Dkt. James Alex Msekela ateuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia

Kabla ya hapo wanasema Msekela alikua RC Dodoma,huyu jamaa alikuwapo kipindi cha Nyuma kwani wa sasa ni Dr Rehema Nchimbi,wadau au mie cjaelewa maelezo haya?
 
Huyu bwana alikuwa mkuu wa mkoa hd septemba mwaka huu na katika uteuzi tuliambiwa amepangiwa kazi nyingine na kazi nyingine yenyewe si ndio hiyo sasa cha ajabu ni nini?pili kukosa kuchaguliwa na wananchi sio kigezo kwamba hufai mbona kina regia mtei walikosa majimbo na bado ni viongozi wetu tumewapa nafasi zingine?
 
Ficha Upumbavu wako; Usiifiche Hekima yako!
Ahsantee.gif

Thank you for supporting JF! <---(click to support us)
Waliochangia 2010: <--- (click to read)
JINSI YA KUCHANGIA JF<---(click to read)
:coffee:
24/7 Email SUPPORT: support@jamiiforums.com
 
Walimkataa wakamchagua Rage lakini Rais anamtaka!

Naona na mimi sasa niingie kwenye siasa manake ukipata utaendelea kupata. Ukikataliwa na wapiga kura kama Rais anakutaka atakuteua tu ukale bata. Ngoja nifanye haraka kabla ya katiba mpya manake naona watanzania wanataka eti kila anayeteuliwa aidhinishwe na bunge! Ikiwa hivyo hata maana ya Urais itakuwa hakuna!!

Rage alichukua nafasi ya Juma Kaboyonga kama sikosei.Halafu nilipata kusikia stori za kijiweni kwamba Dk Msekela ni rafiki mkubwa wa JK nikapuuza!Sasa nitaanza kuziamini stori za vijiweni aisee.
 
Waliosuswa na wananchi wanazidi kuonekana ''deal'' kwa mkuu wa kaya!
Mazingaombwe yanazidi kutokea nchini kila siku.

Jk hawezi kuwaacha wachafu wenzie kwa sababu hawezi kuwaweka watu watakao kuja kumpelekesha baada ya yey kutoka madarakani, ujue kumtafuta mtu msafi serikalini ni shida ni sawa na kipofu kupitisha uzi kwenye tundu la sindano
 
Waliosuswa na wananchi wanazidi kuonekana ''deal'' kwa mkuu wa kaya!
Mazingaombwe yanazidi kutokea nchini kila siku.
Hapana mkuu Maranya, swala nikuwa hao ndio wajumbe walio muingiza mkulu kwanye uongozi kwa hiyo hawezi kuwatupa hata kama wananchi hawawataki.
 
baada ya kuchoma ofisi na kufuja ujenzi wa ofisi mpya unazawadiwa kwenda kunywa mvinyo wa roma..maajab ya mgonjwa kuhonga asichomwe sindano analiwa pesa na bdo haponi.ndo tz yetu ya kulindana
 
Mkuu tuweke facts vizuri Rage in no substitute for Dr Msekela. Rage ni mbunge wa Tabora mjini. Dr Msekela was replaced by Shaffin Mamlo Sumar kuwa mbunge wa Jimbo la Tabora Kaskazini.

BTW Hongera sana Dr Msekela, japo ninasikitika kuwa tunazika utaalam wa 'High Voltage' kwenye siasa na kudunisha maendeleo but I hope you are enjoying your royal support to the then wanamtandao na sasa JK mwenyewe.

Wishing you all the best. Hoping Mgombelo anajuta kuwavuruga jamaa.
Ahsante mkuu kwa kunipa hiyo nilikuwa nimechanganya madawa! Hawa wasomi walinichanganya kidogo. Nakumbuka sasa Prof. Mgombelo alikuwepo pale TBR kisha akaja Mchumi Kaboyonga na baadaye Mzee wa Saigon! Kumbe Dr. Msekela naye ni mtu wa umeme kama Prof. Mgombelo! Hivi Prof. Mgombelo hakupewa haya ujumbe wa bodi ya TANESCO?
 
Rage alichukua nafasi ya Juma Kaboyonga kama sikosei.Halafu nilipata kusikia stori za kijiweni kwamba Dk Msekela ni rafiki mkubwa wa JK nikapuuza!Sasa nitaanza kuziamini stori za vijiweni aisee.
Kweli mkuu. Nilikuwa nimejichanganya tu.
 
Huyu bwana alikuwa mkuu wa mkoa hd septemba mwaka huu na katika uteuzi tuliambiwa amepangiwa kazi nyingine na kazi nyingine yenyewe si ndio hiyo sasa cha ajabu ni nini?pili kukosa kuchaguliwa na wananchi sio kigezo kwamba hufai mbona kina regia mtei walikosa majimbo na bado ni viongozi wetu tumewapa nafasi zingine?
Mkuu huyu Regia Mtei ni yupi tena? Au ni Regia Mtema?
 
Hapana mkuu Maranya, swala nikuwa hao ndio wajumbe walio muingiza mkulu kwanye uongozi kwa hiyo hawezi kuwatupa hata kama wananchi hawawataki.

Ni kweli mkulu hawezi kuwaacha wanamtandao hata kama wananchi watawaona hawawezi kazi
 
Waliosuswa na wananchi wanazidi kuonekana ''deal'' kwa mkuu wa kaya!
Mazingaombwe yanazidi kutokea nchini kila siku.
Mkuu mwita hivi ungekuwa wewe una madaraka ya kuteua watendaji kama madaraka aliyonayo Rais ungeacha kweli kuwateua watu WAKO ukaenda kuteua ma chasaka ama wanyamahanga? Nadhani ungeangalia walio karibu na wewe na unaowajua watakusaidia hata kama watu watawakataa lakini wewe unawaamini utasonga mbele tu! Mwita ukikwaa madaraka najua hutaniacha kwa kuwa unanijua kupitia JF!
 
baada ya kuchoma ofisi na kufuja ujenzi wa ofisi mpya unazawadiwa kwenda kunywa mvinyo wa roma..maajab ya mgonjwa kuhonga asichomwe sindano analiwa pesa na bdo haponi.ndo tz yetu ya kulindana
Mkuu kweli kuna jimoto lilitokea pale ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na kuteketeza ofisi. Hivi haikuundwa tume juu ya hilo?
 
Mkuu kweli kuna jimoto lilitokea pale ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na kuteketeza ofisi. Hivi haikuundwa tume juu ya hilo?
Kimbunga..haya majanga ya moto yanayotokea usiku ac zimezimwa na pia vifaa vingine vya ofisi vipo off ni ya kujiuliza sana..hamna petrol sigara,pasi wala mapishi! Halafu no report!
 
Back
Top Bottom