Dkt. Louis Shika: Undercover informer aliyenusurika kifo ughaibuni?

Kwanza nimpe pole kamanda wa polisi aliyemu underrate Dr Shika kwamba hana thamani hata ya million... Hawa ndio makamanda wetu wenye dhamana kubwa ya kutulinda.... Tungesema sisi wa mitandaoni isingekuwa shida sana maana huku tuko mix grille, wajuzi na wajuvi wa kila jambo.. Kamanda hakujihangaisha kabisa kupata habari za huyu mtu kabla hajatoa taarifa yake mbele ya kamera.... Kumbe mtu aliyemdharau ni viwango vingine kabisa.. Mazoea yale yale ya kuwaamini wasaidizi na bila kujiridhisha na taarifa zao
Dr Shika ni mtu zaidi ya tunavyomfahamu, kaeleza machache kabaki na mengi, lakini machache aliyoasema yametosha kumchora picha yake halisi katika uhalisia wake..... Twende na dondoo zifuatazo

1. Masomoni Urusi na kuanzisha biashara kubwa
Achana na scholarship za siku hizi za kupeana... Wakati ule ukienda kusoma/kusomeshwa nje... Wewe ni cream... Historia inaonesha Dr Shika alikuwa vizuri sana kichwani tangu sekondari.... Na kwa vyovyote huko Urusi alifanya vizuri pia kitu kilichowavutia wengi...
Ni baada ya kumaliza masomo yake hakurudi nchini bali alibaki Urusi na kuanzisha biashara kubwa, yeye pamoja na washirika wengine ambao asili ya kukutana kwao haiwekwi wazi... Dr. Shika yeye ndio akawa rais wa kampuni kubwa yenye mtandao wa makampuni mengi.. Mafanikio ya haraka ya kampuni hii yaliwagutua warusi na kuanza kumdukua

2. Mafanikio ya kampuni na kumiliki mali nyingi
Kampuni yao hiyo bila kujulikana kwa hakika shughuli zao hasa ikawa ni kampuni inayokuwa kwa haraka mpaka kuwa na uwezo wa kumiliki ndege binafsi... Hapa warusi wakashtukia mchezo kuwa pengine hawa watu ni undercover informers wa wamarekani, na hii kampuni ni zuga tuu... Janja hii hutumiwa na mataifa mengi... Dr. Shika inapofikia hapa huwa na kigugumizi kidogo na bahati mbaya hatuna waandishi wanaojua kuhoji

3. Kuwindwa kutekwa na mateso
Dr. Hapa kuna kitu kikubwa sana anakificha.. Aliliwa timing ya muda mrefu mpaka alipokamatwa nyumbani kwake.. Inawezekana kabisa nyumba ilishakaguliwa yote.... Lakini pia style ya kuondoka naye wakiwa wamemfungia kwenye kabati maana yake huyu hakuwa mtu wa kawaida
Kwa maelezo yake alipelekwa mpaka nje ya mji Kwenye nyumba yenye chumba cha siri chini ya ardhi na kuanza kuteswa, kwa madai kwamba watekaji walitaka pesa kiasi cha USD million moja... Dr hapa pia kasema uongo kuna kitu anaficha pia... Kwa utekaje huo watekaji wangetaka awapigie simu jamaa zake wakate mpunga (ransom).. Lakini Dr Shika anakiri kwamba alitekwa na kuteswa na the professionals toka KGB- shirika la kijasusi la Urusi... Kwa mateso yale hawa walikuwa wanamlainisha aseme yeye ni nani hasa.. Amekuwa mlemavu wa vidole vitano vya mikono.. Mkono mmoja viwili, mmoja vitatu, amevunjwa mbavu tano, na sikio moja limepindishwa kwasasa ya makofi... Majambazi wanaotaka hela hawana mateso ya namna hii.. Haya ni mateso ili ufunguke.. Roma anajua vema..

4. Ujasiri, uvumilivu na utulivu
Dr ana viashiria vyote vya majasusi, pamoja na mateso yote hayo na kujeruhiwa vibaya kabisa lakini hakupaniki wala kukata tamaa alikuwa mtulivu jasiri akisuburi one mistake one goal... Na akajenga nao urafiki yani hakuwa kiburi, unateswa unatukanwa unadhalilishwa unaumizwa lakini baada ya hapo unaenda nao sawa... Hii kitu ina mafunzo maalum.. Dr. Alikuwa mtulivu na mvumilivu mpaka akaweza kutoroka akiwa hoi kabisa...

