPM this time haushuki 80%. Huwezi kuilinganisha TL na Lowasa wa 2015. Vinginevyo tuendeleeni kupeana burudani humu JF. JPM ni habari nyingine mtake msitake.
nyomi gani ya kulazimishana kuitana rocal kwa wafanyakazi na wanafunzi kulazimishwa!
 
Jamaa hakuwa na sifa za kura Rais, CCM walichemka sana 2015 sasa yanawatokea puani, watanzania washastuka
 
Kila wakati nasoma sredi zako kuhusu ile barabara muhimu sana kwa ustawi wa nchi. Hii barabara inaunganisha siyo tu Rwanda na Burundi tu, inaunganisha Uganda na Kenya (endapo kipande cha km 124 cha kutoka Benaco hadi nyakahanga). Aidha utafiti tulioufanya miaka ile ilionesha kama mzigo unatoka Mombasa hadi kigali kwa kupita juu ya Uganda ni palefu sana ukilinganisha na kupitia Kyaka benaco hadi kigali (masaa 9).

Hiyo barabara imesahaulika kama unavyosema kila wakati. Ila approach yako kuifanya iwe mtaji wa kisiasa ndipo unaichimbia kaburi. Chonde chonde tusiingize katika siasa. Ni barabara nyeti na kama SGR itajengwa toka isaka hadi kigali; kwa vyovyote itatengenezwa tu. Najua uchungu wa kusahau wilaya ya Ngara.

Unashindwa kuona kwa nini hatimaye siasa inaingia? Ni kwa sababu jitihada zote za kila aina zimeangukia kwenye masikio ya kenge. Angalia nyuzi 3 hizi kwa mfululizo wake. Note pia tarehe za nyuzi hizo tokea well before 2017:

Hali ya mbaya mno ya barabara Nyakanazi Rusumo vipaumbele vyetu ni nini?

Ziara ya Kagera, Magufuli usiende pekee tu Wasaidizi wako wanakokupangia kwenda

Tambua nyuzi zilizo lazimika kuwa za siasa ni baada mno ya jitihada zote kuangukia kwenye deaf ears:

Barabara ya Rusahunga Rusumo mtaji kwa wagombea

Au mkuu wewe uliona baada ya juhudi zote tumwachie Mungu?

Lissu tembelea Rusahunga - Rusumo haraka iwezekanavyo

Kwani maana ya kuwa na wagombea wengi nini kama mmoja hataki kusikia?
 
Nakutakia mafanikio mema
 
Namkumbuka sana Bi.Kirembwe pale anguko lake lilipofikia hali ya kuwa aliamini utawala wake ni wa daima dawamu
 
Alikuwa ananunua wabunge wa upinzani kwa gharama kubwa sana kwa madai ya kuunga Juhudi.

Alikuwa tayari kuona tukirudia chaguzi kwa gharama ili tu apate kuungwa mkono, hii biashara ilikuwa kichaa sana.

Watanzania tusifanye makosa Jiwe must go out .

Nguvu ya umma kwenye sanduku la kura Oct 28 inamhusu sana huyu bwana.

Mola wetu n akazisikie sala zetu.
 
Back
Top Bottom