Dkt. Louis Shika: Undercover informer aliyenusurika kifo ughaibuni?

Inaendelea...
7.Dr. Hakuwakimbia vibaka wa Moscow, kawakimbia watu ambao ni the professional killers.... Wahuni majambazi wa kupora wasingeweza kuwa na nguvu kuzidi serikali eti wamfuatilie mpaka airport ambako kwa hadhi yake na ulinzi ulivyo angeweza kulindwa mpaka anapanda jet lake na kuondoka. Na pia angepata hata wasa wa kuchukua kiasi na fedha nk.... Dr aliondoshwa in rush hour tena kwa ndege maalum ya malkia... Huyu alikuwa ni zaidi ya mtu aliyetaka kuporwa pesa...alikuwa ni kiungo mchezaji katika siasa na vita ya kimataifa... Na alikuwa anagombewa na pande mbili ama zaidi na kwa vyovyote ilikuwa ni mambo ya kijasusi na ushushushu.... Na katika kuondoka huko hakuwa na muda hata wa kufungasha na kuweka mambo yake sawa... Ilibidi aondoke hapo hapo alipokuwa saa hiyo hiyo ili aokoe roho yake, ama abaki na akutane na kilichomtoa kanga manyoya

8. Kurejea nyumbani Tanzania, kujificha na kujitenga kabisa na jamii
Kwakuwa anafahamu vema undani wa kisa kizima katika uhalisia wake, hata safari ya kurudi nyumbanj haikuwa ya moja kwa moja, alirudi zigzag kuwapoteza maboya watesi wake..
Dr. Alikuwa anajua kwa hakika bado anatafutwa. Hivyo akawa ni mtu asiyetulia sehemu moja huku akiishi kwa kujificha na maisha ya chini hasa... Alikata mawasiliano karibia na watu wote, akatumia simu ya hali ya chini kabisa... Akakata mawasiliano na mwenza wake aliyemwacha Urusi... Alijua akimtafuta tu.. Wamemdaka... Mtu aliyetaka kuporwa pesa hawezi kuishi kwa kujihami kiasi hiki... Si mtembezi hana mizunguko ya mbali.. Zaidi ya kwenda kwenye meza ya magazeti kujua nini kinajiri, si mtembezi wa usiku na muda mwingi hujifungia chumbani kwake...hana rafiki na hana mazoea ya karibu sana na watu wengi
9. Kwanini ajitokeze sasa tena kwenye mnada mkubwa?
Kila jambo lina wakati wake na ukitimia jambo husika hujifunua... Dr alifahamu fika ule mnada ungemuweka kwenye macho ya dunia.. Je haogopi tena kufa? Je watesi wake wamekufa wote? Nini kimemfanya ajitokeze sasa? Imethibitishwa polisi kuwa ni kweli ana pesa zake na mmarekani ndio anazishughulikia.. Kwanini mmarekani? Huyu mmarekani huwa hafanyi kazi ya hasara hata mara moja ukiona anakushika mkono jua unamfaa na mengi...hii ishu inaweza kuwa mwanzo wa tamati yenye break through kubwa sana.. Tuwe wapole tuwe na saburi...... .

Mwisho.........
Tumjifunza mengi kwenye ishu ya Dr. Shika, hasa tabia ya kufanya vitu kwa mazoea, kuwadharau wasomi wetu eti tu kwakuwa hawana mwonekano na kuwatukuza wanasiasa wezi...
Funzo lingine ni je tunao wasomi wangapi kama Dr Shika ambao serikali haiwapi heshima na kipaumbele halafu wanatumika na mataifa mengine kiasi cha kuhatarisha maisha yao?
Je tunao wangapi kama Dr Shika ambao tunadhani ni machizi fresh na kuwadharau huko kwenye mishe zetu kumbe wako kazini? Jiulize Dr Shika alivyokuwa ana act low profile kumbe ana mawasiliano na mmarekani na anafuatilia mabilioni yake? Alikuwa anawasiliana nao saa ngapi? Kwa njia gani?

Nimefarijika kuona kuwa kumbe Dr anathamini bado elimu yetu ya kienyeji.. Kubana kende unapopita kwenye mbwa wakali....
Umesikia na hiyo ya mtu aliyelala ukimuangalia usoni anaamka? Kuna siri gani hapo? Hili tutalijadili kwa leo niishie hapa ya haya machache ya Dr Shika...!!!!

