Dkt Bashiru amtaja Membe kwenye sakata la korosho

Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amekosoa kauli iliyotolewa na Bernard Membe aliyedai kuwa msomi huyo ni mgeni ndani ya chama tawala, kusisitiza kuwa anataka kuonana naye ili achote busara za waziri huyo wa zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuhusu zao la korosho

Katika maelezo yake Dk Bashiru amesema yeye ni mgeni katika timu Membe na timu ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, lakini si mgeni kwenye kanuni za CCM.

Bashiru ametoa kauli hiyo jana usiku Desemba 2, 2018 mjini Geita baada ya kumalizika kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Geita.

Kauli hiyo ya Dk Bashiru ni mwendelezo wa vita yake na Membe, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akimtaka afike ofisini kwake kujieleza.

Alitoa kauli hiyo kwa mara ya kwanza akiwa mkoani Geita, akijibu ujumbe uliotumwa kwenye akaunti ya mtandaoni ya mtu mwenye jina la Bernard Membe kujibu tuhuma zilizotolewa na Dk Bashiru akiwa Geita.

Dk Bashiru alimtuhumu Membe kuandaa mpango wa kumkwamisha Rais John Magufuli katika uchaguzi wa rais na kwamba tangu ateuliwe hajawahi kuonana na mbunge huyo za zamani wa Mtama.

Membe alieleza kushangazwa na utaratibu uliotumika kumuita akibainisha kuwa pengine ni ugeni wa kazini wa Bashiru, lakini akaahidi kwenda kumuona akirudi safari ya nje ya nchi.

Lakini jana katika majibu yake Dk Bashiru ameonekana kukerwa na kauli kuwa yeye ni mgeni kazini.

Dk Bashiru amesema tangu ateuliwe kushika wadhifa huo, amekutana na wanachama wengi, akiwemo mbunge wa Mtama, Nape Nnauye, mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe, Hawa Ghasia (Mtwara Vijijini) na kwamba wito wake kwa Membe ni kawaida na ni taratibu za CCM.

Pia, amesisitiza Membe kwenda kumuona ili ampe baraka na si mashtaka.

“Mimi simuhitaji kwa mashtaka nahitaji busara zake alikuwa mbunge kule Mtama sasa tunahangaika na korosho tunapambana na Kangomba ambayo inahusisha viongozi wa chama na Serikali, aje anipe busara tunataka kutokomeza unyonyaji kwa wakulima aje anipe busara,” amesema Bashiru.

Amesema hamzuii Membe kumjibu kwenye mitandao ya kijamii lakini majibu anayotoa yatatoa nafasi kwenye chama kumpima.

Bashiru amesema hawezi kumzungumzia mtu aliyetoa tuhuma dhidi ya Membe kwa kuwa CCM si chama cha kuzungumzia wanaharakati.

Dk Bashiru alisema wanafanya mageuzi makubwa kwenye chama kuhusu tabia hivyo wanaokosoa waendelee kukosoa lakini yeye anafanya kazi kwa mujibu wa kanuni na katiba ya chama na sio mitandao ya kijamii.

Chanzo: Mwananchi
hiki kijamaa mnakiita bashiru mbona kijinga kiasi hiki?........

kamwita membe kupitia mitandao, then anasema hafanyi kazi kupitia mitandao!!!!.......

huyu nina wasiwasi phd yake ni ya kuhonga!...... mbona kichwani ni mweupe hivi?
 
Mbona wana hofu wakati bado mapema sana, jamaa yuko kimya wanaweweseka je siku akisema itakuwaje.

Ni Mtz mbumbumbu tu ambayde hawezi kujua kinachoendelea hapa!
Hizi chokochoko za MEMBE na BASHIR ni vita ya MAGUFULI na WAGOMBEA WOTE WA URAIS MWAKA 2015: MEMBE,JANUARI,MIGIRO,NCHIMBI na MADELU kwa upande wa CCM na LOWASA upinzani!
Ukiangalia kwa jicho la tatu Magufuli anekuwa akiwashughulikia hawa walokuwa wapinzani wake kwenye Urahisi kwa staili tofautitafauti kulingana na nguvu waliyonayo ndani na nje ya chama!
Chama kimeshikwa na MANYANG'AU YA CCM....!!!
 
Mimi nilifikiri suala la korosho lilishaisha. Kumbe bado kuna tatizo licha ya mapesa kutolewa kwa wakulima.

