Dkt. Louis Shika: Undercover informer aliyenusurika kifo ughaibuni?

Dr Luis Shika Afariki dunia siku ya leo

Aliandika Malisa GJ

Dr.Shika alikuwa ni miongoni mwa wasomi wazuri lakini bahati mbaya elimu yake haijaweza kusaidia taifa hili achilia mbali kumsaidia yeye binafsi.

Wengi walimchukulia kimzaha tangu alipoonekana kwenye tukio la mnada wa nyumba za Lugumi (mia tisa itapendeza). Makampuni ya kibiashara yalitumia umaarufu wake kama fursa ya matangazo lakini yakamuacha hohehahe asiye hata na mahali rasmi pa kuishi. Aliwahi kuripotiwa na kituo kimoja cha TV kufukuzwa kwenye nyumba aliyokua akiishi huko Tabata baada ya kushindwa kulipia kodi.

Vyombo vingi vya habari vilikuwa vikimdhihaki na vingine kumuita Kalubandika. Lakini bila shaka vilifanya hivyo pasipo kumjua kiundani *Dr.Shika.*

Ni mzaliwa wa kijiji cha Kalemela wilaya ya Busega, mkoani Simiyu. Majina yake halisi ni Louis Shika Kidola. Yeye na ndugu yake Jeremiah Shika Kidola *(marehemu pia)* walikuwa wanafunzi wenye akili sana na waliofaulu vizuri masomo yao ya sekondari kwa alama za juu na kupata ufadhili wa kusoma udaktari nchini Urusi mwaka 1984 hadi 1991 waliporejea na kuanza kutibu hospitali ya taifa Muhimbili.

Mwaka 1994 Louis Shika alirejea Urusi kujiendeleza kimasomo. Alisomea shahada ya uzamili katika magonjwa ya kuambukiza (MSc in Infectious Diseases) na udaktari bingwa wa magonjwa ya akili Master of Medicine (Psychiatry). Akiwa huko alishirikiana na wenzake kuanzisha kampuni ya usambazaji wa kemikali viwandani iitwayo Lancefort Ltd.

Kwa sasa ni moja ya makampuni makubwa ya usambazaji wa kemikali nchini Urusi, na jina la Dr.Shika lipo kwenye website yao kama Muasisi na Rais wa kwanza wa kampuni.

Inadaiwa shirika la ujasusi la Urusi (KGB) liligundua kwamba akina Shika walipata fedha za kuanzisha kampuni kutoka Marekani kama mkakati wa Marekani kudukua taarifa za Urusi. Kwahiyo baadhi ya viongozi wa kampuni hiyo walikamatwa. Dr.Shika alitekwa na watu waliodhaniwa kuwa majambazi kupewa mateso makali sana ikiwemo kukatwa vidole.

Balozi wa zamani wa Tanzania nchini Urusi, Patrick Chokala mwaka 2017 alinukuliwa na vyombo vya habari kwamba ilibidi kutumia mbinu za "kijasusi" kumnasua Dr.Shika na kumrudisha nchini kwa dharura. Tangu aliporejea alijiingiza kwenye ulevi wa kupindukia kutokana na msongo wa mawazo.

Kwahiyo ukifuatilia historia ya *Marehemu Dr.Shika* utagundua hakuwa "kalubandika" kama ilivyodhaniwa. Ni mtu aliyekua na maono makubwa. Kama si mipango yake kuvurugika huenda angekuwa daktari bingwa na mfanyabiashara mkubwa wa kemikali duniani.

Ni kwamba tu alijikwaa, akadondoka na hakuweza kusimama tena. Serikali ilipaswa kumsaidia kusimama lakini nayo ilimtelekeza. Kwahiyo ameishi maisha ya upweke, masononeko na msongo wa mawazo kwa muda mrefu.

Kampuni aliyoanzisha ya Lancefort Ltd ambayo kwa sasa inamilikiwa na serikali ya Urusi (ilitaifishwa) ina thamani ya $27Bil sawa na TZS 60Trilioni (Bajeti ya nchi kwa miaka miwili).
_
Kwa hiyo Dr.Shika alikuwa anajiita "Bilionea" si kwamba alikuwa anaota. He used to have money. Na hiki ndicho kilichokuwa kinamtesa maana alishindwa kukubaliana na hali yake ya sasa. Hakutaka kuamini kama aliwahi kuwa na pesa.

Kujikwaa na kuanguka ni kawaida katika maisha lakini jambo la msingi ni uwezo wa kusimama tena baada ya kuanguka. Whinston Churchil aliwahi kusema "Success is not final and failure is not fatal. It is the courage to continue that counts"

Dr Shika amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hosipitali ya Nyahunge alioikuwa amelazwa. Kweli dunia ni mapito Shika aliyekuwa bilionea wa kutupwa anakufa kwenye bahari ya Umasikini.

