Dkt Bashiru amtaja Membe kwenye sakata la korosho

Dkt Bashiru amtaja Membe kwenye sakata la korosho

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
21,852
Reaction score
29,579
Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amekosoa kauli iliyotolewa na Bernard Membe aliyedai kuwa msomi huyo ni mgeni ndani ya chama tawala, kusisitiza kuwa anataka kuonana naye ili achote busara za waziri huyo wa zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuhusu zao la korosho

Katika maelezo yake Dk Bashiru amesema yeye ni mgeni katika timu Membe na timu ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, lakini si mgeni kwenye kanuni za CCM.

Bashiru ametoa kauli hiyo jana usiku Desemba 2, 2018 mjini Geita baada ya kumalizika kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Geita.

Kauli hiyo ya Dk Bashiru ni mwendelezo wa vita yake na Membe, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akimtaka afike ofisini kwake kujieleza.

Alitoa kauli hiyo kwa mara ya kwanza akiwa mkoani Geita, akijibu ujumbe uliotumwa kwenye akaunti ya mtandaoni ya mtu mwenye jina la Bernard Membe kujibu tuhuma zilizotolewa na Dk Bashiru akiwa Geita.

Dk Bashiru alimtuhumu Membe kuandaa mpango wa kumkwamisha Rais John Magufuli katika uchaguzi wa rais na kwamba tangu ateuliwe hajawahi kuonana na mbunge huyo za zamani wa Mtama.

Membe alieleza kushangazwa na utaratibu uliotumika kumuita akibainisha kuwa pengine ni ugeni wa kazini wa Bashiru, lakini akaahidi kwenda kumuona akirudi safari ya nje ya nchi.

Lakini jana katika majibu yake Dk Bashiru ameonekana kukerwa na kauli kuwa yeye ni mgeni kazini.

Dk Bashiru amesema tangu ateuliwe kushika wadhifa huo, amekutana na wanachama wengi, akiwemo mbunge wa Mtama, Nape Nnauye, mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe, Hawa Ghasia (Mtwara Vijijini) na kwamba wito wake kwa Membe ni kawaida na ni taratibu za CCM.

Pia, amesisitiza Membe kwenda kumuona ili ampe baraka na si mashtaka.

“Mimi simuhitaji kwa mashtaka nahitaji busara zake alikuwa mbunge kule Mtama sasa tunahangaika na korosho tunapambana na Kangomba ambayo inahusisha viongozi wa chama na Serikali, aje anipe busara tunataka kutokomeza unyonyaji kwa wakulima aje anipe busara,” amesema Bashiru.

Amesema hamzuii Membe kumjibu kwenye mitandao ya kijamii lakini majibu anayotoa yatatoa nafasi kwenye chama kumpima.

Bashiru amesema hawezi kumzungumzia mtu aliyetoa tuhuma dhidi ya Membe kwa kuwa CCM si chama cha kuzungumzia wanaharakati.

Dk Bashiru alisema wanafanya mageuzi makubwa kwenye chama kuhusu tabia hivyo wanaokosoa waendelee kukosoa lakini yeye anafanya kazi kwa mujibu wa kanuni na katiba ya chama na sio mitandao ya kijamii.

Chanzo: Mwananchi
 
Jiwe akimsikia Bashiru kuwa anataka busara za Membe!

Ina maana kwa tafsiri nyingine Mzee baba hawezi kuongoza nchi hivyo watahitaji mawazo ya Membe ili kujikwamua na mkwamo wa korosho.
 
Mwanzo Dr Bashiru alisemakua anamuita ili AKAKANUSHE TUHUMA dhidi yake za kupanga mikakati ya kumkwamisha MH JPM ndani ya chama. Sasa anasema amemuita ili AMPATIE BUSARA YA ZAO LA KOROSHO.[emoji53] [emoji18]

Au ndo tuseme nshakua kichwa tikikiti kama DAB kuhusu kuelewa maelezo (Ya awali na Ya sasa).[emoji57]
 
jamaa(bashiru) anaweweseka balaa,,kama msukule yan....hii imenikumbusha jamaa yangu mmoja alipigwa tu ngumi ya kawaida ila akikuhadithia anasema alipigwa na panga kama sio nondo...maana ake ile ngumi ilifika mahala pake...dadeki.
 
Vita vipo labda kama umevaa miwani ya mbao, kitendo cha Katibu mkuu kjibizana maneno mitandaoni na wanachama wake tayari ni vita ya maneno, ndiyo maana kaambiwa ni mgeni hajui utaratibu wa chama.
Huko upinzani ndiko huwa mnakuwa na vita , huku ni mwendo wa kukumbushana taratibu na kanuni za chama. Bado mna muda wa kujifunza.
 
Kuna kitu kikubwa kinaendelea baina ya wakubwa. Ni kitu kikubwa sana na yawezekana wengi hatujajua hata robo ya kinachoendelea. Hii namna ya Dkt Bashiru kuwasiliana na Mh Membe ni ya namna ya kuchekesha na kushangaza. Binafsi inaniwia vigumu kuamini kuwa kiongozi mkuu wa chama kongwe anaweza asiwe na tel no ya prominent CCM member kama Membe; angeweza hata kuipata toka kwa Kinana au Nape.

Kuna mchezo wa siasa unachezwa hapa ambao iko Siku utaivua nguo CCM. Anyway, wacha waparurane tu.
 
Back
Top Bottom