NB. Nimeandika kwa muktadha wa mtazamo wangu kulingana na simulizi za mlengwa mwenyewe

Jr
Kiongozi.

Naona umefunga na Jr Trademark:D.

Safi sana Kiongozi
 
Wakati wa2 walipokuwa wanasema "Dr.Shika ni mwenda wazimu" niliingia you tube kuangalia baadhi ya interviews zake...,na haya ndyo niliyoyagundua kutoka kwake;
1.Anazo hoja za msingi anapolielezea jambo lolote
2.Anaompangilio mzur wa mawazo (ascending and chronological flowing of ideas/argue)
3.Hata story ikiwa ndefu,ukimwambia arudie jambo flani ambalo alilitolea ufafanuz dk nyingi zilizopita,analitolea ufafanuz kama ule wa mwanzo bila kuongeza wala kupunguza wazo
M2 mwenye tatizo la uendawazimu hawez kuwa na sifa hzo nilizoziandka hapo juu so,Dr. Shika naona kama anatushika ufaham kwa hiv sasa...,tuendelee kuwa wapole mpaka hapo wakati utakapo tueleza vinginevyo
Pia,ninamashaka na hao Wamarekani inaweza fikia mahali wakamdhuru (kumuua) then wanaweza iambia serikali ya Tz itoe maelezo ya kifo chake,huwa sina imani na Wamarekani hata kidogo!
 
Wakati wa2 walipokuwa wanasema "Dr.Shika ni mwenda wazimu" niliingia you tube kuangalia baadhi ya interviews zake...,na haya ndyo niliyoyagundua kutoka kwake;
1.Anazo hoja za msingi anapolielezea jambo lolote
2.Anaompangilio mzur wa mawazo (ascending and chronological flowing of ideas/argue)
3.Hata story ikiwa ndefu,ukimwambia arudie jambo flani ambalo alilitolea ufafanuz dk nyingi zilizopita,analitolea ufafanuz kama ule wa mwanzo bila kuongeza wala kupunguza wazo
M2 mwenye tatizo la uendawazimu hawez kuwa na sifa hzo nilizoziandka hapo juu so,Dr. Shika naona kama anatushika ufaham kwa hiv sasa...,tuendelee kuwa wapole mpaka hapo wakati utakapo tueleza vinginevyo
Pia,ninamashaka na hao Wamarekani inaweza fikia mahali wakamdhuru (kumuua) then wanaweza iambia serikali ya Tz itoe maelezo ya kifo chake,huwa sina imani na Wamarekani hata kidogo!
Argue=argument
 
Ukitazama vizuri ile video anayohojiwa mapaka unatamani umpe labda mwandishi maswali aulize? Unashangaa kwanini mwandishi hamuulizi Dr maswali tunayobaki nayo kichwani?
Kwa mfano ukisikiiza akisimulia jinsi alivyokuwa anateswa.. Yale sio mateso ya kutakiwa utoe pesa ni mateso ya kutakiwa kutoa habari.. Na after all KGB watakudai pesa za nini....
-unafungwa waya za umeme mikononi live na neutral, unaambiwa sema ama tuwashe! Ukigoma wanawashwa hasi inakutana na chanya unatikiswa mpaka unaona roho inatoka.. Wanakupumzisha kidogo wanauliza tena.... Kustahimili haya mateso bila kuzirai na bila kuongea wanachotoka inahitaji mafunzo maalum
-kinachukuliwa kidole kimoja kinawekwa kwenye ubao unaambiwa sema, ukigoma kinapondwa na nundo mpaka kinasagika kabisa... Ni kwa watu jasiri wenye mafunzo maalum ndio huweza kuhimili maumivu yake.. Dr mkono mmoja kapondwa vidole 3, mkono mwingine vimekatwa
-kuna mateso ya kutisha zaidi yasiyo na stara za kiutu si rahisi kuyasimulia... Haya yote si mambo ya kutakiwa kutoa fedha... Ndugu zetu hawakuweza kabisa kuhoji
 
Back
Top Bottom