Dkt Liki Abdallah katika Channel ten kuhusu worl cup

Dkt Liki Abdallah katika Channel ten kuhusu worl cup

acha ubahiri kama umeweza kununua sataelite dish unashindwaje kununua king'amuzi chako cha dstv kwa sh 129500/= ili ufaidi world cup
Acha kumdanganya mwenzako, we unadhani akishanunua hivyo ndio kamaliza? Si anatakiwa alipie kwa mwezi vinginevyo ataishia kuona Dish tv, kama ameshindwa kununua Startimes, DSTV ataiweza?
 
Duuuuuuh yaani huyu jamaa ni noma sana katika uchambuzi wa mpira aiseee, kwa hapa tz hakuna kama Dr. Leakey Abdallah. Mbona chanel ten kama watakua live world cup tutafaidi sana!!!!!!!!
 
Dah! aisee huyu jamaa huchoki kumsikiliza ni noma sana huyu jamaa bwana!
 
Wakuu naomba kama kuna mdau ana ratiba ya mechi zote 64 kwa saa ya EA atuwekee hapa. Maana naona kila ratiba inayotolewa inatolewa kwa saa za CUIABA na MANAUS UTC-4 na UTC-3

Ntaitupia usijali mkuu.
 
Tabu yote ya nini? Tv za kibongo ni majanga mpaka wachambuzi wa mpira nao ni hovyo tu. Kitu ni dstv tu. Kama huna nenda vibanda umiza.
 
ThumbnailServer2

Nashangaa sana huyu mchambuzi wa mpira kutokuwa TBC2 ambao ndio wenye haki ya kurusha kombe la dunia? yeye namuona channel ten katika kipindi kipya wakati channel ten hawana haki ya kurusha kombe la dunia live

lakini jamaa ni kiboko

ilikuwa zamani.............
 
nimeangalia ratiba ya chanel ten ya leo haioneshi kama kutakuwa na kuonesha kombe la dunia wameandika saa tano usiku watakuwa na kipindi cha habari
 
Wala usiwe na wasi wasi mkuu, mie najua wataonyesha na wala sitahangaika kwenda kwenye kumbi za mbali. Jamaa hawasemi direct kwa sababu nadhani wanaunga kutoka TBC2. Kama umefuatilia wanasema nafasi za matangazo ya kibiashara wakati wa kombe la dunia bado zipo ni kupeleka tu halafu wanazirusha wakati wote wa mashindano kulingana na utakavyo lipia! Sasa jiulize warusha mda gani kama si wakati wakiwa wanarusha mechi? Pia wanatangaza sana kununua ving'amzi vya statimes ili kucheki kombe la dunia kupitia TBC2. Kwa kifupi nahisi watarusha mechi zote ila watacgukulia TBC2 na wataonyesha logo ya TBC! Tusubiri tuone make ni leo tu!
nimeangalia ratiba ya chanel ten ya leo haioneshi kama kutakuwa na kuonesha kombe la dunia wameandika saa tano usiku watakuwa na kipindi cha habari
 
jamaa alifukuzwa TBC kwasababu aliwaponda wafaransa kwa kutengeneza upendeleo wa nchi za Afrika ambazo alizozitawala,katika ligi za Afrika .
Since that nchi zenye nguvu CAF ni zile zilizotawaliwa na France, akadai hata kirefu cha neno CAF ni neno la kifaransa.

Hio ndio ikawa sababu ya kupigwa chini TBC.
 
Back
Top Bottom