Dkt Bashiru amtaja Membe kwenye sakata la korosho

Kipima joto
Pesa imeisha
Uzee umekubali, duh strookuuu
 
Nina mashaka na weledi wa dr. Bashiru Ally amekuwa ni entertainer wa mwenyekiti wake anlipiga zumari Kwa ajili ya malipo kutika Kwa aliyempa zumari. Kwa taarifa yake kwenye korosho wameshafeli
1. Wakulima hawajalipwa fedha zao mpaka tarehe ya leo Mimi nikiwa mmoja wao.
2. Uhakiki wa korosho utawachukuwa sio chini ya miezi 16
3. Kangomba siyo haramu kama mnavyotaka kuwaaminisha watanzania wasioishi kusini
4. Kusuwia kangomba siyo kumtetea mkulima bali ni kumtesa Kwa kile alichokitafuta mwenyewe
Kuna mabwege ambao hawajawahi hata. Kuliona bibo watabisha,,,## Kama wanataka kuzuia kangomba walipe cash in hand naleta korosho uninipa pesa yaani mkono kwa mkono,,
 
Wenzetu wa CHADOMO wapo kama fisi leo wanamchukia John siku akipigwa chini tu na CCM anakuwa mgombea uraisi wa Saccos yao yale yale ya Lowassa lazima yatajirudia tu kati ya John au Membe mmoja lazima awe mgombea wa uraisi wa CHADOMO.
Kwani unateseka??
 
Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amekosoa kauli iliyotolewa na Bernard Membe aliyedai kuwa msomi huyo ni mgeni ndani ya chama tawala, kusisitiza kuwa anataka kuonana naye ili achote busara za waziri huyo wa zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuhusu zao la korosho

Katika maelezo yake Dk Bashiru amesema yeye ni mgeni katika timu Membe na timu ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, lakini si mgeni kwenye kanuni za CCM.

Bashiru ametoa kauli hiyo jana usiku Desemba 2, 2018 mjini Geita baada ya kumalizika kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Geita.

Kauli hiyo ya Dk Bashiru ni mwendelezo wa vita yake na Membe, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akimtaka afike ofisini kwake kujieleza.

Alitoa kauli hiyo kwa mara ya kwanza akiwa mkoani Geita, akijibu ujumbe uliotumwa kwenye akaunti ya mtandaoni ya mtu mwenye jina la Bernard Membe kujibu tuhuma zilizotolewa na Dk Bashiru akiwa Geita.

Dk Bashiru alimtuhumu Membe kuandaa mpango wa kumkwamisha Rais John Magufuli katika uchaguzi wa rais na kwamba tangu ateuliwe hajawahi kuonana na mbunge huyo za zamani wa Mtama.

Membe alieleza kushangazwa na utaratibu uliotumika kumuita akibainisha kuwa pengine ni ugeni wa kazini wa Bashiru, lakini akaahidi kwenda kumuona akirudi safari ya nje ya nchi.

Lakini jana katika majibu yake Dk Bashiru ameonekana kukerwa na kauli kuwa yeye ni mgeni kazini.

Dk Bashiru amesema tangu ateuliwe kushika wadhifa huo, amekutana na wanachama wengi, akiwemo mbunge wa Mtama, Nape Nnauye, mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe, Hawa Ghasia (Mtwara Vijijini) na kwamba wito wake kwa Membe ni kawaida na ni taratibu za CCM.

Pia, amesisitiza Membe kwenda kumuona ili ampe baraka na si mashtaka.

“Mimi simuhitaji kwa mashtaka nahitaji busara zake alikuwa mbunge kule Mtama sasa tunahangaika na korosho tunapambana na Kangomba ambayo inahusisha viongozi wa chama na Serikali, aje anipe busara tunataka kutokomeza unyonyaji kwa wakulima aje anipe busara,” amesema Bashiru.

Amesema hamzuii Membe kumjibu kwenye mitandao ya kijamii lakini majibu anayotoa yatatoa nafasi kwenye chama kumpima.

Bashiru amesema hawezi kumzungumzia mtu aliyetoa tuhuma dhidi ya Membe kwa kuwa CCM si chama cha kuzungumzia wanaharakati.

Dk Bashiru alisema wanafanya mageuzi makubwa kwenye chama kuhusu tabia hivyo wanaokosoa waendelee kukosoa lakini yeye anafanya kazi kwa mujibu wa kanuni na katiba ya chama na sio mitandao ya kijamii.

Chanzo: Mwananchi
Jiwe ana hofu kweli kweli, ni wazi jamaa wamejitathmini wanaanguka 2020
 
wapinzani wa jiwe wote ndani ya ccm wameshajisalimisha kwake kasoro kachero membe
jiwe hapati usingizi
 
Wavuja sheria na katiba ndio wanao jitangaza kufuwata sheria na katiba. Yeye mwenyekiti wake wanafikiri sheria na katiba ni midomo yao maana awamu hii kila kiongozi atakacho na kutamka ndio sheria. Awamu ya maajabu ya dunia kazi hii ngumu sana naomba mniombee. Tujenge Tanzania isiyo kiwa na vyama, kawambie wale unao waongozaongoza wasipo kaa kimya wataishia jela wakajifuze kifuwata sheria za watanzania.
 
Ana bwabwaja ..amejishtukia ...si alisema anamuita ili ajitetee kwamba anakwamisha juhudi za jiwe ..Leo imekua korosho ..
 
I hope alimuandikia barua rasmi ya kumuita kikaoni ,maana kama aliishia kumuita kwa kupitia vyombo vya habari ikiwepo hiyo mitandao, alafu aseme kua yeye anafuata kanuni za chama na si mitandao, manaake ni kwamba chama kina taratibu za kuita watu kwa kupitia vyombo vya habari...mmh!? confusion walaah!
 
Sababu za kumuita zimesha badirika mara hii? Siyo kwenda kukanusha tuhuma za kumhujumu Magufuli tena bali kuchota busara za korosho?
Hivi Bashiru ni Ke au Me?

Membe anayo nafasi nzuri sana ya kuwavuruga hawa akijua njia nzuri ya kushughulika nao.
Inaonekana Katibu Mkuu huyu ni kichwa ngumu. Aende naye taratibu tu, mradi asitifue malengo yake, kama anayo.

Kimya chake kilikuwa kizuri sana, sasa wanalazimisha kumtoa huko ili wamtafutie sababu kama hizi.

Membe asiwe na papara nao awaache wahangaike wenyewe; 'unless' kama kuna ushahidi mahususi juu yake kuhusu tuhuma za kuhujumu.
 
Watawala wana mbajambaja tu. Sasa huyo membe akiamua ku"declare interest" ofishale itakuwaje?
 
Back
Top Bottom