Pumzika kwa amani Mr. mia tisa itapendeza
 
Kwanza nimpe pole kamanda wa polisi aliyemu-underrate Dr Shika kwamba hana thamani hata ya million. Hawa ndio makamanda wetu wenye dhamana kubwa ya kutulinda. Tungesema sisi wa mitandaoni isingekuwa shida sana maana huku tuko mix grille, wajuzi na wajuvi wa kila jambo. Kamanda hakujihangaisha kabisa kupata habari za huyu mtu kabla hajatoa taarifa yake mbele ya kamera. Kumbe mtu aliyemdharau ni viwango vingine kabisa. Mazoea yale yale ya kuwaamini wasaidizi na bila kujiridhisha na taarifa zao.

Dr Shika ni mtu zaidi ya tunavyomfahamu, kaeleza machache kabaki na mengi, lakini machache aliyoasema yametosha kumchora picha yake halisi katika uhalisia wake. Twende na dondoo zifuatazo:

1. Masomoni Urusi na kuanzisha biashara kubwa
Achana na scholarship za siku hizi za kupeana. Wakati ule ukienda kusoma/kusomeshwa nje, wewe ni cream. Historia inaonesha Dr Shika alikuwa vizuri sana kichwani tangu sekondari, na kwa vyovyote huko Urusi alifanya vizuri pia kitu kilichowavutia wengi.

Ni baada ya kumaliza masomo yake hakurudi nchini bali alibaki Urusi na kuanzisha biashara kubwa, yeye pamoja na washirika wengine ambao asili ya kukutana kwao haiwekwi wazi. Dr. Shika yeye ndio akawa rais wa kampuni kubwa yenye mtandao wa makampuni mengi. Mafanikio ya haraka ya kampuni hii yaliwagutua Warusi na kuanza kumdukua.

2. Mafanikio ya kampuni na kumiliki mali nyingi
Kampuni yao hiyo bila kujulikana kwa hakika shughuli zao hasa ikawa ni kampuni inayokuwa kwa haraka mpaka kuwa na uwezo wa kumiliki ndege binafsi. Hapa Warusi wakashtukia mchezo kuwa pengine hawa watu ni undercover informers wa Wamarekani, na hii kampuni ni zuga tuu. Janja hii hutumiwa na mataifa mengi. Dr. Shika inapofikia hapa huwa na kigugumizi kidogo na bahati mbaya hatuna waandishi wanaojua kuhoji.

3. Kuwindwa kutekwa na mateso
Dr. Hapa kuna kitu kikubwa sana anakificha. Aliliwa timing ya muda mrefu mpaka alipokamatwa nyumbani kwake.. Inawezekana kabisa nyumba ilishakaguliwa yote. Lakini pia style ya kuondoka naye wakiwa wamemfungia kwenye kabati maana yake huyu hakuwa mtu wa kawaida.

Kwa maelezo yake alipelekwa mpaka nje ya mji Kwenye nyumba yenye chumba cha siri chini ya ardhi na kuanza kuteswa, kwa madai kwamba watekaji walitaka pesa kiasi cha USD million moja. Dr hapa pia kasema uongo kuna kitu anaficha pia. Kwa utekaji huo watekaji wangetaka awapigie simu jamaa zake wakate mpunga (ransom), lakini Dr Shika anakiri kwamba alitekwa na kuteswa na the professionals toka KGB- shirika la kijasusi la Urusi. Kwa mateso yale hawa walikuwa wanamlainisha aseme yeye ni nani hasa. Amekuwa mlemavu wa vidole vitano vya mikono. Mkono mmoja viwili, mmoja vitatu, amevunjwa mbavu tano, na sikio moja limepindishwa kwa makofi. Majambazi wanaotaka hela hawana mateso ya namna hii, haya ni mateso ili ufunguke. Roma anajua vema.

4. Ujasiri, uvumilivu na utulivu
Dr ana viashiria vyote vya majasusi, pamoja na mateso yote hayo na kujeruhiwa vibaya kabisa lakini hakupaniki wala kukata tamaa alikuwa mtulivu jasiri akisuburi one mistake one goal na akajenga nao urafiki yani hakuwa kiburi, unateswa unatukanwa unadhalilishwa unaumizwa lakini baada ya hapo unaenda nao sawa. Hii kitu ina mafunzo maalum; Dr. alikuwa mtulivu na mvumilivu mpaka akaweza kutoroka akiwa hoi kabisa.

5. Kutoroka kwake kunaacha maswali mengi, kwanini alibebwa na ndege maalum ya malkia wa Uholanzi? Je, ilikuwaje? Ni nani walifanikisha hii mipango? Kwanini Mmarekani alitoa msaada mkubwa kwake mpaka akaweza kufika nchini salama? Je, KGB walikuwa sahihi? Je, alifanikiwa kuficha siri kuu ndio maana wamarekani hawakumtupa hata sasa?

