Mbona lugha yako imekuwa inatutatiza sisi mabasha? Uwiii uwiii uwiii ndo nini?Nani aweweseke wewe kijana mdogo veeepe ?
Naona mango inaogopa kurudi maana lupango inamhusu uwiii
Rugaramilization
Unatia kinyaa
Mbona lugha yako imekuwa inatutatiza sisi mabasha? Uwiii uwiii uwiii ndo nini?Nani aweweseke wewe kijana mdogo veeepe ?
Naona mango inaogopa kurudi maana lupango inamhusu uwiii
Rugaramilization
Sheria husika,hilo neno maadili mnalitumia vibaya sana.Huo ufundi unatakiwa pia uzingatie maadili ya uandishi wa habari.
Maadili ni suala mtambuka, kumbuka media zina mlengo na sera zao pia usidhani wanaandika kumridhisha kila mtu.
Kama hii ndio tafsiri ya uchochezi, Ndio maana pia hizi kesi hamshindi mahakamani.Media kama haijasajiliwa kama chombo cha taasisi flani, kinatakiwa kuwa "huru", na kufuata maadili. Kuandika mambo ambayo hayapo ni uchochezi.
Hakuna vita baina ya Membe na Dr. Bashiru. Labda mwandishi aje na maelezo ambayo yataonesha kuwepo kwa hiyo vita. So far huo ni upotoshaji ingawa aidhani anaandika ili auze gazeti.
Naona Gear ya reverse hiyoooSababu za kumuita zimesha badirika mara hii? Siyi kwenda kukanusha tuhuma za kumhujumu Magufuli bali kuchota busara za korosho?
Hivi Bashiru ni Ke au Me?
Ofcoz wengi tunajuwa Maembe ataangukia puwa nakutoka da mingi sana nashanga kwanii Dk kaamua funua kitendawili?Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amekosoa kauli iliyotolewa na Bernard Membe aliyedai kuwa msomi huyo ni mgeni ndani ya chama tawala, kusisitiza kuwa anataka kuonana naye ili achote busara za waziri huyo wa zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuhusu zao la korosho
Katika maelezo yake Dk Bashiru amesema yeye ni mgeni katika timu Membe na timu ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, lakini si mgeni kwenye kanuni za CCM.
Bashiru ametoa kauli hiyo jana usiku Desemba 2, 2018 mjini Geita baada ya kumalizika kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Geita.
Kauli hiyo ya Dk Bashiru ni mwendelezo wa vita yake na Membe, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akimtaka afike ofisini kwake kujieleza.
Alitoa kauli hiyo kwa mara ya kwanza akiwa mkoani Geita, akijibu ujumbe uliotumwa kwenye akaunti ya mtandaoni ya mtu mwenye jina la Bernard Membe kujibu tuhuma zilizotolewa na Dk Bashiru akiwa Geita.
Dk Bashiru alimtuhumu Membe kuandaa mpango wa kumkwamisha Rais John Magufuli katika uchaguzi wa rais na kwamba tangu ateuliwe hajawahi kuonana na mbunge huyo za zamani wa Mtama.
Membe alieleza kushangazwa na utaratibu uliotumika kumuita akibainisha kuwa pengine ni ugeni wa kazini wa Bashiru, lakini akaahidi kwenda kumuona akirudi safari ya nje ya nchi.
Lakini jana katika majibu yake Dk Bashiru ameonekana kukerwa na kauli kuwa yeye ni mgeni kazini.
Dk Bashiru amesema tangu ateuliwe kushika wadhifa huo, amekutana na wanachama wengi, akiwemo mbunge wa Mtama, Nape Nnauye, mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe, Hawa Ghasia (Mtwara Vijijini) na kwamba wito wake kwa Membe ni kawaida na ni taratibu za CCM.
Pia, amesisitiza Membe kwenda kumuona ili ampe baraka na si mashtaka.
“Mimi simuhitaji kwa mashtaka nahitaji busara zake alikuwa mbunge kule Mtama sasa tunahangaika na korosho tunapambana na Kangomba ambayo inahusisha viongozi wa chama na Serikali, aje anipe busara tunataka kutokomeza unyonyaji kwa wakulima aje anipe busara,” amesema Bashiru.
Amesema hamzuii Membe kumjibu kwenye mitandao ya kijamii lakini majibu anayotoa yatatoa nafasi kwenye chama kumpima.
Bashiru amesema hawezi kumzungumzia mtu aliyetoa tuhuma dhidi ya Membe kwa kuwa CCM si chama cha kuzungumzia wanaharakati.
Dk Bashiru alisema wanafanya mageuzi makubwa kwenye chama kuhusu tabia hivyo wanaokosoa waendelee kukosoa lakini yeye anafanya kazi kwa mujibu wa kanuni na katiba ya chama na sio mitandao ya kijamii.
Chanzo: Mwananchi
Jiwe akimsikia Bashiru kuwa anataka busara za Membe!
Ina maana kwa tafsiri nyingine Mzee baba hawezi kuongoza nchi hivyo watahitaji mawazo ya Membe ili kujikwamua na mkwamo
NDO MAANA YAKE MZE WASAIDIZI WAMEMCHOKA
Vita vipo labda kama umevaa miwani ya mbao, kitendo cha Katibu mkuu kjibizana maneno mitandaoni na wanachama wake tayari ni vita ya maneno, ndiyo maana kaambiwa ni mgeni hajui utaratibu wa chama.
Mpaka mwisho wa duniaMimi nilifikiri suala la korosho lilishaisha. Kumbe bado kuna tatizo licha ya mapesa kutolewa kwa wakulima.
Hivi hawa wakulima watabebwa mpaka lini?