Maundumula
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 7,553
- 3,068
Vyeo vya uteuzi bongo mara nyingi wamewekewa political failures
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivi inakuaje kuna mahari nimeona uteuzi huu unaanza October 2011? anaapisha tarehe 5 January , 2011? au ni sehumu tu ya kumuongezea marupurupu baada ya kuakaaa kijiweni kwa miezi mitatu?Katika taarifa yake, Katibu Mkuu Kiongozi Sefue amesema kuwa Rais Kikwete amemteua Dkt. James Alex Msekela kuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia.
Kabla ya hapo Mheshimiwa Msekela alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
Aidha, taarifa hiyo ya Bwana Sefue imesema kuwa Rais Kikwete amemteua Bwana Ramadhani Muombwa Mwinyi kuwa Naibu Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, New York.
Kabla ya hapo, Bwana Mwinyi alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Katibu Mkuu kiongozi amesema katika taarifa yake kuwa wateuliwa hao wawili wataapishwa keshokutwa, Alhamisi, Januari 5, 2012.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
Waliosuswa na wananchi wanazidi kuonekana ''deal'' kwa mkuu wa kaya!
Mazingaombwe yanazidi kutokea nchini kila siku.
kwn nafasi walizoteulowa zinauhusiano na ukaribu kwa wananchi?
SISI-EM ina wenyewe, na wenyewe ndo hao. Hata kama wananchi watakukataa lakini ukawa ni mmoja wao ambao ndo WENYEWE( WENYE SISI-EM) mkulu atakuweka katka orodha ya WATAWALA. Maana wao wameamua kutawala na sio kuongoza.Kuna kitu huwa kinanipa shida kuelewa toka uteuzi wa mabalozi au makatibu wote wanakuwa ni wanachama wa ccm mbaya zaidi wengi wao ni wale walishindwa na kuonekani ni dhaifu na wanaccm wenyewe kwenye michakato ya uchaguzi lakini baada ya muda rais anawateua kuwa mabarozi. Barozi anawakilisha nchi nzima na mbunge anawakilisha jimbo, rais anapomteua mtu ambaye wananchi waliona hafai kuwa mbunge lakini rais anaona anafaa kuwa barozi ni udhaifu mkubwa.
Kuwa mtu wa watu unamaanisha kuwa ana ujuzi na uzoefu wa mambo ya kimataifa? mbona tunao watu wengi wenye sifa hizo, wenye uzoefu wa kutoshakatika sector hiyo. Na je kuna ulazima gani kuwa nafasi zote anazoteua raisi ziend CCM?Wana JF sijawahi kumpongeza Rais Jakaya Mrisho Kikwete, lakini kwa uteuzi ninampongeza kwani amezingatia sifa na uwezo. Dr. James Nsekela ni mtu wa watu hana makuu. Kushindwa kwake kwenye kura za maoni ni kwa sababu alikuwa anashindana na Mhindi ambaye alionga ela nyingi na hivyo kuwa mgombea kwa tiketi ya CCM.
Kweli Tabora walimkataa, lakini mamilioni wengine tunampenda. Nabii hakubaliki kwao.Huyu naye si Tabora walimkataa Ubunge?
Nimewahi kuambiwa kwamba, ubalozi hautolewi kama zawadi kama bwana mkubwa anavyofanya. Nimeambiwa kwamba kiutaratibu, mtu anatakiwa awe amefanya Wizara ya Mambo ya Nje na awe anapanda vyeo vya u-diplomasia Grade III, II, I, n.k. Sasa huyu jamaa anateua vyovyote! Tusaidieni wataalamu. Au hata mimi ninaweza kuwa balozi siku moja?Hivi inakuaje kuna mahari nimeona uteuzi huu unaanza October 2011? anaapisha tarehe 5 January , 2011? au ni sehumu tu ya kumuongezea marupurupu baada ya kuakaaa kijiweni kwa miezi mitatu?
Naona ni wale wale tu............ WALIOANDIKIWA!!!
VICIOUS CIRCLE
JK huwa ananiudhi sana anapowateua wazenji wakati wana nchi yao!
Sidhani kama kutochaguliwa kwenye ubunge ni disqualification kwa kazi nyingine za kuteuliwa. Tufahamu kuwa siasa za uchaguzi hazizingatii sifa na ubora wa wagombea. Mf. wako wabunge waliochaguliwa kwa vigezo vya kugawa ela,kanga,pombe,ukabila, udini n.k Tuwe makini tunapopinga uteuzi kwa kigezo kuwa mteuliwa alikataliwa na wananchi.