6. Vifo vya washirika wake kwenye kampuni
Wenzake karibia wote walikufa kwa kuuwawa. Yeye kaponea shimo la tewa (kuna maswali mengi sana kwenye hili kampuni lao bado lipo lakini limesimamisha shughuli zake. Wamarekani wanamsaidia Dr Shika kupata pesa zake! Kaamua kuishi nyuma ya wakati. Osama alitumia hii mbinu kwa mafanikio makubwa. Dr kaamua ku act low profile na kujitenga kabisa na harakati za dunia.

ITAENDELEA...

7. Dr. Hakuwakimbia vibaka wa Moscow, kawakimbia watu ambao ni the professional killers. Wahuni majambazi wa kupora wasingeweza kuwa na nguvu kuzidi serikali eti wamfuatilie mpaka airport ambako kwa hadhi yake na ulinzi ulivyo angeweza kulindwa mpaka anapanda jet lake na kuondoka. Na pia angepata hata wasa wa kuchukua kiasi na fedha nk. Dr aliondoshwa in rush hour tena kwa ndege maalum ya malkia. Huyu alikuwa ni zaidi ya mtu aliyetaka kuporwa pesa alikuwa ni kiungo mchezaji katika siasa na vita ya kimataifa na alikuwa anagombewa na pande mbili ama zaidi na kwa vyovyote ilikuwa ni mambo ya kijasusi na ushushushu. Na katika kuondoka huko hakuwa na muda hata wa kufungasha na kuweka mambo yake sawa ilibidi aondoke hapo hapo alipokuwa saa hiyo hiyo ili aokoe roho yake, ama abaki na akutane na kilichomtoa kanga manyoya.

8. Kurejea nyumbani Tanzania, kujificha na kujitenga kabisa na jamii
Kwakuwa anafahamu vema undani wa kisa kizima katika uhalisia wake, hata safari ya kurudi nyumbanj haikuwa ya moja kwa moja, alirudi zigzag kuwapoteza maboya watesi wake. Dr. Alikuwa anajua kwa hakika bado anatafutwa. Hivyo akawa ni mtu asiyetulia sehemu moja huku akiishi kwa kujificha na maisha ya chini hasa. Alikata mawasiliano karibia na watu wote, akatumia simu ya hali ya chini kabisa. Akakata mawasiliano na mwenza wake aliyemwacha Urusi. Alijua akimtafuta tu, wamemdaka. Mtu aliyetaka kuporwa pesa hawezi kuishi kwa kujihami kiasi hiki.

Si mtembezi hana mizunguko ya mbali zaidi ya kwenda kwenye meza ya magazeti kujua nini kinajiri, si mtembezi wa usiku na muda mwingi hujifungia chumbani kwake; hana rafiki na hana mazoea ya karibu sana na watu wengi

9. Kwanini ajitokeze sasa tena kwenye mnada mkubwa?
Kila jambo lina wakati wake na ukitimia jambo husika hujifunua. Dr alifahamu fika ule mnada ungemuweka kwenye macho ya dunia. Je, haogopi tena kufa? Je, watesi wake wamekufa wote? Nini kimemfanya ajitokeze sasa? Imethibitishwa polisi kuwa ni kweli ana pesa zake na mmarekani ndio anazishughulikia. Kwanini Mmarekani? Huyu Mmarekani huwa hafanyi kazi ya hasara hata mara moja ukiona anakushika mkono jua unamfaa na mengi; hii ishu inaweza kuwa mwanzo wa tamati yenye break through kubwa sana. Tuwe wapole tuwe na saburi.

Mwisho...

Tumjifunza mengi kwenye ishu ya Dr. Shika, hasa tabia ya kufanya vitu kwa mazoea, kuwadharau wasomi wetu eti tu kwakuwa hawana mwonekano na kuwatukuza wanasiasa wezi.

Funzo lingine ni je tunao wasomi wangapi kama Dr Shika ambao serikali haiwapi heshima na kipaumbele halafu wanatumika na mataifa mengine kiasi cha kuhatarisha maisha yao?

Je, tunao wangapi kama Dr. Shika ambao tunadhani ni machizi fresh na kuwadharau huko kwenye mishe zetu kumbe wako kazini? Jiulize Dr. Shika alivyokuwa ana act low profile kumbe ana mawasiliano na mmarekani na anafuatilia mabilioni yake? Alikuwa anawasiliana nao saa ngapi? Kwa njia gani?

Nimefarijika kuona kuwa kumbe Dr. anathamini bado elimu yetu ya kienyeji. Kubana kende unapopita kwenye mbwa wakali.

Umesikia na hiyo ya mtu aliyelala ukimuangalia usoni anaamka? Kuna siri gani hapo? Hili tutalijadili kwa leo niishie hapa ya haya machache ya Dr Shika!

NB: Nimeandika kwa muktadha wa mtazamo wangu kulingana na simulizi za mlengwa mwenyewe
RIP dk
 
Back
Top Bottom