Bonifasia Mapunda: Polisi Wamwachie Dkt Slaa Bila Masharti

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
610
1,540
Tamko kuhusu ukamatwaji na kuwekwa kizuizini kwa Dkt. Willbrod Peter Slaa na wenzake.

Chama cha ACT Wazalendo kupitia Msemaji wa Sekta ya Mambo ya Ndani ya Nchini, tumepokea Taarifa ya Jeshi la Polisi Tanzania kuwashikilia wanaharakati Wakili Boniface Mwabukusu, Mpaluka Saidi Nyangali na Balozi Dkt. Wilibrod Slaa.

Tunapinga kitendo cha Jeshi la Polisi kukaa na watuhumiwa kwa zaidi ya saa 48 kinyume na sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai kifungu cha 32 kinachowataka polisi kumfikisha mtuhumiwa mahakamani au kumwachia huru ndani ya muda huo. Wakili Boniface Mwabukusu na wenzake wapo kwenye mikono ya Jeshi la Polisi tangu tarehe 11 Agosti 2023 bila kupelekwa mahakamani.

ACT Wazalendo tunaungana na wadau wengine nchini kulitaka Jeshi la Polisi kuwaachia huru na bila masharti yoyote au kuwapeleka mahakamani watanzania hao. Pia, tunarudia rai yetu ya kutaka mageuzi ya Jeshi la Polisi katika kuimarisha mfumo wa haki jinai nchini na kuondoa changamoto nyingi ambazo zinapelekea uonevu, ukandamizaji, unyanyasaji na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Imetolewa na;
Ndg. Bonifasia Aidan Mapunda
Twitter: @BonifasiaMapunda
Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani ya Nchi
ACT Wazalendo.
15 Agostii, 2023
 
Hii taarifa ni matope tu. Haijabainisha mikakati ya nn kitafanyika endapo hawatamwachia.
 
Hii taarifa ni matope tu. Haijabainisha mikakati ya nn kitafanyika endapo hawatamwachia.
unataka nao waitishe Mapinduzi ?

Ushahidi usingewekwa hadharani mngejidai kutaka ushahidi, sasa ushahidi upo hadharan mnatafuta vichaka vingine
 
unataka nao waitishe Mapinduzi ?

Ushahidi usingewekwa hadharani mngejidai kutaka ushahidi, sasa ushahidi upo hadharan mnatafuta vichaka vingine
Upo hadharani katika mahakama ipi? Au hizo clip za kukata na kutengeneza! ? Umeshahudhuria mahakama na ukafuatilia qualities za ushahidi wa kielectronic Kwa maana ya sauti, picha mnato au video na jinsi mahakama inavyoukubali au kuukataa!
 
Tamko kuhusu ukamatwaji na kuwekwa kizuizini kwa Dkt. Willbrod Peter Slaa na wenzake.

Chama cha ACT Wazalendo kupitia Msemaji wa Sekta ya Mambo ya Ndani ya Nchini, tumepokea Taarifa ya Jeshi la Polisi Tanzania kuwashikilia wanaharakati Wakili Boniface Mwabukusu, Mpaluka Saidi Nyangali na Balozi Dkt. Wilibrod Slaa...
Nyinyi wa takataka tupu, wengine wabaki ndani? stupid
 
Tangu mtoe tamko la kuunga mkono kuuza bandari nawalaani sana mbwa nyie tena nilikuwa nawaheshimu sana. Tena ondoeni neno wazalendo kwenye jina lenu maana katika siasa hakuna neno lenye thamani ya juu sana kama uzalendo. ACT Wazalendo
 
Back
Top Bottom