5. Kutoroka kwake kunaacha maswali mengi, kwanini alibebwa na ndege maalum ya malkia wa uholanzi? Je ilikuwaje? Ni nani walifanikisha hii mipango? Kwanini mmarekani alitoa msaada mkubwa kwake mpaka akaweza kufika nchini salama? Je KGB walikuwa sahihi? Je alifanikiwa kuficha siri kuu ndio maana wamarekani hawakumtupa hata sasa?

6. Vifo vya washirika wake kwenye kampuni
Wenzake karibia wote walikufa kwa kuuwawa.. Yeye kaponea shimo la tewa (kuna maswali mengi sana kwenye hili..... Kampuni lao bado lipo lakini limesimamisha shughuli zake.. Wamarekani wanamsaidia Dr Shika kupata pesa zake! Kaamua kuishi nyuma ya wakati.... Osama alitumia hii mbinu kwa mafanikio makubwa.. Dr kaamua ku act low profile na kujitenga kabisa na harakati za dunia.....


ITAENDELEA........
Huyu Dr ni zaidi ya tubavyodhani, huo ununuzi ipo hesabu imepigwa kisayansi
 
Nakubaliana na wewe. Dr kuna kitu hajakisema na hajakiweka wazi.

1. Alipata wapi mtaji wa kuanzisha a very successful business within a short period of time baada ya kumaliza shule?

2. Ilikuaje ubalozi wa marekani wajihusishe kumtorosha kutoka urusi tena kwa ndege ya malkia wa uholanzi hadi Armsterdam na kisha kuja Dar kama anavyosema.

3. Baada ya kufika hapa nchi alipata wapi nauli ya kumpeleka Malaga Hispania na akaweza kuishi huko kwa miaka 8 hafi aliporudi nchini mwaka 2013.

4. Kwa nini baada ya kutoroka toka Urusi bado amekua na wasiwasi kua warusi watamtafta popote alipo wamuue, wasiwasi wake ni wa nini? Kweli vibaka wanaweza kukufuatilia hadi nje ya nchi wakuue?!

5. Anasema warusi wana chuo cha kufundisha jinsi ya kuua, tena anataja KGB ambayo ni taasisi ya serikali, je alitekwa na KGB au alitekwa na vibaka, vibaka gani wanaweza kusomea chuo kikuu jinsi ya kuua mtu na jinsi ya kumtesa?

6. Anasema hataki kuwasiliana na mke wake wasije kumtambua alipo, kwamba simu zote zinarekodiwa ziazotoka nje, hao ambao anahofu kua watamjua alipo ni wale vibaka waliomteka au watu wengine, vibaka wanawezaje kurekodi au kuingilia mawasiliano ya watu toka nje ya nchi?

7. Dr alikimbilia hispania ili kupoteza ushahidi wa uwepo wake, kisha akarudi Tanzania ili kuwapoteza tena kama wanadhani yuko hispania, ni kina nani hao ambao dr anawakimbia kiasi hicho, wale vibaka waliomteka au wengine?

Dr ana kitu hataki kukisema. Kuna kitu kimejificha nyuma yake.

Zaidi Dr ni loser, huwezi kwenda kusoma ukalowea huko ukasahau hata wazazi wako.
 
Huyu ni double agent kwa kiswahili chepesi, ni mtu aliyesoma mambo ya kutengeneza silaha na chemikali, alivyokuwa kitengoni KBG akasukwa na mashirika ya CIA ale mpunga km kampuni arushe Siri hawa monotov wanapanga nini.
80s mpk 90s mmarekani alikua cha mtoto tu kwahawa jamaa mpaka dola ilipoangushwa baadae,
So Warusi wanatafuta mchawi, na inawezekana kabisa ndugu yetu aliingia line akafanyiwa alivyo leo. Ninahisi 100% mkewe alimset upp.
 
He knows exactly where he is going, when to tell the truth and when to mislead... Na kama nilivyosema waandishi wetu hawahoji wanapokea tu
Waandishi wa kuhoji waliishaisha Bongo lala hii. Tumebakiza waandishi wa mapokeo ya udaku na hekaya. Reasoning capacity imebaki robo kilo.
Mfano siku anatoka polisi anaingia maeneo yake ya unyonge, sijui walikuwa waandishi wale au wacheza pool wa mitaani? kipindi wanamuhoji na kuchukua video ilikuwa kituko.
 
Back
Top Bottom