Hivi hawa wakulima watabebwa mpaka lini?
Tuliambiwa Wakulima wamepiga hadi magoti kumsifu mtukufu kwa kununua korosho zao kwa bei nzuri, kumbe bado kuna matatizo?
 
hiki kijamaa mnakiita bashiru mbona kijinga kiasi hiki?........

kamwita membe kupitia mitandao, then anasema hafanyi kazi kupitia mitandao!!!!.......

huyu nina wasiwasi phd yake ni ya kuhonga!...... mbona kichwani ni mweupe hivi?
Dovutwa ana nafuu kubwa sana !
 
Tuliambiwa Wakulima wamepiga hadi magoti kumsifu mtukufu kwa kununua korosho zao kwa bei nzuri, kumbe bado kuna matatizo?
hajatoa hata senti 5 kipande ! wanasubiri Rostam atoe hela !
 
Huko upinzani ndiko huwa mnakuwa na vita , huku ni mwendo wa kukumbushana taratibu na kanuni za chama. Bado mna muda wa kujifunza.
Ukute anayechangia ana kadi ya 1977 kabla ya wewe kujiunga. Check namba.
 
Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amekosoa kauli iliyotolewa na Bernard Membe aliyedai kuwa msomi huyo ni mgeni ndani ya chama tawala, kusisitiza kuwa anataka kuonana naye ili achote busara za waziri huyo wa zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuhusu zao la korosho

Katika maelezo yake Dk Bashiru amesema yeye ni mgeni katika timu Membe na timu ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, lakini si mgeni kwenye kanuni za CCM.

Bashiru ametoa kauli hiyo jana usiku Desemba 2, 2018 mjini Geita baada ya kumalizika kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Geita.

Kauli hiyo ya Dk Bashiru ni mwendelezo wa vita yake na Membe, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akimtaka afike ofisini kwake kujieleza.

Alitoa kauli hiyo kwa mara ya kwanza akiwa mkoani Geita, akijibu ujumbe uliotumwa kwenye akaunti ya mtandaoni ya mtu mwenye jina la Bernard Membe kujibu tuhuma zilizotolewa na Dk Bashiru akiwa Geita.

Dk Bashiru alimtuhumu Membe kuandaa mpango wa kumkwamisha Rais John Magufuli katika uchaguzi wa rais na kwamba tangu ateuliwe hajawahi kuonana na mbunge huyo za zamani wa Mtama.

Membe alieleza kushangazwa na utaratibu uliotumika kumuita akibainisha kuwa pengine ni ugeni wa kazini wa Bashiru, lakini akaahidi kwenda kumuona akirudi safari ya nje ya nchi.

Lakini jana katika majibu yake Dk Bashiru ameonekana kukerwa na kauli kuwa yeye ni mgeni kazini.

Dk Bashiru amesema tangu ateuliwe kushika wadhifa huo, amekutana na wanachama wengi, akiwemo mbunge wa Mtama, Nape Nnauye, mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe, Hawa Ghasia (Mtwara Vijijini) na kwamba wito wake kwa Membe ni kawaida na ni taratibu za CCM.

Pia, amesisitiza Membe kwenda kumuona ili ampe baraka na si mashtaka.

“Mimi simuhitaji kwa mashtaka nahitaji busara zake alikuwa mbunge kule Mtama sasa tunahangaika na korosho tunapambana na Kangomba ambayo inahusisha viongozi wa chama na Serikali, aje anipe busara tunataka kutokomeza unyonyaji kwa wakulima aje anipe busara,” amesema Bashiru.

Amesema hamzuii Membe kumjibu kwenye mitandao ya kijamii lakini majibu anayotoa yatatoa nafasi kwenye chama kumpima.

Bashiru amesema hawezi kumzungumzia mtu aliyetoa tuhuma dhidi ya Membe kwa kuwa CCM si chama cha kuzungumzia wanaharakati.

Dk Bashiru alisema wanafanya mageuzi makubwa kwenye chama kuhusu tabia hivyo wanaokosoa waendelee kukosoa lakini yeye anafanya kazi kwa mujibu wa kanuni na katiba ya chama na sio mitandao ya kijamii.

Chanzo: Mwananchi
Dr. Bashiru anaelekea kuwa mtu wa hovyo sasa, heri Wilson Mukama!
 
Majibu ya kitoto sana ndio Nchi ipate maendeleo kutoka kwa watu wa aina ya Bashiru kazi ipo mpaka muda mwingine unajiuliza mbona maneno hayaendani na u Dr sijui uprof walionao...
 
Namuita ili anipe "busara." Ukishaona mtu anabadilisha sababu basi ujue kuwa hiyo ni dalili ya kuufyata.
 
Back
Top Bottom